Mwaka 2009 umeanza na kuisha kwa ufisadi na malumbano bila uwajibikaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka 2009 umeanza na kuisha kwa ufisadi na malumbano bila uwajibikaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Dec 30, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mwisho wa mwaka ni wakati wa kutafakari tulipotoka, tulipo na tunapotaka kwenda katika mwaka mpya. Kwa taifa ni fursa ya kufanya tafakari hiyo katika muktadha wa hali na mwelekeo wa taifa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

  Yapo masuala na matukio mengi ambayo tunaweza kushawishika kuyatafakari mathalani: hali ya mwaka huu wa 2009 kugubikwa na migomo mbalimbali vyuoni, makazini nk; kutetereshwa kwa misingi ya utawala wa sheria na haki kwa kurejea hukumu ya kesi ya Zombe na wenzake, kesi ya Dereva wa Mohamed Trans, kesi ya Ajali ya Chenge inayoendelea, kesi za Mramba, Yona, Liumba nk; yaliyojiri ndani ya CHADEMA wakati wa mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama; mabomu ya Mbagala; ripoti ya UN na tuhuma kwa Tanzania na watanzania kuhusu silaha nk; ajali na maafa mbalimbali; kuzinduliwa kwa mkakati wa kilimo kwanza; chaguzi za marudio Busanda na Biharamulo; hali ya kisiasa Zanzibar; orodha ni ndefu sana.

  Lakini kwa Tanzania toka CHADEMA na viongozi wake kwa kushirikiana na vyama vingine tutoe orodha ya mafisadi (list of shame) mnamo Septemba 15, 2007; ni vigumu kutathmini na kupanga mikakati ya kidemokrasia na kupanga dira ya maendeleo bila kutafakari kuhusu hoja ya ufisadi na haja ya uwajibikaji katika taifa letu.

  Hivyo katika kuyatafakari masuala na matukio yaliyojitokeza mwaka 2009 ni muhimu kujadili jinsi mwaka husika ulivyoanza na kuisha kwa ufisadi na malumbano bila uwajibikaji kamili wenye kukabiliana na changamoto za ujinga, umasikini na maradhi katika nchi yetu ambayo Mwenyezi Mungu ameijadilia utajiri wa rasilimali.

  Mwaka ulianza mwezi Januari 2009 kwa malumbano yaliyotokana na malalamiko ya Salum Londa (Mjumbe wa NEC CCM na Meya wa Manispaa ya Kinondoni) na Yusuph Makamba (Katibu Mkuu wa CCM) yaliyotokana na kauli ya Halima Mdee bungeni mwishoni 2008, akimtuhumu Makamba “kumlinda” Meya Londa, ambaye alisema anatuhumiwa kwa ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na uuzaji wa viwanja maeneo ya Kawe, Kinondoni. Kwa hiyo, mwaka ulianza kwa tuhuma za ufisadi zilizohusu Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni; manispaa ambayo sehemu kubwa ya viongozi wakuu wa serikali na vyama vya siasa wanaishi

  Mwaka unaisha mwezi Disemba 2009 jinamizi la ufisadi limeendelea kuinyemelea Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, baada ya kukubali kuuziwa matrekta 27 ya kuzoa takataka yasiyokuwa na viwango kutoka kwa mfanyabiashara, Yusuf Manji. Dalili za kuwepo vitendo vya ufisadi zimeonekana wazi baada ya Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo ambalo ndilo lililopitisha zabuni hiyo kugawanyika katika makundi mawili na kuendeleza malumbano bila uwajibikaji. Lakini tuhuma dhidi ya halmashauri hii haziishii kwenye zabuni pekee bali uuzaji na umilikishaji wa ardhi kinyume cha taratibu mathalani Eneo la Ufukwe wa Coco (coco beach) na umegaji wa kiwanja cha shule ya Msingi Kawe nk. Naandika haya mkononi mwangu nikiwa na taarifa ya siri yenye mihutasari na saini za viongozi wa CCM na Halmashauri ya Kinondoni ambazo zinathibitisha wazi kabisa tuhuma hizo zikitaja kwa majina na viwango vya rushwa ambazo zilitolewa ikiwemo kwa madiwani katika kashfa hizo. Taarifa hizo nitaendelea kuziweka hadharani mwaka 2010 kwa lengo la kuchochea uwajibikaji na mabadiliko ya kweli.

  Ikumbukwe kwamba kauli za kupinga ufisadi ziliendelea mwezi Februari, mathalani Dk Wilbroad Slaa akihutubia wananchi sokoni Kariakoo Dar es salaam, katika mkutano wa Operesheni Sangara alirudia mwito wa kutaka Rais Mstaafu Mkapa ashtakiwe kufanya biashara akiwa Ikulu; kuchukua Kiwira kwa bei chee na kushinikiza kulazimisha wabunge waivunje NBC yeye kuchota Milioni 500 kutoka ABSA kama cha juu. Katika mkutano huo uliorejewa na vyombo vya habari Dr Slaa alitetea msimamo wake kuhusu posho za wabunge akieleza dhambi kwa yeye kupokea 180,000 kwa siku wakati walimu wanapokea kiasi hicho kwa mwezi. Mishahara na posho za wabunge ni moja ya masuala yaliyozusha malumbano na mgawanyiko hususani miongoni mwa wabunge katika mwaka huu unaomalizika na kuendeleza mjadala kuhusu kukosekana kwa usawa katika mgawanyo wa keki ya taifa katika nchi yetu.

  Mwezi Machi; Wakati sakata la ujenzi wa maghorofa pacha ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) likinguruma mahakamani kwa kushitakiwa maofisa wake wawili waandamizi, tuhuma nyingine za ziada zikajitokeza tena kuhusu ujenzi wa majengo hayo. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, akathibitisha tuhuma hizo kwa kutamka hadharani kuwa Taasisi ya Kuchunguza na Kudhibiti Rushwa (Takukuru) kuchunguza mashaka yaliyomo kwenye mkataba wa bima wa ujenzi wa maghorofa hayo na kuchukua hatua stahili. Ilibainika kuwa mkataba wa bima wa ujenzi wa makao makuu ya BoT unaacha maswali mengi kutokana na kuwa na mapungufu kadhaa mathalani kukosekana kwa dhamana ya bima, gharama za bima zilizolipwa kuonekana zimezidi kiwango, kuingia mikataba miwili inayofanana na kuwepo kwa taarifa zinazokinzana kwenye mkataba wa bima wa awamu ya pili; ujumla tuhuma hizo zilihusu matumizi ya zaidi ya bilioni 10 za kitanzania. Mwezi huu wa Disemba mwaka unaishia kwa tuhuma zingine hivi sasa zikuhusu matumizi ya anasa ya zaidi ya Bilioni moja(yaani milioni zaidi ya 1000) kutumika kwa ujenzi wa nyumba ya gavana wa BOT ndani ya mkoa wa Dar es salaam ambapo wananchi wakufa kwa magonjwa yanayotibika kwa kukosekana kwa dawa katika hospitali za serikali; huku malumbano yakiendelea bila uwajibikaji.

  Makala inaendelea: http://mnyika.blogspot.com/2009/12/mwaka-2009-umeanza-na-kuisha-kwa.html

   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Who cares? Only in Tz where people believe on top to down GODLISM
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  UWAJIBIKAJI?????????????.........hizo hesabu ndugu yangu ni kukamilisha tu utaratibu wa kukagua hesabu haina maana kuwa lazima kuwepo na uwajibikaji kwa makosa ambayo kwa kweli ni makubwa na ya makusudi..........hii ndiyo tz nchi ya amani na utulivu..................hata wewe mnyika japo chama chako kinaitwa chadema inawezekana tukakupa uongozi fulani lakini ukalenga kuchukua chako mapema yaani ccm..............utu haupo...selfish carelwess to others is the only prevailing characteristic of tzn people......wale tuliowapa dhamana ya kusimamia raslimali zetu na kuchukua hatua kwa kufanya isivyo takiwa wenyewe ndio wa kwanza kutowajibika sasa nani hata akisikia kuwa kuna uozo pale atachukua hatua..............sijui tukate tamaa au tuendelee kujipa moyo kwamba tutafika?..............mi naona tumefikiri kwa muda mrefu baada ya kuwa huru zaidi ya miaka 40 sasa nahisi tumechoka tunatakiwa kuajili wazungu waje wafikiri kwa ajiri yetu..............mnashangaaa???????/...........inakuwaje kama viongozi wetu tumewaweka ili wafikiri kwa ajili ya taifa letu wao wanashinda kuombaomba na kufanya starehe majuu wakati watu mifugo yao yafa,watu wafa njaaa...mafuriko usiseme ila utasikia tu rais katuma salamu za rambirambi badala ya kufika.............kwa hali hii mimi napendekeza tuajili watu wa kufikiri kwa niaba yetu sisi tumeshindwa la sivyo system iliyopo ya kuchukua chako mapema iondolewe...........lakini nayo itaondolewa vp kama upinzani wenyewe ndio huu wa akina mrema na akina zitto?.............wanataka lazima wawe viongozi hii yote ni maslahi binafsi zaidi na kutaka sifa.....................waliostahili misifa sasa hawapo.................tungoje labda mungu atatujalia
  NIMEWAHI KUSIKIA KUWA SISI TUNA RASLIMALI NYINGI KAMA SIO ZOTE NA KWAMBA UMASIKINI WETU NIO WA KUJITAKIA NA HATUSTAHILI KUWA MASIKINI-NISAIDIE KAMA KWELI NI KWA NINI SISI BADO TUNAZIDI KUWA MASIKINI ILIHALI TUNA RASILIMALI LUKUKI?????????????KWAKO MNYIKA
   
 4. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #4
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Pole sana, umewasilisha fikra zako kwa hisia kali sana. Sababu ni kuwa tunaongozi uliokosa dira na uadilifu; tuna tatizo la kusosa uwajibikaji, haliko tu kwa viongozi bali pia kwa raia. Taifa linaongozwa kwa mazoea ya ufisadi na ubinafsi. Tunahitaji kubadili si tu sura za uongozi; bali mfumo mzima wa utawala na utamaduni wa kiraia katika nchi yetu.

  JJ
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Yohana wa Mnyika,

  Usihofu, tutaendelea kulumbana mpaka kieleweke! Kaeni Chonjo, Saa inakuja!
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  miaka inakwenda vivyo hivyo kila inapoitwa siku kila inapoitwa mwaka!lakini YOTE NI YALE YALE
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  well said my nephew Mnyika.
  Jitihada tuzifanye sisi VIJANA wa leo kwa faida ya vitukuu vyetu
   
 8. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante Mnyika kwa makala yako nzuri ya kusisimua na kuelimisha.

  Mimi nadhani suala la uwajibikaji ndo swala muhimu kuliko yote katika taifa letu. Nasikitika tu si watu wote wanalipa uzito linaostahili.

  Ili kuwawajibisha viongozi wabovu, naamini wananchi tunahitaji maarifa zaidi. Tunahitaji elimu zaidi juu ya haki zetu na wajibu wetu kama raia. Ninyi wanasiasa ndo mpo katika nafasi nzuri ya kutupa haya maarifa.

  Kila mnapoanika uozo na ufisadi wao, hapohapo pia msichoke kuelimisha wananchi jinsi ya kuwawajibisha.

  Taratibu kitaeleweka.
   
Loading...