Mwajiri ana haki ya kumlazimisha mwajiriwa kupima afya?

FURY BORN

JF-Expert Member
Jul 11, 2020
638
1,145
Hivi majuzi timu ya mpira wa miguu ya Simba baada ya kikao cha kamati ya nidhamu iliadhimia kumpeleka mchezaji Jonas Mkude kupima afya ya akili Mhimbili.

Swali iko wapi haki ya Siri ya afya ya mwajiriwa? Je, endapo Mkude atakataa kwenda hospital Simba watamfanya nini?

Na vipi Mkude akiamua kufungua madai dhidi ya daktari na hospital itayoendesha fidia na kudai mamilio ikiwa matokeo ya madhara ya vipimo?
 
Hawa wachezaji kuwapima Ni sawa tu.
Wanavuta Sana bangi.
Nahisi huyu jamaa wa Utelembwe De mapaka fc anavuta pia.
 
Kuna baadhi ya kazi ni haki kupimwa na mwajiri kupata vipimo..Mpira ni mojawapo.Hata Ulaya tunaona hili linafanyika kabla ya klabu kununua mchezaji,anapimwa na kujiridhisha.
 
Mwajiri kumpima Afya mwajiriwa kabla ya ajira ni faida vile vile kwa mwajiriwa.

Siku ukimaliza mkataba ukapima, ikaonekana una madhara yaliyotokana na ajira yako. Unapata haki ya kudai fidia
 
Hivi majuzi timu ya mpira wa miguu ya Simba baada ya kikao cha kamati ya nidhamu iliadhimia kumpeleka mchezaji Jonas Mkude kupima afya ya akili Mhimbili.

Swali iko wapi haki ya Siri ya afya ya mwajiriwa? Je, endapo Mkude atakataa kwenda hospital Simba watamfanya nini?

Na vipi Mkude akiamua kufungua madai dhidi ya daktari na hospital itayoendesha fidia na kudai mamilio ikiwa matokeo ya madhara ya vipimo?
Kama masharti ya mkataba yanasema hivyo hakuna shida kabisa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya kazi ni haki kupimwa na mwajiri kupata vipimo..Mpira ni mojawapo.Hata Ulaya tunaona hili linafanyika kabla ya klabu kununua mchezaji,anapimwa na kujiridhisha.
Ulaya hawapimi ukiwa tayari mwajiriwa Bali kabla ya kuajiriwa. Pia sikumbuki kama huwa wanapima afya ya akili
 
Afya ya akili,unasema wewe.
Wao wamesema afya
Tumia akili kufikiria na Rudi kwenye barua iliyoandikwa na club ya Simba, nadhani wewe tayari wewe umeingia kwenye ushabiki, Kwa mawazo yako unadhani ataenda kupima Choo au mkojo? Ama umesikia ana majeraha ya goti au enka?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom