Mwaka 2025: Selemani Jaffo ni mgombea wa CCM urais(?)

Mtoa mada badilisha mwaka weka 2020 sio 2025 tafadhali. Hatutakivumilia hiki chama kurudi tena 2020 hata wawepo kina jecha 20. Tutapiga kura za "kishetani" vilevile kama nyie mnavyotufanya mashetani kwa sasa.
 
mtoa mada kama una kipaji cha utabiri jitangaze upige pesa kama akina sheikh yahya
Siyo kutabiri ni kupata fursa ya kujua yajayo, pasico alisema lazima ajaye ni KATTO, watu waka puuza, sasa ajaye anajulikana
 
Ni pale ambapo huwa namtafuta mchora ramani wa CCM na kugundua kuwa watakuwa wana nguvu ya ziada ,
Kwa kuwa ni mapema mno na ndo Mheshimiwa ana mwaka mmoja madarakani, ni kawaida ya CCM kujitokeza watu wa kugombea nafasi za juu na maandaliz huanza mapema mno,

Tetesi za utaratibu unaosukwa mpaka najiuliza sana kuwa nani hasa uwa anawashauri katika masuala haya, maana mnapoanza kuhisi wameishiwa wanakuwa na mtu mpya ambaye ni wa kushangaza ambaye hakutegemewa,

Nilitamani nitaje jina lake lakin naona nisije nikasababisha akaanza kuchafuliwa na timu mbali mbali zinazosaka madaraka, nimeainisha kifupi tu cha jina lake , kuwa ndiye atakaye shika wadhifa wa juu baada ya uongozi wa Mh tuliyenaye, kutokana na habari za karibu nilizonazo zimeonesha kuwa mpango wa kumuandaa kijana Huyo kujiandaa kisaikolojia kwa awamu ijayo,

Miongozo na mienendo aliyopewa kijana huyo ni siri ambazo hapaswi kuzijua mwingine,

Sifa zake zilizoina haraka haraka
1. Ni msomi
2. Mtaratibu mwenye maamuzi sahihi
3. Afya njema na mungu tunaomba amlinde sana
4. Ni dini Fulani ambayo sitaki kuitaja,
6. Ni wa kanda ile ya upande unaoonekana kupata marais wengi kutoka.upande uo,
7. Si msemaji ni mtendaji tu.
8. Ni mtiifu kwa wananchi

Safari imeanza, sasa, asante jopo la wazee 13 kuendelea kutuletea vijana na kuwaandaa


Jikiteni kufanya kazi ili kuleta maendeleo binafsi na nchi pia, tumsaidie raisi kwa kufanya kazi, tuache majungu na uvivu na tamaa za kipumbavu, ni uwendawazimu ya hali ya juu kuanza kupanga safu za kipuuzi sasahivi, Kwanza kwa taarifa yako Mh Magufuli hawezi kukubali upuuzi huo, mtu ambaye ameingia serikalini kujijenga kisiasa binafai na si kufanya kazi ya kumsaidia raisi huyo hana nafasi ni wa kutumbua tu,
 
Atakayeweza kupumbaza watu sasa hivi kutoka ccm ni HM tu; wengine wote ccm wajiandae kufanya wizi mkubwa.

Watanzania wamejifunza ubaya wa kuwa na mkuu mkurupukaji, bora tuendelee na wapole wetu maana maendeleo ni safari tutafika tu hata miaka bilioni ijayo.
HM nani huyu Hussein Mwinyi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom