Mwajiri anapokuachisha kazi baada ya kutumikia kampuni kwa miaka 10

Upanga

Senior Member
Jun 18, 2007
145
50
Ndugu wana JF Naomba kujulishwa hivi inakuaje mtu umeajiliwa katika kampuni ya mtu binafsi na wewe ukiwa ni Mwajiliwa wa kwanza katika ofisi hiyo yaani ndo umeanza nayo,sasa mwenye kampuni anafungua Kampuni nyingine na anataka wewe tena ukaanze upya katika hiyo Kampuni Mpya,ikiwa namaana ajira yako ya awali inakufa.
Je ni haki zipi za msingi unastahili kupewa katika zoezi hilo zima?Kama kuna mtu anafahamu basi naomba maoni au inavyotakiwa kuwa ili nami nimsaidie mtu mawazo.
 
Kama kuna sababu ya kuachishwa basi anachukua mafao yake yote halafu anaanza upya. Kuna technicalities involved na kila mtu anategemea na each particular situation. Hiyo ya kwako iko juujuu sana na ndo maana unapata usahuri juu juu.

Laki swali la kizushi hivi kwa nini watanzania hawapendi kutoa elfu 20 halafu wakapewa ushauri wa kisheria? Why is it so difficult to ask and inquire?
 
Hapo inabidi mvunje mkataba wa awali muaanze kukubaliana mkataba mpya wa kazi mpya.
Kama utaamua kugoma na kuacha kazi inabidi ufate taratibu zinazoruhusiwa kisheria na hata huyo muajiri wako akiamua kukuachisha kazi naye afate utaratibu.
Kama hiyo kampuni mpya ni branch tu ya kampuni ya awali ila location tofauti nafikiri hapo utakuwa unapewa job transfer ambayo nayo ina taratibu zake za kisheria.
Nenda kwenye hizi firms za wanasheria ukapate ushauri zaidi kama devils advocate alivyopendekeza.
 
Back
Top Bottom