Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Utafiti wa hali ya joto duniani na mashirika mawili ya Marekani umeonyesha kuwa mwaka 2021 umeshika nafasi ya sita wenye joto zaidi duniani.
Takwimu za hivi karibuni zilizokusanywa na Shirika la taifa la Marekani linaloshughulikia utafiti wa anga za mbali, NASA na Idara ya Bahari na Anga ya Marekani, NOAA zinasisitiza kuhusu mzozo wa hali ya hewa duniani.
Kulingana na NASA, mwaka 2021 umefungana na mwaka 2018 kwa nafasi ya sita ambayo hutumia kipindi cha miaka 30.
Uchambuzi tofauti wa NOAA umeonyesha wastani wa hali ya joto kwa mwaka 2021 ulikuwa na nyuzi joto 1.51 za kipimo cha Celsius juu ya viwango vya karne ya 20, na kuufanya mwaka uliopita kuwa katika nafasi ya sita, mbele ya mwaka 2018.
Maafisa wamesema hiyo ni sehemu ya hali ya joto ya muda mrefu ambayo inaonyesha dalili za kuongezeka kasi.
DW Swahili