Mwaka 2019 utakuwa mgumu sana kimaisha. Tuchukue tahadhari

Haya ni maoni na tafakuri yangu.

Iwe ulilia kwa sauti na kububujikwa na machozi mengi au ulililia tumboni na kuvaa tabasamu danganyifu mwaka huu wa 2018, kilio zaidi kwa mwaka 2019 .

Mwaka 2019 Tutarajie haya:

1) Misaada mingi ya wahisani kupungua sana kama sio kukwama.

2) Mapato mengi ya serikali kutumika kulipia miradi ya maendeleo inayoendelea kujengwa kama SGR, Stiglers Gorge, Ujenzi wa Meli, Kununua Ndege na Miundo mbinu

3) Kupanda kwa gharama za nishati ya mafuta na usafiri kama ilivyoanza kuonekana hivi sasa.

4) Kuporomoka kwa thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine.

5) Ukosefu wa ajira rasmi - Hakutakuwa na ajira mpya.

6) Anguko kubwa la Sekta binafsi ambayo ndio inaajiri theluthi mbili ya watanzania wenye ajira rasmi.

7) Matumizi mapya ya serikali haswa uchaguzi wa serikali za mitaa nakadhalika.

8) Kuanguka kwa sekta ya kilimo ambako kutatokana na anguko la bei ya mazao na uzalishaji kama inavyojionesha katika kanda zinazozalisha mazao kipindi hiki cha vuli.

Ni vizuri Watanzania wakajua yajayo na yatarajiwayo ili wachukue tahadhari zinazofaa - KNOWLEDGE IS POWER

Heri ya mwaka mpya 2019 Watanzania wote
..inaelekea mwaka 2019 ndo ulitunga usemi usemao yajayo yanafurahisha je uko tayari?
 
Back
Top Bottom