Mwaka 2018 utakuwa mgumu sana kwa utawala wa Magufuli

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
2017 ulikuwa mwaka wa matukio makubwa mengine ya ajabu ambayo Watanzania kwa muda mrefu hatujawahi kuyashuhudia, matukio haya ndiyo yaliyonifanya niuone mwaka 2018 kama sio mwaka mzuri kwa serikali yake.

Tumeshuhudia ukiukwaji mkubwa wa katiba na sheria za nchi kwa kisingizio cha kuleta maendeleo, tumeshuhudia amri halali za mahakama zikikiukwa waziwazi.

Watu wametekwa na kupelekwa kusikojulikana bila serikali kujali, kwa mara ya kwanza tumeshuhudia viroba vyenye miili ya watu vikiokotwa kando kando ya bahari na mto Ruvu pasipo serikali kutolea maelezo ya kuridhisha, bila kusahau matukio ya mauaji ya Kibiti.

Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi mchana kweupe na serikali kutojali wala kumhudumia mbunge wa Jamhuri ya Muungano si tu limesononesha watanzania wengi bali pia dunia nzima ya wapenda amani. Hadi leo hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, hii inaonyesha mwaka ujao utakuwa na matukio mengi ya aina hii. Mungu amponye haraka.

Mwaka huu nauita wa matukio kwa sababu kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru tumefanikiwa kuokota vichwa vya treni na semi treila zisizo na mwenyewe, hata baada ya mhusika kujulikana hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa.

Tukio la Makinikia ambalo mwisho wake haujajulikana nalo lilichukua airtime kubwa, bila kusahau tukio la ndege yetu aina ya Bombardier inayoshikiliwa Canada hadi leo. Je, tukiendelea kutoheshimu mikataba ya kimataifa hatuoni 2018 ndege zetu nyingi zaidi zitashikiliwa ughaibuni?

Hostel za chuo kikuu zilizojulikana kama 'hostel za Magufuli' nazo ziliacha gumuzo lililotawala anga la Tanzania hasa issue ya gharama zake na 'expansion joint', bila wahusika kuitwa na kuhojiwa.

Hatuwezi kusahau ushindi wa kishindo wa CCM wa Kata 43 ushindi ambao ulipatikana kwa msaada wa nguvu kubwa kupita kiasi za dola na kupelekea vyama vinavyounda UKAWA kususia uchaguzi wa January 2018. Bila NEC, msajili wa vyama, na vyama vyenyewe kukaa pamoja kumaliza dosari sioni mwanga wa demokrasia mwaka ujao wa 2018.

Tukio la kuachiwa kwa Babu Seya nalo liliwashangaza wengi ambao hatukutarajia wala Babu Seya mwenyewe kutarajia kuwa kuna siku atakuwa huru. Hata hivyo kuna watu wanahoji kuachiwa kwake, hata mkiti wa Parole mh. Mrema alihoji iweje mtu aliyehukumiwa kwa ubakaji akaachiwa huru.

Ulikuwa mwaka wa bomoabomoa, bomoabomoa iliwakumba watu wengi akiwemo Mh. Mbowe, wananchi wa Kimara na kwingineko. Huko Kimara kulikuwa na Stop Oder ya mahakama lakini serikali kwa kibri pasipo kujali muhimili wa Mahakama iliwabomolea wakazi wa huko. Wasiwasi wangu uvunjwaji huu wa amri halali hautazidi mwaka ujao na kusababisha matatizo makubwa kwa serikali ikiwemo kulipa fidia.

Kwa mara ya kwanza tangu rais Magufuli aingie madarakani takriban miaka miwili sasa hakujawahi kuwa na wimbi la watumishi wa Mungu kumpinga hadharani kiasi hiki.

Naliona tukio hili la kufungia mwaka kama kiashiria cha nini kitatokea kwenye utawala wa rais Magufuli kwa mwaka ujao wa 2018. Mara nyingi watu husema 'mwanzo mwema huashiria mema' kwahiyo ukianza vibaya tegemea mwisho mbaya au kukutana na matatizo makubwa.

Huwezi kuongoza vizuri huku wananchi wako wakinung'unika maisha magumu, viongozi wa dini wakinung'unika, wafanyakazi wakinung'unika, wafanyabiashara wakinung'unika, wanafunzi wakinung'unika.

NAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WA 2018.
 
nafikiri atakuwa ametimiza kauli mbiu yake ya watanzania kuishi kama mashetani
 
Back
Top Bottom