Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,399
Ugonjwa wa COVID -19 ambao ni wa homa ya mapafu waendelea kuua watu duniani huku kukiwa hakuna dawa ya kukabiliana nao.
Na kwa mujibu wa wataalam mbalimbali duniani, hata dawa hiyo kuwa tayari kwa matumizi itachukua miezi karibu 18.
Ugonjwa huu uliripotiwa mwaka jana na tangu hapo hadi leo dunia imesimama na huenda ugonjwa huu ukabadilisha kabisa maisha ya watu, shughuli za kiuchumi na mstatakabali mzima wa maendelo ya mwanadamu duniani kote.
Kirusi chenyewe cha COVID -19 hakikuweza kutabiriwa na wataalam kwa usahihi lakini wataalm hao na wajuzi wa magonjwa na tabibu mbalimbali wamekuwa wakihisi kuja kutokea ugonjwa ambao ungeua watu wengi duniani kwa kipindi kirefu.
Lakini katika kupitia baadhi ya rekodi mbalimbali za mahojiano baina ya watu mashuhuri nimekuja kukutana na kauli alotoa bwana Bill Gates mwaka 2015 kwenye kipindi cha TED Talk.
Hiyo ni baada ya kumuangalia Bill Gates leo alipokuwa akihojiwa na televisheni moja ya kimataifa ambapo alisema kwamba ugonjwa huu leo umeiacha dunia katika eneo llisilo na mwenyewe yaani "uncharted territory "
Miaka mitano ilopita Billa Gates akihojiwa na kipindi hicho cha TED Talk alisema akitoa onyo kwamba maangamizi ya kidunia hayangesababishwa na vita bali kirusi. Alisema kwa kiingereza : "next ‘global catastrophe’ would not be caused by war, but by a virus"
Akaendelea kusema katika mahojiano hayo kwamba " kama kitu kinaua watu milioni 10 katika miaka 10 ijayo basi itakuwa ni kirusi kinachoambukiza kwa uzito kuliko vita na wala sio makombora bali ni virusi"
Bwana Gates akaendelea kusema kwamba sababu kubwa ni kwamba tumewekeza sana kwenye mitambo na manowari za kuzuia makombora kuepusha kupigana lakini tumeshindwa kuwekeza kwenye mifumo ya kujilinda na milipuko ya magonjwa .
Na akamalizia kwa kusema hatuko tayari kwa mlipuko wa mgonjwa ujao yaani
‘We’re not ready for the next epidemic.’
Akizungumzia matatizo zaidi ya kidunia bwana Gates akitoa mfano wa uginjwa wa Ebola ambao umeua waafrika.
Katika moja ya majarida ya Business Insider, la mwaka 2017 bwana Gates anasema katika makala yake kwamba uambukizaji kwa njia ya hewa utaua watu wengi zaidi ya milioni 10.
Bill Gates na mkewe Melinda mpaka sasa wamechangia kiasi cha dola milioni 100 ambazo zitaelekezwa kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa COVID -19 khasa kwenye kugharamia vifaa vya kujikinga, matibabu na vifaa kama vya kusaidia kupumua.
Mtazame bwana Bill Gates akizungumza
Je watu kama Bill Gates huwa wanapotoa kauli za kufikirisha huwa wanachukuliwa vipi?