Mwaka 2020 upinzani utapata tabu sana kuandaa Ilani zao za Uchaguzi

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Nimewaza sana,
Chaguzi zilizotangulia, Vyama vya upinzani nchini vilitumia sana changamoto za kisiasa, Kiuchumi na Kijamii zilizokuwa zikiikabili nchi yetu katika kuandaa ilani za Uchaguzi za vyama vyao.

1. Huduma duni za Afya, Elimu, Umeme,Maji, barabara zilikuwa ni changamoto sana awamu zilizopita.
2. Mfumuko wa bei, uzembe kazini, miungu watu kwenye taasisi za Umma, unyanyasaji wa wafanyabiashara ndogo ndogo(Mama ntilie, Bodaboda, Wamachinga
) , watu kunyang'anywa mali zao(Mashamba, nyumba, viwanja) ni mambo ambayo yalikuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa kawaida.
3. Ufisadi, rushwa, ukwepaji kodi halikadhalika yalikuwa na matatizo sugu nchini.
4. Matumizi mabaya ya rasimali za taifa(Madini, Gesi, misitu, Mbuga za Wanyama) vilevile kwa muda mrefu yamekuwa donda ndugu.
5. Kukosekana kwa uwekezaji wenye kujenga uchumi endelevu wa taifa kama Ndege, Reli, Umeme ni miongoni mwa mambo ambayo waliumiza sana vichwa vya viongozi wetu bila ya mafanikio.
Wapinzani walitumia changamoto hizi kuwaonesha wananchi kuwa Serikali inayoongozwa na CCM kwa vipindi vyote ilifikia kikomo na isingeweza kukabiliana na changamoto hizi. Ilani za Vyama hivi zimekuwa zikizimulika changamoto hizi.
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Bulldozer, Jiwe, Watapata tabu sana, Dkt. John Pombe Magufuli imedhihirisha kwa vitendo ndani ya kipindi cha miaka miwili na nusu kuwa inawezekana. Wote wanaobeza namna Serikali hii inavyokabiliana na changamoto hizi, wanatapatapa tu, wengine wanaukubali utekelezaji huu ila wanafanya propaganda tu japo nao waendelee kuonekana kuwa wapo lakini kimsingi kisiasa wamefilisika.
Natafakari tu, 2020 wapinzani watakuwa na kipi cha kuandika kwenye ilani zao.
 
Hawa jamaa leo watakutukana sana, hawatakagi kuambiwa maneno yanayowachoma
Nyie mlioshindwa kuongeza mishahara ndio wa kututisha; nyinyi mnaokata 15% ya mshara kulipia mikopo ya Bodi ndio wananchi wawachague; nyinyi mnaoshindwa kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati ndio wenye sera za kuvutia wapiga kura?

Nyinyi mnaoshindwa kulipa mafao kwa wakati; mlioshindwa kukamata watu wasiojulikana; mliotekeleza kilimo; mlioamua kuchukua hela za wakulima wa korosha; mlioshindwa kuajiri vijana wanaomaliza vyuo vikuu, n.k ndio wenye sera za nzuri za kutisha wapinzani?

Nyinyi wenye sera za kibaguzi za utoaji wa mikopo; nyinyi mlioshindwa kutekeleza ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji; nyinyi mlioshindwa kueleza umma zilipo shilingi trilioni 1.5.nyinyi wenye tuhuma za kununua madiwani na wabunge;

Nyinyi wenye kuminya uhuru wa watu kutoa maoni; nyinyi wenye kuonekane kwenye tv mkikimbia na masanduku ya kura; nyinyi mliozuia Bunge live, nyinyi mnaosema katiba mpya sio kipaumbele chenu, nyinyi mnaobeza na kukejeli maandiko ya viongozi wa dini;

Nyinyi mliofukuza watumishi wenye vyeti feki huku Bashite mkimbeba, nyinyi mlioshindwa kuweka hadharani mahesabu ya ATCL, n.k nani mwenye akili timamu atawachagua?
 
Nyie mlioshindwa kuongeza mishahara ndio wa kututisha; nyinyi mnaokata 15% ya mshara kulipia mikopo ya Bodi ndio wananchi wawachague; nyinyi mnaoshindwa kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati ndio wenye sera za kuvutia wapiga kura?

Nyinyi mnaoshindwa kulipa mafao; mlioshindwa kukamata watu wasiojulikana; mliotekeleza kilimo; mlioamua kuchukua hela za wakulima wa korosha; mlioshindwa kuajiri vijana wanaomaliza vyuo vikuu, n.k ndio wenye sera za nzuri za kutisha wapinzani?

Nyinyi wenye sera za kibaguzi za utoaji wa mikopo; nyinyi mlioshindwa kutekeleza ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji; nyinyi mlioshindwa kueleza umma zilipo shilingi trilioni 1.5.nyinyi wenye tuhuma za kununua madiwani na wabunge;

Nyinyi wenye kuminya uhuru wa watu kutoa maoni; nyinyi wenye kuonekane kwenye tv mkikimbia na masanduku ya kura; nyinyi mliozuia Bunge live, nyinyi mnaosema katiba mpya sio kipaumbele chenu, nyinyi mnaobeza na kukejeli maandiko ya viongozi wa dini;

Nyinyi mliofukuza watumishi wenye vyeti feki huku Bashite mkimbeba, nyinyi mlioshindwa kuweka hadharani mahesabu ya ATCL, n.k nani mwenye akili timamu atawachagua?
Wenye akili wanajua ni heri mishahara isipande lakini bei ya unga ikabaki palepale badala kuliko kuongezewa mshahara shililingi 10000 lakini sukari,unga, chumvi vikapaa bei. Ndiyo maana naona 2020 mtapata tabu sana kama hoja zenu ni dhaifu kiasi hiki
 
Wapinzani wanatakiwa kujipanga upya na wafanye maamuzi magumu kama kuuondoa uongozi wa juu ambao ndio umewafikisha hapo.
Hilo wao hawalioni kama ni tatizo na kuendelea kuona mchawi ni CCM? Watapata tabu sana 2020
 
Nimewaza sana,
Chaguzi zilizotangulia, Vyama vya upinzani nchini vilitumia sana changamoto za kisiasa, Kiuchumi na Kijamii zilizokuwa zikiikabili nchi yetu katika kuandaa ilani za Uchaguzi za vyama vyao.

1. Huduma duni za Afya, Elimu, Umeme,Maji, barabara zilikuwa ni changamoto sana awamu zilizopita.
2. Mfumuko wa bei, uzembe kazini, miungu watu kwenye taasisi za Umma, unyanyasaji wa wafanyabiashara ndogo ndogo(Mama ntilie, Bodaboda, Wamachinga
) , watu kunyang'anywa mali zao(Mashamba, nyumba, viwanja) ni mambo ambayo yalikuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa kawaida.
3. Ufisadi, rushwa, ukwepaji kodi halikadhalika yalikuwa na matatizo sugu nchini.
4. Matumizi mabaya ya rasimali za taifa(Madini, Gesi, misitu, Mbuga za Wanyama) vilevile kwa muda mrefu yamekuwa donda ndugu.
5. Kukosekana kwa uwekezaji wenye kujenga uchumi endelevu wa taifa kama Ndege, Reli, Umeme ni miongoni mwa mambo ambayo waliumiza sana vichwa vya viongozi wetu bila ya mafanikio.
Wapinzani walitumia changamoto hizi kuwaonesha wananchi kuwa Serikali inayoongozwa na CCM kwa vipindi vyote ilifikia kikomo na isingeweza kukabiliana na changamoto hizi. Ilani za Vyama hivi zimekuwa zikizimulika changamoto hizi.
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Bulldozer, Jiwe, Watapata tabu sana, Dkt. John Pombe Magufuli imedhihirisha kwa vitendo ndani ya kipindi cha miaka miwili na nusu kuwa inawezekana. Wote wanaobeza namna Serikali hii inavyokabiliana na changamoto hizi, wanatapatapa tu, wengine wanaukubali utekelezaji huu ila wanafanya propaganda tu japo nao waendelee kuonekana kuwa wapo lakini kimsingi kisiasa wamefilisika.
Natafakari tu, 2020 wapinzani watakuwa na kipi cha kuandika kwenye ilani zao.
Sasa watapata tabu gani nchi ni moja na kinachotakiwa ni kuinua mtanzania was hali ya chini naw apande just na miundo mbinu iwepo ya uhakika ccm wakifanya vizuri wanafanya kwa ajili ya watanzania wakikosea wanaambiwa. Hata ww uwezi kuwa kama mm lazima tutofautiane katika mawazo. Muda mwingine kaa na kuwaza ili uweze kujua unaandika nn. Ondoa mawazo ya kiccmccm. Tanzania ni ya watanzania siyo ya chadema Wala ccm. Na watu wa kuisaidia Tanzania ni sisi wenyewe ila wenzetu mnachanganyikiwa mkionyeshwa mwekundu wa msimbasi yaani akili zenu huruka na kuisahau Tanzania
 
ccm imechokwa kila sehemu. wamebaki kutegemea polis na kubebwa na tume tu basi. kule iringa mjini mkurugenzi na watendaji kata wanashirikiana kuwahujumu wagombea wa chadema kwa kuwanyima fomu ili wasiteuliwe kugombea ili mgombea wa ccm apite bila kupingwa.pia kuwateka wagombea.
 
Back
Top Bottom