Mwajuma utamuua mumeo...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Namshukuru Mungu kwa ajili ya akina dada/mama mlio wengi humu mlio na vipato na mnaochangia matumizi katika Masuala ya familia.
Hata hivyp naomba ninene na Mwajuma, akiwakilisha kundi la akina dada/mama ambao kwa mazingira ya Kitanzania amejikuta akiwa 'mama wa nyumbani', ambaye hana kipato na kama anacho ni kidogo hivyo bado anamtegemea sana mumewe Mashaka ambaye naye kipato chake kidogo anakipata kwa kazi ya 'udeiwaka', kuuza mtumba pale Karume...

Mwajuma anaelewa ya kwamba, mumewe kipato chake kidogo,
Hivyo inawabidi ya kwamba, waishi kufuatana na uwezo,
Lakini sivyo anavyofanya Mwajuma, Mwajuma hajui kukosa wala kupata,
Tamaa nyingi ndiyo kaweka mbele, na mambo mengine yamemzidi kimo,

Ooh Mwajuma loo! Achana na tamaa, ooh mwajuma loo! tamaa itakuponza,
Wala hana hata huruma, hana fikira hata kidogo,
Mume anampeleka mbio, mpaka mume hana raha tena',

Kila kukicha mwanamke nataka kile, jioni yake 'bwana nataka kile'!...
Akiletewa hata shukurani hana, leo na kesho kashau kila kitu

Ooh Mwajuma pesa hupatikana kwa tabu, ooh mwajuma pesa hupatikana kwa jasho...
Wanaishi nyumba ya kupanga, kila mwezi ni kodi ya nyumba,
Watoto wanataka matunzo, Mwajuma wala habari hana,

Akili yote kwenye urembo na mapambo, uchungu eti 'leo mwenzangu kavaa nini,
Akiona mwenziwe leo kapata kanga, lazima na yeye akadai kanga,
Hata kama mumewe yuko na hali mbaya, Atalazimishwa mpaka akakope,
Kama si hivyo, nyumbani hakulaliki, malalamiko na maneno chngu tele,
Vituko vyake Mwajuma, vimemtosha mumewe....



Rererence; Mwajuma song, by Marijabu Rajabu.
 
Lol hivi kwa maisha ya sasa, UPATU, Vicoba, saccos, n.k bado kuna wamama wanaowanyanyasa waume zao kwa vitu kama hivi? Hebu waamke jamani. MWanamke kujishughulisha eh!

Aksante Tuko kwa ujumbe huu mzuri
 
mkuu Tuko,tuwekee na ule wa max bushoke 'masoud amekuwa balaa,ukikutana naye.....' maana tusilaumu tu kinamama na sisi mmmhhhhh....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom