Mwaka 2020 upinzani utapata tabu sana kuandaa Ilani zao za Uchaguzi

Nyie mlioshindwa kuongeza mishahara ndio wa kututisha; nyinyi mnaokata 15% ya mshara kulipia mikopo ya Bodi ndio wananchi wawachague; nyinyi mnaoshindwa kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati ndio wenye sera za kuvutia wapiga kura?

Nyinyi mnaoshindwa kulipa mafao kwa wakati; mlioshindwa kukamata watu wasiojulikana; mliotekeleza kilimo; mlioamua kuchukua hela za wakulima wa korosha; mlioshindwa kuajiri vijana wanaomaliza vyuo vikuu, n.k ndio wenye sera za nzuri za kutisha wapinzani?

Nyinyi wenye sera za kibaguzi za utoaji wa mikopo; nyinyi mlioshindwa kutekeleza ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji; nyinyi mlioshindwa kueleza umma zilipo shilingi trilioni 1.5.nyinyi wenye tuhuma za kununua madiwani na wabunge;

Nyinyi wenye kuminya uhuru wa watu kutoa maoni; nyinyi wenye kuonekane kwenye tv mkikimbia na masanduku ya kura; nyinyi mliozuia Bunge live, nyinyi mnaosema katiba mpya sio kipaumbele chenu, nyinyi mnaobeza na kukejeli maandiko ya viongozi wa dini;

Nyinyi mliofukuza watumishi wenye vyeti feki huku Bashite mkimbeba, nyinyi mlioshindwa kuweka hadharani mahesabu ya ATCL, n.k nani mwenye akili timamu atawachagua?
Point noted
 
Nimewaza sana,
Chaguzi zilizotangulia, Vyama vya upinzani nchini vilitumia sana changamoto za kisiasa, Kiuchumi na Kijamii zilizokuwa zikiikabili nchi yetu katika kuandaa ilani za Uchaguzi za vyama vyao.

1. Huduma duni za Afya, Elimu, Umeme,Maji, barabara zilikuwa ni changamoto sana awamu zilizopita.
2. Mfumuko wa bei, uzembe kazini, miungu watu kwenye taasisi za Umma, unyanyasaji wa wafanyabiashara ndogo ndogo(Mama ntilie, Bodaboda, Wamachinga
) , watu kunyang'anywa mali zao(Mashamba, nyumba, viwanja) ni mambo ambayo yalikuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa kawaida.
3. Ufisadi, rushwa, ukwepaji kodi halikadhalika yalikuwa na matatizo sugu nchini.
4. Matumizi mabaya ya rasimali za taifa(Madini, Gesi, misitu, Mbuga za Wanyama) vilevile kwa muda mrefu yamekuwa donda ndugu.
5. Kukosekana kwa uwekezaji wenye kujenga uchumi endelevu wa taifa kama Ndege, Reli, Umeme ni miongoni mwa mambo ambayo waliumiza sana vichwa vya viongozi wetu bila ya mafanikio.
Wapinzani walitumia changamoto hizi kuwaonesha wananchi kuwa Serikali inayoongozwa na CCM kwa vipindi vyote ilifikia kikomo na isingeweza kukabiliana na changamoto hizi. Ilani za Vyama hivi zimekuwa zikizimulika changamoto hizi.
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Bulldozer, Jiwe, Watapata tabu sana, Dkt. John Pombe Magufuli imedhihirisha kwa vitendo ndani ya kipindi cha miaka miwili na nusu kuwa inawezekana. Wote wanaobeza namna Serikali hii inavyokabiliana na changamoto hizi, wanatapatapa tu, wengine wanaukubali utekelezaji huu ila wanafanya propaganda tu japo nao waendelee kuonekana kuwa wapo lakini kimsingi kisiasa wamefilisika.
Natafakari tu, 2020 wapinzani watakuwa na kipi cha kuandika kwenye ilani zao.
umeandika mengi lakini hujasema
kwenye sekta ya afya idadi ya vifo vya mama na mtoto umepungua kwa kiasi gani kabla ya kusifia.
ubora wa elimu sio kwa maana ya watoto wanaoandikisha hapana nazungumzia ubora ( quality) je watt wa tz watakuwa na uwezo waa kushindaana na wale wa nchi nyingine kama kenya? au wale wa shule yingine za humu humu?
maisha ya watumishi wa umma sio wabunge yatakuwa yameimarika kwa kiwango gani?
zile 1.5 trilion zitakuwa zimepatikana?
je mtakuwa mmeacha kuwaita watengeneza ndege ikulu na kuwapa specifications?
kiwango cha umasikini cha watanzania kitakuwa kimepungua kwa kiasi gani?
yapo mengi ila ukipenda kusifiwa upende pia kukosolewa na wapinzani kazi yao sio kuisifia serikali hapana wao wapo kwa ajili ya kunyoosha njia ili serikali itende. kuwa mpinzani sionuadui .kama ule wa kufikia hata kumpoka mzee dr. slaa mkewe lakini leo anaonekana lulu kisa kaongoka.
 
Nchi za Ulaya na Amerika kuna wapinzani na tunafata siasa zao,Nadhal kwa maendeleo walofikia kusingekua na upinzani mana hata ilani ingeliwahinda.
Karne ya 21 unazungumzia maendeleo ya misosi miwili kwa siku na kutatua changamoto za utapia mlo?
 
Wenye akili wanajua ni heri mishahara isipande lakini bei ya unga ikabaki palepale badala kuliko kuongezewa mshahara shililingi 10000 lakini sukari,unga, chumvi vikapaa bei. Ndiyo maana naona 2020 mtapata tabu sana kama hoja zenu ni dhaifu kiasi hiki
Kwa nguvu ya Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya wanaobadirishwa kila kukicha .......... CCM lazima ipete tu.

Kwa hali ilivyo 2020 hakuna uchaguzi bali kutangaza matokeo tu kwa kufuata maelekezo .... Hiyo ni kuanzia ndani ya chama!!
 
Furaha yenu mbowe atoke mpandikize mtu wenu mfanye kama mlivyofanya kwa cuf, hell no
Mbowe hana madhara tena, tangu amuuzie Lowassa Chama, CCM wanataka aendelee kuwepo sana huyo mzee wa kubadili gia angani
 
Kwa nguvu ya Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya wanaobadirishwa kila kukicha .......... CCM lazima ipete tu.

Kwa hali ilivyo 2020 hakuna uchaguzi bali kutangaza matokeo tu kwa kufuata maelekezo .... Hiyo ni kuanzia ndani ya chama!!
Haya ni maneno ya kutapatapa kiukweli 2020 mtapata tabu sana.
 
Mimi ni chadema lakini kwa sasa ccm inanguvu nahisi ni muda wao umefika kwakweli tutapata tabu sana
 
Back
Top Bottom