Mwaka 2020 upinzani utapata tabu sana kuandaa Ilani zao za Uchaguzi

ccm imechokwa kila sehemu. wamebaki kutegemea polis na kubebwa na tume tu basi. kule iringa mjini mkurugenzi na watendaji kata wanashirikiana kuwahujumu wagombea wa chadema kwa kuwanyima fomu ili wasiteuliwe kugombea ili mgombea wa ccm apite bila kupingwa.pia kuwateka wagombea.
Upinzani tunataka kushika dola wakati harata kufuata Sheria za uchaguzi hatuzifuati
 
Hao wapinzani nao wakikosa cha kusema itabidi waachane na siasa, tena tusiwape ruzuku zetu kabisa, japo hata sasa hamna justification ya matumizi yake kwani hawafanyi siasa wakati ruzuku wanapewa. Back to the point, yakusema yapo mengi sana kwani changamoto nyingi bado zipo sema tu taarifa hazitoki. Mwezi juzi nilipita Mwanza, Pamba secondary nikashuhudia watoto wengi wamekaa kwenye matofali!!.....
 
Ujinga ni mzigo kuliko umasikini
Hakika.
Sijajua anaongelea barabara za wapi huyu UVCCM. Mkoa wa Kigoma kwa mfano, tangu upate uhuru haujaunganishwa na mikoa mingine kwa lami mpaka ninavyoongea na hakuna mpango wowote wa kufanya hivyo. Ni mbaya sana kufikiria kwamba Tanzania nzima iko kama Lumumba Dar. Kuhusu maji, Dar ndio sina hata la kusema. Watu wnakunywa majitaka na kujaharishia kila leo.
 
Hao wapinzani nao wakikosa cha kusema itabidi waachane na siasa, tena tusiwape ruzuku zetu kabisa, japo hata sasa hamna justification ya matumizi yake kwani hawafanyi siasa wakati ruzuku wanapewa. Back to the point, yakusema yapo mengi sana kwani changamoto nyingi bado zipo sema tu taarifa hazitoki. Mwezi juzi nilipita Mwanza, Pamba secondary nikashuhudia watoto wengi wamekaa kwenye matofali!!.....
Hiyo ccm unayoiabudu ndio unaona chama cha siasa?!
 
Wanadamu wengine uwezo wa kufikiri ni mdogo sana, hivi kuna nchi gani duniani imemaliza matatizo ya wananchi wake? hata America na Scandinavia bado hawajamaliza matatizo yao seuze sisi ulimwengui wa tatu?

Nakupa mada za kuongea wakati wa kampeni za upinzani
1) kurudisha uhuru kwa wananchi especially wa kujieleza
2) kurudisha utawala wa sheria
3) kuzuia vitendo vya mauaji ya ovyo
4) kuzuia unyanyasaji wa taasisi za dini
5) kurudisha bunge kuoneshwa live
6) Kufuta sheria ya mitandao inayowanyanyasa watu
7) Kurejesha mchakato wa katiba mpya.
Halafu unakuja umebana pua eti wapinzani hawana cha kuongea? Give me a break
 
kwani wapinzani sio wananchi..kwani upinzani haukubaliki Tanzania..kwani katiba imefuta mfumo wa vyama vingi? Tukubaliane tu kwamba wananchi wanyonge watazidi kupata shida Zaidi..
 
Nimewaza sana,
Chaguzi zilizotangulia, Vyama vya upinzani nchini vilitumia sana changamoto za kisiasa, Kiuchumi na Kijamii zilizokuwa zikiikabili nchi yetu katika kuandaa ilani za Uchaguzi za vyama vyao.

1. Huduma duni za Afya, Elimu, Umeme,Maji, barabara zilikuwa ni changamoto sana awamu zilizopita.
2. Mfumuko wa bei, uzembe kazini, miungu watu kwenye taasisi za Umma, unyanyasaji wa wafanyabiashara ndogo ndogo(Mama ntilie, Bodaboda, Wamachinga
) , watu kunyang'anywa mali zao(Mashamba, nyumba, viwanja) ni mambo ambayo yalikuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa kawaida.
3. Ufisadi, rushwa, ukwepaji kodi halikadhalika yalikuwa na matatizo sugu nchini.
4. Matumizi mabaya ya rasimali za taifa(Madini, Gesi, misitu, Mbuga za Wanyama) vilevile kwa muda mrefu yamekuwa donda ndugu.
5. Kukosekana kwa uwekezaji wenye kujenga uchumi endelevu wa taifa kama Ndege, Reli, Umeme ni miongoni mwa mambo ambayo waliumiza sana vichwa vya viongozi wetu bila ya mafanikio.
Wapinzani walitumia changamoto hizi kuwaonesha wananchi kuwa Serikali inayoongozwa na CCM kwa vipindi vyote ilifikia kikomo na isingeweza kukabiliana na changamoto hizi. Ilani za Vyama hivi zimekuwa zikizimulika changamoto hizi.
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Bulldozer, Jiwe, Watapata tabu sana, Dkt. John Pombe Magufuli imedhihirisha kwa vitendo ndani ya kipindi cha miaka miwili na nusu kuwa inawezekana. Wote wanaobeza namna Serikali hii inavyokabiliana na changamoto hizi, wanatapatapa tu, wengine wanaukubali utekelezaji huu ila wanafanya propaganda tu japo nao waendelee kuonekana kuwa wapo lakini kimsingi kisiasa wamefilisika.
Natafakari tu, 2020 wapinzani watakuwa na kipi cha kuandika kwenye ilani zao.
Mbona zipo nyingi sana mkuu, ambazo zinaudhi na kukera wananchi,
 
Back
Top Bottom