Mwaka 2013 wakulima walifanya vurugu kukataa bei ya korosho ya 1,200 kwa kilo, serikali ilitatua vipi suala hilo?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Mwaka 2013 kulifanyika vurugu kubwa ambapo wakulima wa korosho walichoma moto nyumba 20 ikiwemo ya mbunge wa Liwale, wakipinga bei elekezi ya shilingi 1200 kwa kilo.

Vurumai hilo lilianza baada ya wawakilishi wa bodi ya korosho, kwenda kununuaa korosho hiyo kwa wakulima wakiwa na bei ingine waloibadilisha masaa machache yalopita.

Ilibidi askari polisi waende huko Mtwara kutuliza vurumai hilo na baadae kukatulia.

Bodi ya korosho ni moja kati ya bodi mbovu kabisa kuwahi kutoka kwenye historia ya nchi hii.

Baada ya bei ya korosho kupangwa awali kati ya wawakilishi wa bodi hiyo na wakulima, wanunuzi wanatoa fedha ambazo ndizo zinatumika kuwalipa wakulima hao kwa awamu.

Mchezo unaofanywa ni kwa wawakilishi hao wa bodi ya korosho, kubinya kiasi cha fedha halisi za malipo hayo na kuamua kupanga bei yao mpya ili kuwanyenga wakulima hao.

Lakini mwaka huo wa 2013 wakulima hao walichachamaa kwa kuona haki yao ya msingi ya kupata bei halali inaondolewa na ndipo walipopatwa na hasira.

Ni ufisadi huu ambao pengine ndio umemkosesha kazi mwenyekiti wa bodi mama Anna Abdalllah ambae ameshindwa kubaini michezo michafu inayochezwa bila yeye kufahamu.

Mwenyekiti wa bodi ya korosho anatakiwa awe mchumi au angalau ana mawazo ya kibiashara na anaweza kusoma alama za nyakati kwa wakati sahihi, kuhusiana na soko la korosho duniani.

Soko la dunia na mabadiliko ya bei ya zao hilo muhimu kwa uchumi wa Tanzania huleta sintofahamu kubwa kwa wakulima wa zao hilo ambalo ndilo mkombozi wao kiuchumi.

Lakini je, mwaka huo wa 2013 na ule ulofuata wa 2014 serikali ya CCM ilisimamia vipi bei hiyo ya kunyenga ya 1200 inayofanywa kati ya bodi wa korosho ikishirikiana na wafanyabiashara wenye kupenda kuweka maslahi yao mbele na kutanguliza faida bila kumjali mkulima?

Kwanini leo hii serikali ya awamu ya 5 ipigiwe kelele kwanini imeweka bei elekezi ya shilingi 3000 ambayo inalenga kumsaidia mkulima na kumnyanyua kiuchumi?
 
Mwaka 2014 yakafanyika mabadiliko ya wakuu wa mikoa. Na mkoa wa Mtwara alipelekwa bi Halima Dendego.. Mambo yakabadilika na mkulima akanufaika manake alijitahidi sana kukabiliana na kangomba. Ila fitina za wafanyabiashara na baadhi ya viongozi zikamfanya atolewe na leo hii baada ya mwaka ya kutolewa kwake korosho inasumbua
 
Wanaopinga ni chadema.

Wanatetea kila aina ya uchafu kwenye nchi yetu kuanzia wakulima kunyonywa hadi ushoga
Unawapenda chadema, Mme wako atakuwa mwanachadema tu. Haiwezekani kila baya linalifanywa na CCM uwasingizie chadema.
 
Mwaka 2014 yakafanyika mabadiliko ya wakuu wa mikoa. Na mkoa wa Mtwara alipelekwa bi Halima Dendego.. Mambo yakabadilika na mkulima akanufaika manake alijitahidi sana kukabiliana na kangomba. Ila fitina za wafanyabiashara na baadhi ya viongozi zikamfanya atolewe na leo hii baada ya mwaka ya kutolewa kwake korosho inasumbua
Huyo Halima alikuwa mpiga dili sana kwa kuwa karibu na wafanyabiashara wa korosho
 
Ndio maana sasa kwa kuwa nchi hii ni kubwa sio kama Rwanda na Burundi ,ni vema pakawa na serikali za majimbo!
Haiwezekani Korosho inalimwa Mtwara halafu Mwenyekiti wa Body anaishi Dar es Salaam.
Ni ujanja ujanja tu.

Pangekua na serikali za majimbo suala la Korosho lingekua limepata uvumbuzi wa kudumu mana lingekua linasimamiwa na kutolewa maamuzi kwa karibu na kwa manufaa ya wakulima kabla ya kitu kingine!!
 
Back
Top Bottom