Mwaka 2030

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Najaribu kujiuliza hali na mabadiliko yatakayokuwepo mwaka 2030 duniani hasa hapa Tanzania mwaka huo nitakuwa mtu mzima ambaye nimestaafu kwa mujibu wa sheria wakati huo rais mstaafu Kikwete atakuwa na umri wa miaka 80 rais wa awamu ya tatu Mkapa atakuwa na 92 na Mzee Ruksa wakati huo atakuwa amegonga 105 kamili

wakati huo Chama cha mapinduzi kitatimiza miaka 53 umri wa kuelekea uzeeni kitakuwepo lakini kitakuwa kimechoka sana nafikiria vyama vya upinzani vitakuwa vimepukutika na kubaki vitatu vingine ni majina tu kwenye daftari la msajili wakati huo si Tendwa tena

wakati huo serikali itakuwa ya mseto wa vyama vinne CCM-A, CCM-B, Chadema na CUF bunge litakuwa na sura mpya kabisa zingine hata kutoka JF members nafikiria Spika wa bunge atatoka nje ya vyama atakuwa mbunge toka mgombea binafsi

wakati huo mtoto wangu atakuwa na miaka 15 atakuwa mdadisi kweli nafikiria siku moja ataniuliza eti baba nasikia Lowassa ni baba wa Taifa, kwa nini, tumeambiwa shuleni; hapana baba wa Taifa alikuwa Nyerere alifariki kabla wewe hujazaliwa

ataniuliza tena eti baba nasikia mlima Kilimanjaro ulikuwa Tanzania; kwani sasa uko wapi atanijibu East African Federation atakuwa amenikumbusha kwani wakati huo hatutakuwa na rais wa Tanzania ataniuliza tena eti Loliondo... na Muungano ulivu................weee nenda kalale kesho shule hapo itabidi niwe mkali.

Jamani wana JF tumekuwa tukijikumbusha sana mambo yaliyopita ya enzi zileeee hatuwezi kujaribi angalau kubashiri kidogo mambo yajayo hata tukipatia au kukosea kwa 50% inatosha.
 
293avjt.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom