Mwaka 2019 ulivyokuwa na mafanikio ya Bima ya Afya

Papaa Muu

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
243
292
Mwaka 2019 ulivyokuwa na mafanikio ya bima ya afya

Na John Mwakilasa-Mbeya

Kabla sijaanza kusema ninachokusudia kusema, naomba nitoe angalizo! Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa wala Sina itikadi hizo.

Mwaka 2013 nilikuwa na bima ya afya ambayo niliikata kwa gharama kubwa sana, lakini nilipopatwa na homa sikuweza kupata huduma zinazostahili.

Kila kipimo nililazimika kukilipia hali iliyonipa tabu sana, sikuitamani tena huduma hiyo ya bima ya afya.

Na hii ilitokana na usimamizi mbovu wa sekta ya afya, kwani suala langu nililifikisha mpaka kwa waziri mwenye dhamana ya afya wa wakati huo lakini suala langu halikupata ufumbuzi.

Nilikata tamaa kabisaaa, sikuitaka tena huduma hiyo ya bima ya afya kwani niliona nalazimika kulipia huduma mara mbili.

Miaka mitano baadae nikamsikia Rais wangu Dkt Magufuli akituhakikishia watanzania kuwa huduma za bima Sasa zimeimarika, nilijishauri nikaona ni wakati muafaka nijaribu tena kulipia bima ya afya, sijajuta!

Kama kuna mtu hana bima ya afya kwa sababu kama zangu nilizozitaja hapo juu Sasa ni wakati muafaka wa kutumia huduma hizo.

Nazifurahia sana kwani pesa yangu inatumika kwa huduma nzuri na za uhakika.

Nilimsikia Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF Bernard Konga akisema wamefanikiwa kuanzisha taratibu mbalimbali zinazowapa fursa wananchi wa makundi mbalimbali kujiunga na huduma zake hatimaye kuwa na huduma za matibabu wakati wote na mahali popote nchini.

Taratibu hizo ni pamoja na uanzishwaji wa bima ya afya kwa wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika wa mazao inayojulikana kama ushirika afya, pamoja na Toto Afya kadi kwa Watoto walio chini ya umri wa miaka 18.

Mkurugenzi huyo alisema mfuko kwa sasa unahudumia wanachama 966,792 sawa na wanufaika 4,025,693 ambapo katika kipindi cha miaka minne kumekuwa na ongezeko la wanachama la asilimia 38.

Alisema katika kipindi cha miaka minne mfuko umewekeza jumla ya shillingi Bilioni 13.7 ambazo zimewezesha ukarabati wa miundombinu na ununuzi wa vifaa kama MRI, CT-Scan na mashine mbalimbali za vipimo na matibabu.

Kwa mambo haya hatuna budi kumpongeza Rais Magufuli kwa jitihada hizi za kutuhakikishia afya Bora.
 
Back
Top Bottom