Mwaka 2018 Benki ya Kilimo itanunua Korosho, mwaka 2019 nani atanunua?

Huu ndio mwanzo wa anguko la Bank ya Kilimo Tanzania. Tunarudia makosa yaleyale ya kuingiza siasa kwenye uchumi

Hapo maana yake hakuna tena mtu mwingine kukopeshwa na Benki ya kilimo kwa sababu kipaumbele na fedha zote zinaelekezwa kwenye ununuzi wa korosho

Nasikia maneno kwamba zao la korosho ni miongoni mwa mazao ambayo yana syndicate ya hatari sana kwa wafanyabiashara wake. Itakuaje pale watakapocheza na soko na kufanya bei kwenye soko la dunia iporomoke kiasi cha kuisababishia serikali hasara kubwa?

Lakini labda ni kweli Tanzania sasa tunarudi kwa kasi kwenye siasa ya ujamaa ambapo uchumi unatumikia siasa na kwamba sio hasara kuua Shirika la Uma kama hiyo Bank ya Kilimo ili tu kutimiza matamko ya kisiasa, maana mbuzi ni wa Bwana Heri na shamba ni la Bwana Heri pia[/QUOTES
Soko la korosho utegemea internal factor na external.tuki control internal factor(value addition).tunabaki na factor za nje ambazo ni SOKO juu au chini ,kosa ni waliopewa viwanda wamefeli kuviendesha itakuwaje chokambaya kama mozambique wawaeze kubangua sisi tushindwe!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom