Mwafrika wa kike kumuunga Mkono Mheshimiwa Kikwete

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
Okay!

Habari kwamba kuna watu wanatoa vitisho huko serikalini kuwa watabomoa serikali ya Kikwete kama akiwashughulikia kwa makosa yao ya ufisadi zimefikia kipimo cha juu kabisa cha uvumilivu. Sina sababu ya kuanzisha mjadala wa kujua kama ni kweli au ni propaganda ingawa mpiganaji mwenzangu Kubenea amehakikisha kuwa hii habari ina ukweli ndani yake.

Ninakumbuka vizuri juhudi za mzee wa kasungura na ndege iliyoishiwa mafuta AKA morani AKA mzee wa tripi AKA zungu la Richmonduli AKA Lowasa alivyojaribu kujisafisha kwa kuwatumia kina Balile na wenzake lakini in the process kulipa kisasi kwa kina Mwakyembe na wenzake (JK?) waliomshushua bungeni.

Nimevisikia kwa makini vitisho vya mzee wa vijisenti na kunywa sumu AKA mzee mpenda mbichi (wanafunzi wa shule) AKA mzee wa kashfa kibao kabisa za wizi na ufisadi Tanzania AKA Chenge na lawyer wake kuwa "watalipiza kisasi" na kuwaumbua wote wale wanaowafuatilia kwenye kesi ya wizi.

Nimevisikia pia vitisho vya Patel, Manji, Rostam, Kagoda, Mramba na wezi wenzao kibao kuwa watahakikisha utawala wa nchi na sheria unakuwa mgumu kwa vile watu wanafuatilia ulaji wao. Kwa yote haya, hili la kumtisha hadi Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali yake limefikia kipimo cha juu. Haijalishi kama Mkapa anahusika au ni Apson na wanausalama wenzake. Katika hili hakuna cha mswalie yeyote.

Nimeamua kumpa Kikwete nafasi ili afanye kweli katika hili. Najua kuwa alinidisapointi Butiama lakini kwa sasa nampa tena nafasi nyingine ya kufanya kweli na kuwa supporter wake kila mara anapowachukulia hatua mafisadi. Nitaacha kumpondea Kikwete kwa mwezi mzima (Kikwete-Bashing-Free posts for a month). Niko nawe mheshimiwa sana raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Ingawa najua bado hujafanya chochote kwenye wito wangu wa kupunguza bei ya nishati Tanzania lakini sasa nakupa nafasi tena ya kutokomeza ufisadi na mafisadi toka kwenye serikali yako. Kwa hili utapata free ride toka kwangu na free media attacks kwa wale maadui zako wote watakaojaribu kuleta propaganda zao hapa JF na kwingine kote ambako kazi zangu zinafika.

kwa mwezi mzima, mwafrika wa kike anamuunga mkono Kikwete katika juhudi zake za kutokomeza ufisadi Tanzania.

Asante.
 
MWK, Rais wa nchi hatishiwi Nyau naye akaogopa. Ikitokea Rais wa nchi aliyetishiwa nyau akaingia woga, basi ujue kuna siri kubwa sana. Panapofuka moshi....
 
Mwafrika wa Kike,
Kama kweli Kikwete ataweza kuwafikisha mahakamani hawa mafisadi basi wananchi wote watakuwa nyuma yake as a fact naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, mimi hapa nitakuwa mmoja kati ya wapenzi wake toka siku hiyo!
Kwanza yeye kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hizi habari za migahawani haiwezi kabisa kuhatarisha national security ati kwa sababu ya watu wachache wahuni na mafisadi wasiopendwa na wananchi wote.

Nakumbuka enzi za mwalimu alipotangaza Azimio la Arusha, watu walisema kama haya wengine wakaenda misikitini na makanisani kumwombea mabaya wengine hata kuingia msituni lakini - Alichofanya mwalimu kilikuwa kilipewa baraka za watanzania wote.. Washeikh wakubwa wote na Mapadre wakubwa wote..zaidi ya yote yeye ndiye amiri jeshi mkuu na jeshi lote lipo nyuma yake, hivyo vitisho kama hivi haviwezi hata siku moja kupewa nafasi.kama kweli anaweza kufanya afanye hakuna kisingizio.. kiti cha Ikulu amekikalia yeye na sio Lowassa wala Patel.

Kama ningekuwa Kikwete ningeyafanya ya mwalimu, unaposikia fununu kama hizi unamwita mtu IKULU na kumweka kitimoto... akitoka hapo atafute choo kushusha mzigo kwanza.
 
MWK,
kama kuna wakati muafaka wa kumweka kikwete under massive pressure basi ni huu......kama unawasha Jiefang vile kwa "handeli," hupunguzi kasi pale linapokaribia kuwaka bali ni kinyume chake(unaongeza), yaani unapulizia moto mpaka uwake kabisaaaa!!!

pulizi, usimpe hiyo "pressure free" holiday........nadhani itakuwa ni makosa kufanya hivyo!!.
And it is by Principle that:"If the rate of Pressure on the outside (of JK) exceeds the rate of Pressure on the inside, the end is near"
 
MWK, Rais wa nchi hatishiwi Nyau naye akaogopa. Ikitokea Rais wa nchi aliyetishiwa nyau akaingia woga, basi ujue kuna siri kubwa sana. Panapofuka moshi....

Of course kuna siri kubwa....Kama tujuavyo jamani siasa ni mchezo mchafu na sasa ukiangalia katika dunia ya sasa bila pesa huwezi kuupata wacha ubunge hata ule ukatibu wa chama wa wilaya.

JK amekuwa kwenye govt muda mrefu sana na ameona uchafu wote uliomo katika CCM na serikali na tujiulize je wakati wote huo alpokuwa serikalini wakati kina Mramba,Chenge na hawo mafisdi wengine wakijichukulia mapesa nmbona yeye alikuwa hajilimbikizii?.

Mimi naamini (MAONI YANGU) kuwa alikuwa anangojea siku ambayo atapopata na kuwa rais basi ataisafisha nchi yetu.

Watu mtajiuliza kwa nini asijiuzulu wakati ule and blow the whistle?.Mimi nafikiri kuwa aliona haitaleta mabadiliko kwani wote mnajua kujiuzulu hakusaidii chochote angalia watu kama Powell au yule mama wa kiingereza Claire Short na Robin Cook aliyekufa.

Kwa hiyo ilibidi ashirikiane na hawa mafisadi ili watoe hayo mapesa kwa ajili ya kampeni na sasa ameamua kuwatoa mmoja mmoja....hii ni ngazi ngumu sana kusafisha chama ambcho tawala kwa muda mrefu na kina mzizi kila mahali yaani polisi,usalama wa taifa,jeshi,...kila mahali wana mizizi.

Kufanya vitu vyote hivyo vinahitaji ujasiri na muda.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.....IKO SIKU TUTAFIKA
 
Mwanatanu,
I hope haitatokea siku Kikwete atakuvunja moyo.
Sidhani ni msafi kama unavyomfikiria wewe.
 
Mkuu, hapo umekuwa diplomatic sana, lakini ukweli ni kwamba supporters wa Kikwete wamekuwa wakimtetea na kutoa sababu nyingi wakiahidi mtaona mabadiliko hivi karibuni lakini wapi! He cannot handle the heat in the kitchen!
 
Mwanatanu,
I hope haitatokea siku Kikwete atakuvunja moyo.
Sidhani ni msafi kama unavyomfikiria wewe.

Amenivunja moyo sana kwa ile hotuba yake Singida.
Kuhusu usafi inawezekana naye anavijisenti lakini life style yake alipokuwa waziri haikuwa na dalili yoyote ile ya vijisenti maybe he was playing cool akingojea jackpot
 
Of course kuna siri kubwa....Kama tujuavyo jamani siasa ni mchezo mchafu na sasa ukiangalia katika dunia ya sasa bila pesa huwezi kuupata wacha ubunge hata ule ukatibu wa chama wa wilaya.

JK amekuwa kwenye govt muda mrefu sana na ameona uchafu wote uliomo katika CCM na serikali na tujiulize je wakati wote huo alpokuwa serikalini wakati kina Mramba,Chenge na hawo mafisdi wengine wakijichukulia mapesa nmbona yeye alikuwa hajilimbikizii?.

Mimi naamini (MAONI YANGU) kuwa alikuwa anangojea siku ambayo atapopata na kuwa rais basi ataisafisha nchi yetu.

Watu mtajiuliza kwa nini asijiuzulu wakati ule and blow the whistle?.Mimi nafikiri kuwa aliona haitaleta mabadiliko kwani wote mnajua kujiuzulu hakusaidii chochote angalia watu kama Powell au yule mama wa kiingereza Claire Short na Robin Cook aliyekufa.

