Mwaka 2011 unakwisha kwa vituko, wizi na unafiki wa wazee waliokula chumvi nyingi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka 2011 unakwisha kwa vituko, wizi na unafiki wa wazee waliokula chumvi nyingi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rich Dad, Dec 31, 2011.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wazee ni watu wanaoheshimika sana katika jamii kutokana na busara wanazoaminika kuwa nazo. wameishi miaka mingi, na hivyo kushuhudia mambo mengi, pamoja na kukumbana na changamoto nyingi.
  Lakini tukiwa tunauaga mwaka 2011 baadhi ya wazee hao wameacha dosari katika jamii kutokana na vitendo vyao vya aibu walivyovifanya. Embu tujikumbushie baadhi ya wazee hawa waliokuwa wameaminiwa kwamba ni lulu ya taifa lakini kumbe ni kinyume chake:-
  1. Basil Pesambili Mramba - kesi ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi imeharibu kabisa taswira ya huyu mzee
  2. Philemon Luhanjo - Leo kamaliza muda wake wa kukalia kiti cha ukatibu mkuu kwa aibu kubwa pale alipojaribu kumsafisha muhalifu David Jairo
  3. Ludovick Uttoh - Kazi yale iliyotukuka iliingia dosari pale alipotoa report zilizopikwa kumsafisha David Jairo
  4. Samweli Sitta - Uropokaji kupitia vyombo vya habari na ndani ya bunge kuwabeza wapinzani ilhali ana sifa zote za kuipinga CCM.
  5. Edward Lowassa - Kujitahidi kujisafisha kutokana na scandal ya Richmond lakini bado wananchi hawamuelewi.
  6. Malechela - Uroho wa madaraka hadi pale alipoangukia pua, baada ya bwana mdogo kumpiga chini.
  7. Mzee Yusufu Makamba - Scandal zake za kupaka mtoto wa shule.
  8. Lyatonga Mrema - Kikombe cha babu wa Loliondo kimezidi kumchanga, alikuwa na mgombea wa urais kwenye chama chake lakini cha ajabu alikuwa akimpigia kampeni ndugu JK.
  9. Mama Anne Makinda - Jazba na sintofahamu za sheria na kanuni mbalimbali awapo bungeni.
  10. Wazee wa CCM wote wenye njaa kali wanaopewa ujira wa TZS 10,000 kwa kikao ili wajaze ukumbi na JK ahutubie.
  11. Mizengo Pinda - Kutaka kuonewa huruma pale anaposhindwa kujibu hoja kwa hoja.
  Unaweza kuongezea list......
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mbona yote hayo ni kawaida ya magamba!!
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Kingunge kwa kukwibia jiji kupitia stendi kuu ya mabasi Ubungo na tozo za kopaki magari jijini
  Wengine ni waliojiuzia mgodi wa makaa ya mawe kiwira kwa bei chee,wakautumia kuchukua mkopo na sasa huo mkopo sirikali ndio inalipa
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Slaa kuwalazimisha wakazi wa Arusha wakeshe uwanjani.
   
Loading...