Mwaka 2019 umemalizika huku Tanzania na Dunia ikishuhudia mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana nchini Tanzania

Papaa Muu

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
243
292
Ni dhahiri uchapakazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli umeonyesha mabadiliko makubwa ya kiutendaji ya ambapo tumeshuhudia hadi kufikia Mwezi Mei mwaka 2019, Hospitali za Rufaa za Mikoa zilikuwa na jumla ya Watumishi 8,443 huku upatikanaji wa dawa muhimu ambazo ni aina 30 katika hospitali za rufaa za mikoa ukifikia asilimia 93.

Licha ya upatikanaji huo wa dawa wa uhakika, pia tunashuhudia maduka ya madawa yakiwa na dawa za kutosha huku huduma za bima ya afya zikiendelea kuimarika kwenye maeneo mengi nchini.

Katika kuhakikisha sekta hiyo inaimarika, Serikali imenunua mashine 8 za kidigitali za x-ray na kupelekwa katika Hospitali za rufaa za mikoa ya Ruvuma, Morogoro, Simiyu, Singida, Njombe, Kagera, Amana na Katavi.

Upatikanaji wa mashine hizo umeongeza ubora wa matibabu kutokana na uchunguzi sahihi sahihi wa magonjwa ya Binaadamu.

Mambo haya yanapatikana kwa haraka hususan katika kipindi hiki cha Serikali inayosimamiwa na Rais Magufuli, kwani takwimu zinaonyesha kuwa kulikuwa na kusuasua kwa ujenzi wa maeneo ya huduma za kijamii, na sasa tunaona faida za kuwa na kiongozi shupavu na imara kwani kusua sua huko hakupo tena.

Katika kuhakikisha gharama za matibabu nje ya nchi zinapungua na kuondoka kabisa, Serikali kwa nia ya dhati kabisa imedhamiria kuimarisha huduma hizo nchini ili kuokoa fedha nyingi za matibabu nje ya nchi.

Inasikitisha kuona kuwa wapo baadhi ya watu wanaobeza juhudi hizi, watanzania hatuna budi kuwaacha nasi tukasonga mbele katika kumpa moyo na sapoti kubwa Rais wetu ambaye amedhamiria kuokoa maisha ya watanzania.

Tulishududia ufisadi mkubwa katika awamu zilizopita, watu kujilimbikizia mali pasipo kuwa na huruma na watanzania.

Hali mbaya za hospitali zetu, miundombinu mibovu, huduma mbovu za afya ni miongoni mwa mambo yaliyokuwepo enzi hizo ambayo sasa imekuwa ni historia.

Migomo ya madaktari na watumishi wengine wa afya kutokana na kudai maslahi yao jambo ambalo lilisababisha ndugu zetu wengi kupoteza maisha, tena wagonjwa wasiokuwa na hatia Sasa haipo tena.

Inasikitisha na inaumiza sana kuona ndugu na jamaa zetu wakipoteza maisha kutokaba na migomo hiyo, lakini kwa sasa jambo hilo limekuwa ni historia.

Suala la afya sio la kulifanyia mchezo hata kidogo, afya ni suala ambalo halina mjadala, hakuna mbadala wa afya, yaani mtu akiumwa anahitaji huduma nzuri na za haraka ili aweze kupona na kuendelea na majukumu mengine ya kulijenga Taifa, na ndio maana Rais anafanya kazi kubwa ya kuhakikisha maisha bora na huduma nzuri za afya zinapatokana wakati wote.

Kwa upande wa fani za kibingwa kuna Madaktari 170 kati ya Madaktari 1,120 wanaohhitajika ukilinganisha na Madaktari Bingwa 138 waliokuwepo Novemba 2017.

Aidha Serikali pia imeanza ujenzi wa hospitali za rufaa za mikoa mipya ya Songwe, Katavi, Njombe, Geita na Simiyu ambapo ujenzi huo upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na imeshatoa zaidi ya shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kumamilisha ujenzi wa hospitali hizo za mikoa mipya.

Mambo yote haya yanafanywa na Rais wetu, Jemedari wetu, mpendwa wetu Dkt John Pombe Magufuli.

Mungu akupe afya njema na azidi kukutunza, Rais wetu na nakutakia heri ya mwaka mpya wa 2020.

Ni Mimi John Mwakilasa-Mbeya
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Hajatutakiwa heri ya mwaka mpya 2020 mim nina wasiwasi kama huu mwaka utakuwa wa heri kwake kwa sababu katususa na hatupendi sisi watanzania
 
December 31, 2019
Dar-es-Salaam, Tanzania

State of the Nation Address 2019 by Zitto Kabwe, Leader of ACT- Wazalendo party (Tanzania)

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo akitoa hotuba yake ya mwisho wa mwaka 2019 kuelekea mwaka mpya 2020. Ambapo alitumia fursa hiyo kubainisha hali ya Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na Geopolitics ambayo kwa kifupi Taifa chini ya utawala wa CCM imeidumaza na kubinya si uchumi tu bali hata haki na maendeleo ya watu

Source: MwanaHALISI TV
 
Umesema Tulishududia ufisadi mkubwa katika awamu zilizopita, watu kujilimbikizia mali pasipo kuwa na huruma na watanzania. hivi hao mafisadi kwa sasa wameokoka ehee! au wamepumzika mana nilifikiri wangerudisha pesa zetu kama zakayo wa kwenye biblia.
 
Back
Top Bottom