Kwa hiyo ilibidi ashirikiane na hawa mafisadi ili watoe hayo mapesa kwa ajili ya kampeni na sasa ameamua kuwatoa mmoja mmoja....hii ni ngazi ngumu sana kusafisha chama ambcho tawala kwa muda mrefu na kina mzizi kila mahali yaani polisi,usalama wa taifa,jeshi,...kila mahali wana mizizi.

Kufanya vitu vyote hivyo vinahitaji ujasiri na muda.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.....IKO SIKU TUTAFIKA

Mwanatanu,
I hope haitatokea siku Kikwete atakuvunja moyo.
Sidhani ni msafi kama unavyomfikiria wewe.

Jasusi,

Post hiyo hapo juu imekujibu vizuri mno. Ili uweze kuwajua na kuwatokomeza adui zako, jiunge nao.....

Wengine wanaweza kukufikiria vibaya kwa kujiunga nao lakini ndio njia sahihi. Ameshawajua kwa hiyo anawateketeza mmoja mmoja.

Big up Muungwana!
 
Okay!

Habari kwamba kuna watu wanatoa vitisho huko serikalini kuwa watabomoa serikali ya Kikwete kama akiwashughulikia kwa makosa yao ya ufisadi zimefikia kipimo cha juu kabisa cha uvumilivu. Sina sababu ya kuanzisha mjadala wa kujua kama ni kweli au ni propaganda ingawa mpiganaji mwenzangu Kubenea amehakikisha kuwa hii habari ina ukweli ndani yake.

Ninakumbuka vizuri juhudi za mzee wa kasungura na ndege iliyoishiwa mafuta AKA morani AKA mzee wa tripi AKA zungu la Richmonduli AKA Lowasa alivyojaribu kujisafisha kwa kuwatumia kina Balile na wenzake lakini in the process kulipa kisasi kwa kina Mwakyembe na wenzake (JK?) waliomshushua bungeni.

Nimevisikia kwa makini vitisho vya mzee wa vijisenti na kunywa sumu AKA mzee mpenda mbichi (wanafunzi wa shule) AKA mzee wa kashfa kibao kabisa za wizi na ufisadi Tanzania AKA Chenge na lawyer wake kuwa "watalipiza kisasi" na kuwaumbua wote wale wanaowafuatilia kwenye kesi ya wizi.

Nimevisikia pia vitisho vya Patel, Manji, Rostam, Kagoda, Mramba na wezi wenzao kibao kuwa watahakikisha utawala wa nchi na sheria unakuwa mgumu kwa vile watu wanafuatilia ulaji wao. Kwa yote haya, hili la kumtisha hadi Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali yake limefikia kipimo cha juu. Haijalishi kama Mkapa anahusika au ni Apson na wanausalama wenzake. Katika hili hakuna cha mswalie yeyote.

Nimeamua kumpa Kikwete nafasi ili afanye kweli katika hili. Najua kuwa alinidisapointi Butiama lakini kwa sasa nampa tena nafasi nyingine ya kufanya kweli na kuwa supporter wake kila mara anapowachukulia hatua mafisadi. Nitaacha kumpondea Kikwete kwa mwezi mzima (Kikwete-Bashing-Free posts for a month). Niko nawe mheshimiwa sana raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Ingawa najua bado hujafanya chochote kwenye wito wangu wa kupunguza bei ya nishati Tanzania lakini sasa nakupa nafasi tena ya kutokomeza ufisadi na mafisadi toka kwenye serikali yako. Kwa hili utapata free ride toka kwangu na free media attacks kwa wale maadui zako wote watakaojaribu kuleta propaganda zao hapa JF na kwingine kote ambako kazi zangu zinafika.

kwa mwezi mzima, mwafrika wa kike anamuunga mkono Kikwete katika juhudi zake za kutokomeza ufisadi Tanzania.

Asante.

Mh!, Kaazi kweli kweli.
 
Ukipata uongozi kwa rushwa hata kutimiza majukumu yako ya uongozi utashindwa,Na ndicho kinachotokea sasa hivi nchini.Mafisadi wanatamba na tena wanapokelewa kwa misafara kama ya Bush.Nchi hii bado kuna watu wa mawazo ya kijima sana.Mtu kaingizia Taifa hasara,alafu bado wanaungua jua barabarani kumsubiri mporaji.This is BS.

Ukiangalia kikatiba Rais ana mamlaka kubwa sana ambayo inampa kutamka jambo na kuwa kama sheria ambayo watu wa chini yake ni kutekeleza.

