Mwaka 2019 niliulizwa kuhusu wasifu wangu na mtu nisiyemjua na alichukua CV yangu

Israel

Senior Member
Apr 9, 2012
170
39
Habari Wakuu.

Naomba kuuliza ivi mtu ukiitwa na mtu usiyemfaham anakuambia ametokea ofisi ya utumishi na akaanza kukuuliza maswali ya historia ulipozaliwa, uliposoma na kufanya kazi, unaonaje kuhusu Rais na una kadi ya chama kipi lakin anakataa kukuambia anakufanyia interview ya nini na anakuomba umuachie cv yako lakini hakuombi ela wala kukupigia simu.

Pia hasemi ni interview ya nini. Ni miaka miwili sasa imepita tangu October 2019. Ila simu anapokea na kusema nilifanya yanipasayo na ripoti nilishakabidhi, kwan hujaitwa? nikasema bado huku akishangaa, basi endelea kusubiri.

Naomba kufahamu hii ilikuwa ni nini?

Maana mara ya kwanza nilifikiri utapeli lakini nikasema angalau angaliomba pesa au akaunti ya benk lakini hakufanya hivyo.
Swali. Lingine hata kama ni vetting, hii ni ya namna gani hujui hata ofisi na hakuna maelezo ya kueleweka.

Niko serious naomba msaada.kwa mwenye ujuzi wa ili jambo, tafadhali usiweke masihara kama huna cha kujibu.

Akhsanteni.
 
Ila kuna watanzania mnanidhamu za kipuuzi sana yaani mtu humjui gafla unampa taarifa zako bila sababu wala huna mawasiliano naye na wala hakupi maelezo.
Itabidi uwe mjinga kabisa kufanya upuuzi huo yaani akili yako iwe 0 kabisa kama sio hasi.
 
Back
Top Bottom