Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Wadau, hili ndio swali tunalopaswa kujiuliza kwa kuzingatia yaliyotokea mwaka 2015 ambapo matokeo ya uchaguzi yalifutwa na Bwana Jecha ambae ndio alikuwa kiongozi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Binafsi na ni imani yangu tuko wengi tunaoamini kuwa hata mwaka huu Maalim Seif atashinda uchaguzi huko Zanzibar kama dalili zinavyoonyesha.
Swali hapa ni je, safari hii atatangazwa mshindi iwapo atashinda?
Wasipomtangaza, wamejipanga kufanya nini au muda ndio utajua nini kifanyike?
Na wapinzani safari hii walivyopania, watakubali kutotangazwa washindi iwapo watakuwa na uhakika wameshinda huko Visiwani na hata huku Bara?
Pengine swali gumu kuliko yote ni je, Maalim Seif akiingia Ikulu ya Zanzibar, ataacha kuitisha kura ya maoni Wazanzibar waamue hatima ya Muungano?
Tuombe uzima kuona Taifa hili likirekodi historia mpya mwaka huu kuhusiana na maswala ya uchaguzi Bara na Visiwani.