Kushindwa kutimiza wajibu husabishwa na hofu ambayo mhusika anajua dhahiri walikuwa ktk vikao vya siri na mafisadi na wakaandikiana kabisa na kumbukumbu kuwekwa.Hao mafisadi wana jeuri kwa kuwa wana vibaraka wao ktk ngazi za uongozi ambao Rais alikuwa tu akipelekewa mapendekezo/watu na yeye akayabariki kwa kuapisha.iliwahi kuvuja mapema kuwa IGP angekuwa kamishna fulani hapa DAR,Lakini kwa matakwa ya watu binafsi wakapindisha.

Huyu mheshimiwa kuthubutu kuleta mapinduzi ya ki uongozi ni lazima kwanza AENEE KATIKA KITI KAMA RAIS maana sasa hivi wala hajakalia kiti cha Rais kama ambavyo tunajua majukumu ya Rais kikatiba kwa kuwa wapo watu wachache tena wapuuzi wanaopeleka nchi hii pabaya.

Pili kama anaona chama cha kijani kimemzibia aanzishe njia kama ya BINGU WA MUTHARIKA kule Malawi aanzishe chama chake.
 
Okay!

Habari kwamba kuna watu wanatoa vitisho huko serikalini kuwa watabomoa serikali ya Kikwete kama akiwashughulikia kwa makosa yao ya ufisadi zimefikia kipimo cha juu kabisa cha uvumilivu. Sina sababu ya kuanzisha mjadala wa kujua kama ni kweli au ni propaganda ingawa mpiganaji mwenzangu Kubenea amehakikisha kuwa hii habari ina ukweli ndani yake.

Ninakumbuka vizuri juhudi za mzee wa kasungura na ndege iliyoishiwa mafuta AKA morani AKA mzee wa tripi AKA zungu la Richmonduli AKA Lowasa alivyojaribu kujisafisha kwa kuwatumia kina Balile na wenzake lakini in the process kulipa kisasi kwa kina Mwakyembe na wenzake (JK?) waliomshushua bungeni.

Nimevisikia kwa makini vitisho vya mzee wa vijisenti na kunywa sumu AKA mzee mpenda mbichi (wanafunzi wa shule) AKA mzee wa kashfa kibao kabisa za wizi na ufisadi Tanzania AKA Chenge na lawyer wake kuwa "watalipiza kisasi" na kuwaumbua wote wale wanaowafuatilia kwenye kesi ya wizi.

Nimevisikia pia vitisho vya Patel, Manji, Rostam, Kagoda, Mramba na wezi wenzao kibao kuwa watahakikisha utawala wa nchi na sheria unakuwa mgumu kwa vile watu wanafuatilia ulaji wao. Kwa yote haya, hili la kumtisha hadi Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali yake limefikia kipimo cha juu. Haijalishi kama Mkapa anahusika au ni Apson na wanausalama wenzake. Katika hili hakuna cha mswalie yeyote.

Nimeamua kumpa Kikwete nafasi ili afanye kweli katika hili. Najua kuwa alinidisapointi Butiama lakini kwa sasa nampa tena nafasi nyingine ya kufanya kweli na kuwa supporter wake kila mara anapowachukulia hatua mafisadi. Nitaacha kumpondea Kikwete kwa mwezi mzima (Kikwete-Bashing-Free posts for a month). Niko nawe mheshimiwa sana raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Ingawa najua bado hujafanya chochote kwenye wito wangu wa kupunguza bei ya nishati Tanzania lakini sasa nakupa nafasi tena ya kutokomeza ufisadi na mafisadi toka kwenye serikali yako. Kwa hili utapata free ride toka kwangu na free media attacks kwa wale maadui zako wote watakaojaribu kuleta propaganda zao hapa JF na kwingine kote ambako kazi zangu zinafika.

kwa mwezi mzima, mwafrika wa kike anamuunga mkono Kikwete katika juhudi zake za kutokomeza ufisadi Tanzania.

Asante.

Naona una point za msingi Mwafrika wa kike. Basi tumpe pumzi Kikwete aweze kusafisha ufisadi katika nchi yetu Tanzania ili kuiwezesha hali ya kiuchumi na kisiasa iboreke na maendeleo ya nchi na watu yasonge mbele. Mwenye masikio na asikie.
 
