Mwaka 2021, wapinzani bado wataongoza kwenye uteuzi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,979
Tunaanza utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi katika maeneo mengi hii ikiwa ni baada yakuitimishwa kwa uchaguzi mkuu nchini.

Mwaka 2015 hadi 2020 viongozi waandamizi wa chama tawala walielekeza nguvu zao kubomoa upinzani kwa kauli mbiu ya kuunga mkono. Kupitia mradi huu, wapinzani wengi hasa vijana waliokuwa wanaushawishi wa kisiasa ila hawana ajira walifanikiwa kuajiriwa mara tu walipotangaza kujiunga Ccm.

Kitendo Cha kuwapa ajira wapinzani na kuwaacha wanachama wa ccm kiliwakera wajumbe na ilipofika 2020 wajumbe kwa kauli moja waliwafyeka zaidi ya asilimia 90 ya wale waliounga mkono juhudi. Hii ilikuwa ishara tosha kwa viongozi wa ccm kwamba wanachama wamekwazika na awakufurahi kuona upinzani unakabidhiwa madaraka huku wenye ccm wakiachwa.

Aidha, katika kampeni wananchi walionekana wazi kutokukubaliana na chama Tawala kutoka na aina ya siasa zao.

Tumeanza mwaka mpya 2021 ambao ni mwaka wa Kwanza baada ya uchaguzi. Je tutaendelea kutumia nguvu kupambana na vyama vya upinzani ikiwemo chadema au tutakiimarisha chama chetu tawala? Je, vijana wa upinzani watapewa kipaumbele kwenye ajira zinazohusu uteuzi?

Naomba uwe mwaka wakuona Kama lipo lesson learned kutoka previous 5 years au bado tunawaza vilevile? Happy new year Tanzania
 
Lazima upinzani waendelee kuongoza kuteuliwa. Maana CCM kimejaa makopo nani anafaa kuteuliwa kule?
 
Wapinzani walishinda ila wakapokwa kwa hiyo wacha wapewe vyeo kwani ni vchwa. Kweli weli!
 
Mimi sio nabii,ila suphian juma atateuliwa Na johnbaptist ataachwao
 
Kitendo Cha kuwapa ajira wapinzani na kuwaacha wanachama wa ccm kiliwakera wajumbe na ilipofika 2020 wajumbe kwa kauli moja waliwafyeka zaidi ya asilimia 90 ya wale waliounga mkono juhudi. Hii ilikuwa ishara tosha kwa viongozi wa ccm kwamba wanachama wamekwazika na awakufurahi kuona upinzani unakabidhiwa madaraka huku wenye ccm wakiachwa.
Tatizo mnakariri sana.

Waitara unasema mpinzani?Alikua ccm,akaenda chadema akarudi nyumbani.

Katambi ni mpinzani?alipokua bavicha,alikua ni msaidizi wa Anthony Diallo!
 
Samahani, Magufuli alikuwa mpinzani ndani ya ccm na serekali ya Jakaya. Na ni wazi Magufuli amejipanga kuwa chama wapinzani.

Sintashangaa nikijasikia Lissu amejiunga CCM, na ndiyo mgombea uraisi mtarajiwa kupitia ccm.

Hi inaitwa transformation of the highest caliber.
 
Beatrice tupiamo picha basi maana kina bite mnakuwaga pisikali tena ww mhaya hapo guu guu daaaaadadeki... eehe mada ilikua inasema bitewangu??
 
Tunaanza utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi katika maeneo mengi hii ikiwa ni baada yakuitimishwa kwa uchaguzi mkuu nchini...
Hii kitu siipendi sana, nchi hii linapokuja swala la kujenga nchi hakuna upinzani wala utawala, kama hakuna mwenye hati miliki yake, ndio maana ni kawaida kukuta mtu leo yupo ACT kesho chadema ,na ata CCM, na anapohama sehemu moja kwenda nyingine,maneno ni kuwa wale sio wakweli, hawaitakii mema nchi.

Sasa kwavile lengo ni kujenga unaweza kutoa nafasi kwa yule aliedhani unakosea, mfano yupo Mwanaccm ,Bashe, ambaye alikuwa mkosoaji mzuri, amepewa nafasi pale akafanye anachoamini , ata kuwaweka watu waliokuwa wapinzani kwenye serikali ni kwa falsafa hiyo, hivyo ni ujinga kusema wapinzani wamepewa, kwa maana hakuna mwenye hati miliki ya upinzani unless uwe muasisi wa chama Hicho.
 
Hii kitu siipendi sana, nchi hii linapokuja swala la kujenga nchi hakuna upinzani wala utawala, kama hakuna mwenye hati miliki yake, ndio maana ni kawaida kukuta mtu leo yupo ACT kesho chadema ,na ata CCM, na anapohama sehemu moja kwenda nyingine,maneno ni kuwa wale sio wakweli, hawaitakii mema nchi...
Unajisahaulisha tulupoambiwa WAPINZANI WANACHELEWESHA MAENDELEO?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom