Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,952
Of course hii inaweza ikatolewa hapa baada ya muda na kuwekwa panapofaa-sijui ni wapi??!!
Lakini ukweli ni kwamba Mwafrika wa Kike ameniudhi sana kwa sababu haiwezekani yeye apotee kipindi hiki ambacho ni critical na taifa letu linapita katika majaribu mazito likwemo la uchawi huko bungeni. Kama bado anatafuta habari za Balali, namwomba aachane nazo kwa sababu hizo habari sasa hivi sio deal tena. Kama kawaida yetu watanzania hilo tumeshalisahau, na sasa tuna-deal na issue ya uchawi kule bungeni Dodoma.
Kwa hiyo dadangu rudi tafadhali tuje tushirikiane katika hili la uchawi, na ukichelewa utakuta hili nalo limeshaisha na tutakuwa tumeanza na lingine. Matokeo ya kupotea kwako ndiyo haya unaona vijana ambao ndio wanaanza ukada wa CCM, hawasikii chochote, wao wanasifia kila kitu hata uchawi. Hapa namuongelea huyu kijana wetu Mashaka ambaye amekuja kwa moto wa kifuu na kumshinda kwa mbali kabisa kada mpinzani kwa kutetea yasiyoteteeka na kuhalalisha yasiyohalalishika. Kama hutarudi hivi karibuni huyu kijana ataendelea kusumbua wengi; nimeona wazee wameshaanza kumrushia mawea makali lakini sidhani kama wataweza kumuweka sawa kabla hujarudi.
Ok, sasa na hawa wameenda wapi? Kwa nini wameogopa kushiriki kwenye hili la kujadili uchawi kule bungeni? hapa nawaongelea ndugu zetu: Game Theory, Madela-wa Madilu na Kichuguu (huyu kapotea siku nyini sijui nini kimemsibu).
Mbaya zaidi Brazameni ndiyo kabisa kajificha wakati anajua kabisa kipindi kama hiki ndio kwanza tunahitaji sana commercial breaks zake na zile picha motomoto.
Na katika hizi siku mbili Nyani Ngabu kauchuna kabisa na hataki kutia neno kwenye hili sakata, au ndio umeshahitimisha kwamba ndivyo tulivyo.
Hebu acheni hizo, rudini hapa- haya mambo ndiyo kwanza yanaanza.
If this didn't make you smile, sorry but I am not to be blamed, I had forgotten that the weekend has actually just gone and we are at the beginning of the new week!