Mwaka 2007 kulikuwa na Nokia toka Hungary (Ulaya), Chaji wiki moja na huku unaitumia, sasa za Wahindi na Wachina kiwango duni, Why?

Mimi mwenyewe ninaisubiri harmony OS, halafu chief kipindi hicho tulikuwa bado kwenye edge, hakukuwa na 3g wala 4g.
Naisubiri harmony OS maana kweli apps siku hizi ni kubwa sana ila chief si ukubwa wa app si unaendana na features, na graphic interfaces ilizonazo?


2021 tutaona simu ya kwanza ya harmonyOS kutoka kwa huawei. Sijui sie watumiaji wa huawei kama tutaweza ku upgrade kutoka android kwenda huko.
 
Najiuliza kwanini tusilete simu bora toka Ulaya kama Nokia ambayo mwaka 2007 nilinunua elfu sabini na ilikuwa inakaa na chaji wiki nzima na huku naitumia, ilitengenezwa nchini Hungary barani Ulaya na zilikuwa nyingi toka makampuni tofauti ila bora.

Nashangaa sasa hivi zinaletwa simu toka India na China kiwango duni Battery unachaji muda huu ukiongea Battery IPO nusu na sio smart phone, hata Nokia nayozungumzia haikuwa smart phone.

Nawaomba mnaohusika na uingizwaji wa vitu mturudishie simu zisizo za smart toka Ulaya, hizi za China na India tunateseka kuchaji.

Mie nadhani issue sio simu inatoka nchi gani. Inakuwa ngumu kwa mzungu kukaa chini ku assemble simu kwa mshahara anaopewa mchina au muhindi hasa linapokuja swala la mass production.

Hapo ndo kinapokuja swala la OEM. Yaani mchina au muhindi atakutengenezea kitu chako according ulivyokidesign. Ikatokea design hiyo hyo ukaipeleka ulaya pia wataitengeneza kama alivyotengeneza muhindi au mchina tofauti yake itakuwa ni cost. Ss hapo issue ipo kwa wafanyabiashara. wachina au wahindi wao wanafuata maelekezo tu.

Ukiwachana na wahindi na wachina nchi zinazoongoza kutengeneza simu nyingine ni korea, japan, taiwan, indonesia na nyinginezo.

Wafanyabiashara wanaweza kuleta vitochi madhubuti kama jiwe na vinakaa na chaji mwaka mzima kutoka china. Swali ni je tutaweza kununua?

Nimekuwekea mfano tu hapa wa smartphone na muda inayokaa na chaji. Na utaona simu nyingi ni za kutoka china. Unaweza kuadjust aina ya matumizi na ikakupa majibu ya ukaaji wake na chaji. Ukihitaji link ntakuwekea

Screenshot_20200920_024549_com.android.chrome.jpg
 
2021 tutaona simu ya kwanza ya harmonyOS kutoka kwa huawei. Sijui sie watumiaji wa huawei kama tutaweza ku upgrade kutoka android kwenda huko.
Hutaweza atleast Officially, unless Usa watoe vikwazo. Na sasa hivi Nvidia kanunua Arm ndo kabisa Sahau.
 
Kuna vitu tulikuwq tunafanya Symbian mpaka leo Android havipo, na Apps nyingi za sasa Za Android zilianzia symbian, tulikuwa tunaangalia tv online, kutumia whatsapp, facebook, games na emulators za kutosha.
Kwel mkuu nakumbuka nilikua naplay music wakati naongea nasim nauomziki ukasikika mpaka yule ninae ongeanae,
 
Sasa mkuu simu ilikuwa ina run symbian OS, au nyingine ni feature phone ram unakuta 500kb screen ndogo internal memory 12mb, screen resolution ndogo, unategemea chaji iishe saa ngapi mkuu?
wanapotengeneza betri hayo yote yapo into consideration labda umpe sababu nyingine
 
wanapotengeneza betri hayo yote yapo into consideration labda umpe sababu nyingine
Kuna technology limitations kwa muda husika, simu wanatak iwe nyembamba, lakini iwe na mamb mengi battery kwa wembamba ni upana wa simu unakuta haiwezi kuzidi labda 5000mah battery kwa technology iliyopo, option hapo wanakupa fast charging ili hata kama ikiisha uweze kuichaji kwa muda mfupi. Na atleast now zinakuwa na uwezo huo wakati previously zilikuwa zinachezea 1500mah mpaka 2500mah
 
Back
Top Bottom