Hivyo vitisho, na mambo atakayoyafanya Kikwete ni sehemu ya usanii ambao watanzania tumeushuhudia tangu tulipoelezwa kuwa maisha bora kwa kila mtanzania ni kitu kinachowezekana
 
MWK,
kama kuna wakati muafaka wa kumweka kikwete under massive pressure basi ni huu......kama unawasha Jiefang vile kwa "handeli," hupunguzi kasi pale linapokaribia kuwaka bali ni kinyume chake(unaongeza), yaani unapulizia moto mpaka uwake kabisaaaa!!!

pulizi, usimpe hiyo "pressure free" holiday........nadhani itakuwa ni makosa kufanya hivyo!!.

YNIM,

I hear you mkuu!

Nilichotangaza hapa ni kuacha Kikwete bashing for a month! Kama kawaida yangu unajua mimi ni mmoja wa wachache wanaopeleka mpira kwa Kikwete kila mara tena kwa lugha ya ki-fix news (courtesy ya Keith Olbermann).

Ninaacha bashing for only a month! Ninajaribu kumtenga Kikwete toka kwenye mafisadi waliomzunguka (ambao ni wengi kupindukia). Ninataka nimuamini kuwa atafanya kitu haraka sana bila kuchelewa na huku akipata cheering squad ya nguvu toka kwa timu yangu. Hii haitazuia thou kuwapiga madongo ccm (as usual) au viongozi uchwara huko serikalini kama Mkullo.

Just another way of doing things for a month!
 
One must have an incredibly inflated ego to speak of oneself in public in the third person. What's even more confounding is placing one's "name" right next to the leader of a country of 34 million plus people in a most nonchalant manner as if you both shared the same VIP status?! What a disgrace!
 
a disgrace to whom?
 
Mwafrika wa kike asante sana kwa kuwakilisha, natumaini hili wazo lilikuwa karibu vichwani mwa kila mmtu

sana ningependa kukumbusha kitisho kingine toka kwa YONA kuwa kama kuna mbabe ampeleke mahakamani(aone)

Pili ningependa kumuombea rasmi raisi wangu wa hii jamuhuri japo umuongezee muda kidogo japo miezi miwili zaidi ili asipate sbb
 
Mwafrika wa Kike,
Kama kweli Kikwete ataweza kuwafikisha mahakamani hawa mafisadi basi wananchi wote watakuwa nyuma yake as a fact naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, mimi hapa nitakuwa mmoja kati ya wapenzi wake toka siku hiyo!
Kwanza yeye kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hizi habari za migahawani haiwezi kabisa kuhatarisha national security ati kwa sababu ya watu wachache wahuni na mafisadi wasiopendwa na wananchi wote.

Nakumbuka enzi za mwalimu alipotangaza Azimio la Arusha, watu walisema kama haya wengine wakaenda misikitini na makanisani kumwombea mabaya wengine hata kuingia msituni lakini - Alichofanya mwalimu kilikuwa kilipewa baraka za watanzania wote.. Washeikh wakubwa wote na Mapadre wakubwa wote..zaidi ya yote yeye ndiye amiri jeshi mkuu na jeshi lote lipo nyuma yake, hivyo vitisho kama hivi haviwezi hata siku moja kupewa nafasi.kama kweli anaweza kufanya afanye hakuna kisingizio.. kiti cha Ikulu amekikalia yeye na sio Lowassa wala Patel.

Kama ningekuwa Kikwete ningeyafanya ya mwalimu, unaposikia fununu kama hizi unamwita mtu IKULU na kumweka kitimoto... akitoka hapo atafute choo kushusha mzigo kwanza.

Naona Mwafrika wa Kike anazo zile taarifa za siri za jinsi Kikwete anavyoushughulikia ufisadi!
Time will tell bana na tutajua tofauti kati ya mchele na chuya!
Tuko mkao wa kula! Tunataka hizo siri hapa!
Hala hala isije kuwa propaganda! adawise time is the factor pamoja na uzima!
 
One must have an incredibly inflated ego to speak of oneself in public in the third person. What's even more confounding is placing one's "name" right next to the leader of a country of 34 million plus people in a most nonchalant manner as if you both shared the same VIP status?! What a disgrace!

POLE SANA NA HIYO copy and paste.....
 
Naona una point za msingi Mwafrika wa kike. Basi tumpe pumzi Kikwete aweze kusafisha ufisadi katika nchi yetu Tanzania ili kuiwezesha hali ya kiuchumi na kisiasa iboreke na maendeleo ya nchi na watu yasonge mbele. Mwenye masikio na asikie.
Si masikio tu tunayo! Bali hata macho ya kuona!
Tunataka ushahidi pls!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom