Mwajiri hajapeleka PSPF michango ya mfanyakazi wake ni nini adhabu yake?

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,556
25,334
Amani iwe kwenu.
Imenibidi kuleta mbele yenu hoja hii, ndugu ameajiriwa miaka kumi iliyopita, mwaka wa kwanza wa ajira yake mwajiri wake hakupeleka michango yake kwenye mfuko wa jamii PSPF.

Mwaka huu alipaswa kupata moja kati ya mafao yanayotolewa na PSPF, katika kuwasilisha nyaraka ndipo walipompa orodha ya michango yake inayoonyesha kuna miezi zaidi ya 18 ambayo hakuchangia, wakatishia kumnyima fao hilo.

Kwa kuwa jukumu la kuwasilisha michango hiyo ni la mwajiri,
Je mwajiri anabanwaje na sheria ili apeleke michango ya mwanachama (pamoja na adhabu kama zinakuwepo)
Naomba kuelimishwa.
 
Back
Top Bottom