Nimemaliza chuo mwaka 2016, na kwa sasa nafanya kazi na shirika Fulani hapa Tz. Ingawa nafanya kazi ila sijaridhika na mshahara ninaolipwa na ndio maana niliendelea kupambana kutafuta kazi nyingine.
Katika mwaka huu unaomalizika nilkuwa na bahati ya kuitwa kwenye usaili lakini kupata kazi hizo ndo ilikuwa tatizo. Nilifanikiwa kupata moja tu ambayo ndio nafanya kwa sasa.
Kwanza niliitwa na shirika LA Norwegian refugee council nafasi mbili tofauti lakini zote nilikosa, ingawa hapa siwezi kulaumu kwa kuwa hata kabla sijafanya oral interview waliniweka wazi kuwa nafasi tunazogombani tayari zina watu ila wana mpango wa kuongeza wafanyakazi wengine wakipata funding ( hawa niliona wababaishaji)
Pili nilifanya usaili na shirika la Save the children kwa nafasi ya Education officer - Formal, hii nayo nilikosa
Tatu nikafanya usaili na shirika la Good neighbors Tanzania kwa nafasi ya Community outreach officer na hii NATO sikufanikiwa kuipata. Alikuwa anahitajika mtu mmoja na baada ya kufanya usaili tuliambiwa na wafanyakazi wengine wa pale pale kuwa tumepoteza muda wetu maana kuna mtu tayari yuko field anaendelea na kazi hiyo. Hawa nao walikuwa wababaishaji.
Nne na ya mwisho nimefanya usaili shirikala La Plan international nafasi ya ................. Nimeweka desh desh kwa kuwa majibu bado hayajatoka. Hii nadhan ndio ya kufungia mwaka.
Mambo niliyagundua katika harakati hizi;
Mashirika mengi yanaita watu ili kukamilisha taratibu tu za uajiri lakini wanakuwa tayari wana watu.
Ingawa huenda zipo ambazo nilizikosa kwa kuzidiwa na wengine lakini bado naamini mashirika mengi yana figisu sana katika michakato ya uajiri.
Natumai kuwa mwaka ujao nitaendelea kuitwa na nitafanikiwa kupata kazi nzuri zaidi na yenye mshahara mkubwa zaidi ya hii niliyonayo kwa sasa. Mungu nisaidie.