Mwaka 2021 ni mwaka ambao umenifanya ni experience na kujifunza vitu vingi

Tobechukwu

Senior Member
Oct 15, 2018
112
415
Habari zenu wakuu, natumai wote mpo salama kabisa, ila kwa mwenye matatizo Mungu awasaidie.

Tukiwa tunaelekea kumaliza huu mwaka 2021 nimshukuru tu Mungu kwanza kufika mpaka hapa leo, maana bila yeye sijui ningekuwa wapi.

Mwaka 2021 ni mwaka ambao umenifanya ni experience na kujifunza vitu vingi mno kuhusu mahusiano, pesa na familia.

Niliyojifunza ni kama ifiatavyo:

1) KUMTANGULIZA MUNGU KWENYE KILA KITU NINACHOFANYA NA KUMSHUKURU KWA KILA JAMBO.

Kuna nguvu kubwa sana katika kumshirikisha Mungu kila kitu na kurelax kumwacha afanye, nikiri kuna muda nilikuaga naona kama haniskii vile au hajibu najifanya kutumia akili mwisho naangukia pua tu, na badala nishukuru kila jambo nakuwa nalalamika tu, ila namshukuru Mungu nimevuka hapa siku hizi nasema tu na aliyeniumba natulia nikiamini atajibu na anajibu.

2) KUJIPA FURAHA MWENYEWE.

Hapa sasa nilikuaga kama kayatima yani, najiweka ki kutia tia huruma nikitegemea furaha niipate toka kwa wengine hasa mpenzi wangu, ila nilipokuja kugundua kuwa kila mtu anajijali mwenyewe nikaacha huo ujinga, nikajifunza kujitoa out, kujinunulia zawadi nikiona nimeboreka najipeleka mahali nikaenjoy na sitaki company ya mtu naenjoy company yangu.

3)KUTOKUSHIRIKISHA WATU MAMBO YANGU.

Mimi huwa napenda sana privacy japo kuna mda unajikuta umekaa na rafiki ako anaongea vyake nawewe unajikuta unaanza kusema vyako kussoport lol, na sio marafiki tu hata ndugu lakini mwisho wa siku yanageuka mengine, hapa nimejifunza kukaa na vitu vyangu moyoni hata iweje ongea yako mi sisemi yangu ng'oo.

4) KUTOKUPANGA PLAN ZAKUFANYA BIASHARA NA MPENZI.

Hapa nilipigwa na kitu kizito nikajifunza mpenzi sio mtu wa kusema mpange oooh tufungue biashara mara kiwanja tununue, nduugu mapenzi yanaishaga na yakiisha ndo umeliwa hapo usifkiri hela itarudi.
Hizo mambo nitakujaga kufanya na mume wangu nikiolewa ila mpezi hapana tena.
Wapenzi wanaofanikiwaga hapa ni wawili kati ya mia.

5) KUTOKUJALI SANA WENGINE.

Hapa nashukuru nimebadilika kama sio kuacha kabisa. Mimi ni wale watu nilikua radhi niumie mimi nikiamini kesho nitapata tena ili mwingine afurahi tu, lol ikija zamu yangu sasa nikiwa nina shida sipati msaada popote napambana na hali yangu, nikaona ujinga huu kwanzia sasa nitajiweka mimi mbele kabla ya mtu mwingine bora nionekane mbaya.

6) KUWA BAHIRI.

Ukitaka kufanikiwa haya maisha kuwa bahiri.
Mimi nilikua mtu wa kutoa toa jamani mtu akiomba hela huyo shwaaa nishampa kiroho safi naona fresh tu mkono utoao ndo upokeao, ila nilipoona pia anayepokea hachoki kuomba kilasiku anarudi kwavile anajua zipo zinatoka tu, saivi mtu akiniomba hela namimi naanza kulia shida kama yeye.

7) KUTOKUPENDA SANA

Hapa nimejifunza kutokuja kumpenda mtoto wa mtu kuliko ninavyojipenda mimi, maana nishapendaga sana nikaishiaga kuangukia pua tu nikiamini kumuonyesha mtu upendo atatulia lakini waaaapi holaaa, nikiwa na mtu nitakuwepo tu ila sitaki sumbuaana na mtu kulilia kuonyeshwa upendi wala kumganda mtoto wa mtu kujifanya najua kupenda.

Ni mengi mno nimejifunza il hayo naona ni makubwa kwangu kwamba ningejifunza mapema kuna vitu ningekwepa kwa huu mwaka, ila Mungu mwema anatupa nafasi ya kuanguka na kujifunza kikubwa uzima tunakuwa na nafasi ya kutengeneza upya.

Mungu akinivusha salama naamini 2022 utakua mwaka mzuri sana kwangu.
Niwatakie heri ya mwaka mpya mvuke salama.
 
WELL UPO RIGHT KWA KIASI FULANI....

ENDELEA KUWA ANTI SOCIAL TU

ACHA DHARAU KIBURI NA MAJIGAMBO HIVYO VITU HUISHAA

JITENGE NA WATU KAMA USEMAVYO, KESHO NA KESHOKUTWA UTAKUJA KUWAHITAJI WATU HAO HAO UNAOJITENGA NAO

Maisha haya yana namna nyingi ya kukuprove wrong, usijiwekee limit kuwa kitu fulani hakitatokea kwangu...who knows?
 
UNAZINGUA SASA WE JOSE, SINA DHARAU NA SIPENDI DHARAU IWE KUMDHARAU MTU AU MTU ANIDHARAU, SASA HAPO DHARAU NA KUJIGAMBA UMEVIONEA WAPI? KUNA WATU MNABOAA
 
UNAZINGUA SASA WE JOSE, SINA DHARAU NA SIPENDI DHARAU IWE KUMDHARAU MTU AU MTU ANIDHARAU, SASA HAPO DHARAU NA KUJIGAMBA UMEVIONEA WAPI? KUNA WATU MNABOAA
Kisaikolojia nimekutest kupitia hiyo reply nimehisi something is not right

kuna tatizo lipo kwako halafu ni mbishi kulikubali na kusonga mbele, punguza hivyo utakuwa sawa ndugu yangu

Kuwa na amani hata sijakudharau, kubali changamoto unazopitia zifanyie kazi kwa kujifunza utafanikiwa mwaka 2022

Naweza kuwa nakuboa ndio ila jitafakari na sio kwa ubaya wala nini kwa uzuri tu

RELAX, CHIILL AND TAKE IT EASY... Usichukulie kila kitu so serious saana, life is too short!

Barikiwa mpendwa na Mungu akuvushe uuone mwaka 2022!
 
Tuvuke wote
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom