Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,154
- 10,809
Kwa jinsi Rais Magufuli anavyokwenda ,na kwa kuzingatia anavyoichekecha nchi kila kona ,mwaka 2025 natarajia kuona maandamano makubwa kutoka kwa watu hawa
1.Wamachinga, mama ntilie na boda boda.
Bila kupepesa macho makundi tajwa hapo juu kwenye utawala wa rais Magufuli wanaishi kifalme. Wanafanya biashara zao katikati ya jii na miji mikubwa bila bugudha yoyote ,mpaka wamepewa vitambulisho .Kwa kuzingatia haya makundi haya hayatakubali Magufuli aondoke madarakani 2025, hivyo wataitisha maandamano makubwa kushinikiza mabadiliko ya katiba ili rais Magufuli aendelee kukaa madarakani .
Hofu yao ya kutaka Magufuli aendelee kukaa madarakani inasababishwa na kwamba hawajui yule anayekuja ataweza kuwajali ,huenda wakaanza kufukuzwa tena na kumwagiwa vyakula vyao kama zamani.
2. Wakulima na wafugaji.
Bila shaka yoyote wakulima wa mazao yote wamenufaika mno na utawala wa rais Magufuli ,wakulima wa pamba, korosho ,kahawa ,wanakula kwa mrija tu .
Wafugaji nao wamefutiwa kodi mbalimbali za kero zaidi ya 17 ! Kama mnakumbuka kulikuwa na kodi hadi za kwato mnadani.!
Hivyo kundi hili nalo bila shaka halitakubali rais Magufuli aondoke madarakani ,hivyo kuitisha maandamano makubwa ya kumtaka Magufuli aendelee kuwa rais kwa miaka 20 zaidi.
3 Akina na mama na sekta ya afya kwa ujumla .
Rais Magufuli amewajengea vituo vya afya zaidi ya 360 na hospitali za wilaya 66 nchi nzima.
Kwa hiyo akina mama stori za kujifungulia mabarabarani na kukosa huduma bora za afya zimeisha kwenye enzi za utawala wa rais Magufuli. Hivyo kundi hili halitakubali rais Magufuli aondoke madarakani hivyo wataitisha maandamano makubwa kumshikiza abaki.
4. Itaendelea.....