Mwaka 2019-2020 Serikali ilikamata cocaine na heroin kg 426.363, bangi na mirungi Tani 26.34

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,830
2,000
Waziri wa Nchi - Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema katika kipindi cha mwaka 2019 hadi 2020 jumla ya Dawa za Viwandani Kilo 426.363, pia bangi na mirungi Tani 26.34 zilikamatwa.

Amesema Serikali imebaini mitandao ya wafanyabiashara wakubwa wa Dawa za Kulevya na imeimarisha ulinzi wa majini, Nchi kavu na kwenye Viwanja vya Ndege ili kupambana na Biashara hiyo.

Watuhumiwa 124 wamekamatwa katika kipindi cha Januari 2020 hadi Mei 2021 ambapo 23 wametiwa hatiani huku mchakato wa mashauri 40 yanayohusisha watuhumiwa wengine ukiwa unaendelea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom