MWAHALISI/ KUBENEA KWISHA! Ni Malipo ya Kutumiwa na Mafisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MWAHALISI/ KUBENEA KWISHA! Ni Malipo ya Kutumiwa na Mafisadi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kapela Msonda, Jun 1, 2011.

 1. K

  Kapela Msonda Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kulundikana kwa magazeti ya MwanaHalisi kwenye baadhi ya vibanda vya magazeti jijini Dar es Salaam mpaka saa hizi za jioni ni dalili tosha ya kuisha mvuto wa gazeti hili lililokuwa kipenzi cha wapigania haki nchini pamoja na mhariri wake Kubenea kama ambavyo mvuto wa RAI/Mtanzania ulivyokwisha kwa mara moja na wahariri wake akina Mhingo na Balile kutokana na kutumiwa na Mafisadi.

  Pamoja na kujitutumua safari hii na kichwa cha habari cha kudanganyia wasomaji "Mafisadi CCM sasa wageuka Mbogo", Kubenea bado anaonesha kubanwa koo na Mafisadi ambao inasemekana sasa wanammiliki kwa kurashiarashia habari hii na kuishia kuwananga wabaya wake wapya: Sitta, Mwakyembe na Nape!

  Kilichonilazimu nijitose hapa JF ni tamko la MwanaHalisi kuwa litakuja wiki ijayo na taarifa nyeti juu ya hao wabaya watatu wapya wa Kubenea kuhusu chama kisichokuwepo cha CCJ kwa mujibu wa mtu mmoja aitwaye Dickson Ng'hily, anayetambulishwa kuwa naibu katibu mkuu wa CCJ wa zamani. Mimi na wenzangu tuishio Temeke pamoja na Mbunge wetu, tunamhakikishia Kubenea kuwa sasa anajiua mwenyewe kitaaluma kwani tunamjua sana huyo Ng'hily, si chochote, si lolote.

  Bwana Dickson A. Mg'hily anajulikana sehemu mbalimbali hapa Dar es Salaam kama Mchungaji (sampuli ya akina Mtikila). Aligombea ubunge Temeke mwaka 2010 kwa tikiti ya CHADEMA, akabwagwa na CCM kwa sababu huyu jamaa ni TAPELI! Anajiita Mchungaji, lakini ukimpenyezea rupia tu yuko radhi kufunga ndoa na shetani. Nasema hivi kwa kuwa namfahamu sana msanii huyu.

  Sitashangaa kuja kujua baadaye kuwa huyu baba hamfahamu Sitta, Nape wala Mwakyembe, ila kapenyezewa kitu yuko radhi kuapa kuwajua! Hafasi kabisa mtu huyu, lakini wiki ijayo ndo anapamba gazeti la MwanaHalisi!

  Mtume! MwanaHalisi bye bye!
   
 2. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,088
  Likes Received: 883
  Trophy Points: 280
  R.I.P Mwanahalisi. Huko uendako utakutana na Rai. Mungu ailaze mahali pema peponi. Amen!!!!!!!!!!
   
 3. G

  Galula Jr Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wewe umetumwa na Nape, mwambie akakupe semina elekezi upya. Huu ni upupu tu umeandika. MWANAHALISI ni kiboko ya MAGAMBA
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Siamini km ni habari za kweli maana mwanahalisi lilikuwa gazeti langu kipenzi mwenyewe nimestuka kidogo habari za leo.....ila kwa sasa ngoja niamini kwa muda kuwa huu ni umbeya wako mwandishi ila nafuatilia kwa kina nikigundua mwandishi umenena ukweli nitakuomba radhi.......naondoka kutafuta data
   
 5. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60

  M/Halisi litasomeka daima, jaribu kukusanya takwim za mauzo ya

  UHURU/MZALENDO
  HABARI LEO N.K

  Kisha urudi hapa
   
 6. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  KASOME UHURU, MZALENDO, MTANZANIA, RAI, HABARI LEO, DAILY NEWS AMBAYO KUFIKIA SA MBILI YAMEKWISHA

  TOKA LINI KUBENEA MBAYA WAKE SITA, MWAKIEMBE NA NAPE

  WAPIGANAJI TUNASOMA MWANAHALISI AND WILL NEVER DIE

  [​IMG]
   
 7. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kubenea ni kama msumeno inakata kotekote, mimi nafanya kazi kwenye kampuni ya magazeti ndugu yangu kapela msonda nakuhakikishia kuwa Mwanahalisi ndio gazeti linaloongoza kwa mauzo sokoni ,kuzikuta kwenye baadhi ya vibanda is not a issue inawezekana ameongeza suply and for your information hili ni gazeti la wiki returns zinarudishwa jumapili kwahiyo usilihukumu mapema

  Msonda kinachokutisha ni toleo lijalo la mahojiano ya kubenea na kamanda Nghili kama umetumwa na sita , Dr Mwakyembe ,Nape pamoja membe hili umtishe kubenea pole imekula kwako, kubenea usiterereke washughulikie wote Mafisadi na wasaliti CCJ
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  siamini kama yatatokea mabadiliko nchi hii,mafisadi watatumaliza
   
 9. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  MwanaHalisi kwangu limekuwa maruhumu nimeshalizika na hata Kubenea sijui aje kwa staili gani hata akiwa ya kujivua ngozi badala ya gamba tayari kawa kwishne,hakika nakubaliana na maneno ya Kardinali Pengo kuwa wote wanaowasema mafisadi ni kuwa nao wangekuwa mafisadi ila tu wamekosa fursa za kufisadi,kumbe kelele zote za Kubenea kuhusu mafisadi alikuwa anatafuta njia za kuwa fisadi kwa kuwatisha kwanza hao mafisadi na akisha fanikiwa kuwatisha hao mafisadi naye ajifisadi kwa hao nguli wa ufisadi
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mada imemlenga Dickson A. Mg'hily , tunasubiri majibu yake
   
 11. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kuna watu wakiona habari wala hawajiulizi hata kidogo. wanakurupukaa tuuuuu, hata ukiwambia Mungu yuko kigamboni watasema kweli wamemuona wakati wanadanganywa. Habari itakuja kama ilivyo wala haitabadilika. Kawaambie mganga wao amewaingiza mjini.
   
 12. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mmh, mbona haiingii akilini? Anyway, nitarudi baadaye!
   
 13. M'bongo

  M'bongo Senior Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Ni kweli WISDOM SEEDS, hata mimi nimeisoma hii thread na kuirudia tena lakini sijaelewa sawasawa
  ingawa nahisi kama kuna kitu ndani yake ambacho kimefichika. Please kapela hebu fafanua vizuri kuhusu hili
   
 14. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Katika waandishi niwapendao Tz, Kubenea no.1,Hizi taarifa za kununuliwa kwake na LA&RA zimezagaa kwa kasi kuanzia mwezi wa 5,sijaona sehem akikanusha hizi habari Kubenea mwenyewe.Lisemwalo lipo ebu tuangalie siku hizi haandiki makala za EL&RA kwa kina zaidi ni kuwashambulia kwa kina Mwakyembe,Sitta na Nnape.

  Kwa upande wangu sifikiri kama Mwakyembe,Sitta na Nnape wamefanya kosa la jinai kuanzisha CCJ.Kuanzisha chama cha siasa ni ukomavu wa kisiasa kama huridhishwi na sera za chama ulichopo.Tumeona miaka ya 1990s viongozi wengi wa CCM walitoka na kuanzisha vyama vingine.Sizani kwa gazeti letu pendwa mwanahalisi kuipa uzito habari za akina mwakyembe sitta na nnape kwa sasa.

  Kwa nini habari za RA,Che&EL kwa sasa hatuziskii kabisa na kama zikizungumzwa kinagusiwa kwa mbali sana.

  Nachelea kwa sasa kukanusha hizi habari ila matukio yanatuonesha

  History will judge our action
   
 15. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  mimi binafsi leo nimezunguka mji mzima wa arusha kutafuta gazeti hili kila kibanda linakua limeisha, sasa wewe umefanya reseach Kisarawe pekee au??
   
 16. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tusikurupuke, tusiamini kila kiandikwacho! kwanza hbr yenyewe inaonekana wazi imegubikwa na chuki! Mwandiko wa katibu wa itikadi huo!!
   
 17. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  ngojea tusubiri tuone yetu macho, ukweli utadhihirika baadae kama ni kweli au la!
   
 18. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mwanahalisi na gazeti si jarida hivyo linaandika ukweli bila kujali unamgusa nani sasa km ww unapenda ukweli endelea kusoma km vp lipotezee kwa sababu lengo la kuchapishwa kwake ni
  Kutoa taarifa sahihi na si kuangalia zitamfurahisha au kumuudhi KM
  Kubenea kanyaga twende
   
 19. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamaa katumwa na haraka haraka mpaka kaandika MWAHALISI!
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuonyesha kuwa wewe ni hujui ulisemalo ni taarifa yako kuwa magezeti ya MwanaHalisi hadi jioni hii yamejaa. Toa taarifa yenye takwimu kuwa kila jumatano yalipokuwa yanatoka mtaani kiasi fulani kilikuwa kinauzwa na sasa kiasi hicho kimeshuka kwa kiasi kadha kwa sababau kadha. Kwa taarifa tu chunguza uwezo wa watu wa kipato kililivyoshuka.

  Unazungumzia Dickson A. Mg'hily kuwa unamfahamu kwa hiyo tukuamini kama wewe ni malaika kumbe ni pepo. Halafu umejilineup na wapambe wa kukupongeza hapa JF wanaojulikana. Mimi binafsi nakuona huna hoja angalau ungetuambia undani wa hao mafisadi wamelimalizaje gazeti kwa lengo jema kwa nchi yetu; kumbe mwenzetu unashabikia maafa ya nchi yetu. Lakima kama mlivyokuwa wakweli kwenye kujivua magamba na kubakia na sumu kali kwa nchi yetu, mnajitahidi kufa na mtu. Mmebainika na baadhi yetu.

  Ebu tubadirike tushabikie upambanaji wa kweli wa taifa hili hata kama ni kutoka gazeti la uhuru kama litaanza mapambano ya ukombozi kesho.

  Sijui umri wako lakini uandikaji wako una taswira ya mtu mzima, ila OVYOO
   
Loading...