Mwajiriwa usiyetaka mafanikio usisome hapa.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,143
22,103
Wakuu wa JF natumaini mko poa.

Ninatumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya waajiriwa ambao hawasongi mbele kimaendeleo bila kujua sababu inayowafanya wawe hivyo. Wakuu kwanza kabisa ninamheshimu na kumpenda sana mtu anaefanya kazi yake kwa kujituma na kwa ubunifu. Ninaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na waajiriwa kwenye taasisi wanazofanyia kazi.

Kinachonifanya niandike leo ni hii hali ya baadhi ya waajiriwa kutotenga muda hata wa saa moja kufanya au kufikiria jambo kwa maendeleo yake binafsi. Utakuta mtu kaondoka alfajiri kwenda kazini na kurudi usiku na bado akirudi atalala usiku mkali kwasababu ya kuendelea kufanya kazi ya mwajiri wake.

Sasa kama muda wako wote unampa mwajiri, je wewe utafanya mambo yako mengine lini? Utawezaje kuongeza kipato cha ziada? Watu kama hawa mara nyingi hutegemea mshahara kwa 100% na kusubiria huruma za boss kumwongezea mshahara. Wakuu nimalize kwa kusema kuwa MUDA ndo kitu chenye thamani zaidi. Ukiamua kumpa mtu muda hakikisha kunakuwa na maslahi sio unautoa kiholela.

Asanteni kwa kunisoma.
 
Tumekusoma, Lakini Inategemea Na Kazi Unayofanya Wengine Wanaondoka Saa 12 Na Kurudi Saa 1 Usiku, Utafanya Kazi Gani Hapo
 
Wakuu wa JF natumaini mko poa.

Ninatumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya waajiriwa ambao hawasongi mbele kimaendeleo bila kujua sababu inayowafanya wawe hivyo. Wakuu kwanza kabisa ninamheshimu na kumpenda sana mtu anaefanya kazi yake kwa kujituma na kwa ubunifu. Ninaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na waajiriwa kwenye taasisi wanazofanyia kazi.
Kinachonifanya niandike leo ni hii hali ya baadhi ya waajiriwa kutotenga muda hata wa saa moja kufanya au kufikiria jambo kwa maendeleo yake binafsi. Utakuta mtu kaondoka alfajiri kwenda kazini na kurudi usiku na bado akirudi atalala usiku mkali kwasababu ya kuendelea kufanya kazi ya mwajiri wake. Sasa kama muda wako wote unampa mwajiri, je wewe utafanya mambo yako mengine lini? Utawezaje kuongeza kipato cha ziada? Watu kama hawa mara nyingi hutegemea mshahara kwa 100% na kusubiria huruma za boss kumwongezea mshahara. Wakuu nimalize kwa kusema kuwa MUDA ndo kitu chenye thamani zaidi. Ukiamua kumpa mtu muda hakikisha kunakuwa na maslahi sio unautoa kiholela.

Asanteni kwa kunisoma.
Sema tu wazi kuajiliwa na kutegemea ajira peke yake ni kuendelea kua masikini na kuishi kwa mawazo,hofu ya kila mala na kushindwa kuihudumia vyema familia,hakuna kitu kinaniuma kama ikatokea mtoto wangu anataka embe au tikiti maji na nikashindwa kumnunulia eti sijapokea mshahara.
 
Back
Top Bottom