Mwaka 2037 nitakua tajiri wa kwanza Afrika

nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,733
6,970
Sina kipaji cha kuandika sana ila nitaeleza kwa ufupi.

Ni ukweli usiopingika kwamba kila mtu ana ndoto za kuwa tajiri. Pia nimejifunza kuwa utajiri sio bahati nasibu. Ili kuufikia utajiri unahitaji kufuata hatua za utajiri.

Nimeamua kufuata hatua za utajiri na nina uhakika nitaufikia. Najua wengi mtakuja kwa kunibeza nakusema naota ndoto za mchana. Ila ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2037 nitakua na utajiri wa ajabu.

Nataka niseme kitu hapa. Ili uwe tajiri ni lazima uwe na plan za muda mrefu. Miaka 20 Si mchezo na hiyo hiyo ni michache sana kama utauchezea muda. Kwa upande wangu nimejipanga na ninajua ni vikwazo gani nitapitia.

Na endapo sitakua hai kufika kipindi hicho, nimeweka mpango madhubuti wa kuhakikisha vizazi vyangu vinafanikisha hili jambo.

Nimeandaa urithi wa elimu ya hiki ninachokifanya ambacho kitawapa mwanga wa kuendeleza na kutimiza ndoto zangu

Ni hayo tu. Tukutane mwaka 2037
 
Hakuna malengo ya kuwa wa kwanza kushinda wote kwenye utajiri huo ni uchizi na ROHO MBAYA pia.

malengo yako we weka tu na yafanyie kazi na ikiwa utakuwa wa kwanza au wa mwisho kwenye utajiri hiyo haijalishi.
 
That is only possible if you are a Forex Trader...
Really? Yaani uwe Forex Trader TU ndio unaweza kuwa na Utajiri wa kufikia namba moja afrika mnamo 2037. Hebu twambie matajiri wa Top 10 Africa na utwambie kama wanafanya forex trading... Hii kitu naona mnaipigia kampeni sana.....
 
Sina kipaji cha kuandika sana ila nitaeleza kwa ufupi.

Ni ukweli usiopingika kwamba kila mtu ana ndoto za kuwa tajiri. Pia nimejifunza kuwa utajiri sio bahati nasibu. Ili kuufikia utajiri unahitaji kufuata hatua za utajiri.

Nimeamua kufuata hatua za utajiri na nina uhakika nitaufikia. Najua wengi mtakuja kwa kunibeza nakusema naota ndoto za mchana. Ila ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2037 nitakua na utajiri wa ajabu.

Nataka niseme kitu hapa. Ili uwe tajiri ni lazima uwe na plan za muda mrefu. Miaka 20 Si mchezo na hiyo hiyo ni michache sana kama utauchezea muda. Kwa upande wangu nimejipanga na ninajua ni vikwazo gani nitapitia.

Na endapo sitakua hai kufika kipindi hicho, nimeweka mpango madhubuti wa kuhakikisha vizazi vyangu vinafanikisha hili jambo.

Nimeandaa urithi wa elimu ya hiki ninachokifanya ambacho kitawapa mwanga wa kuendeleza na kutimiza ndoto zangu

Ni hayo tu. Tukutane mwaka 2037
Akina Dr Shika kumbe mpo wengi nchi hii! Asa hizo plans na resources zitakazokupa huo utajiri ziko wapi?
 
Binafsi nakuelewa 100% labda uwe huna nia ya dhati na nidhamu ya hali ya juu.Lakini hayo yote yako katika uwezo wako.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom