- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Natumaini mko njema kabisa,katika pita pita zangu kwenye makitaba za kimataifa nimekutana na hii kwamba mtu alie vumbua ndege wakwanza kabisa ni mwafrika amerika 1906 alikuwa anaitwa Charles Fredrick page
Anaejua undani wastory hii anifafanulie maana mi nilijua ni wale watoto wa mchungaji Wright brothers ndo waligundua n.k.
Anaejua undani wastory hii anifafanulie maana mi nilijua ni wale watoto wa mchungaji Wright brothers ndo waligundua n.k.
- Tunachokijua
- Charles F. Page alikuwa na asili ya Afrika aliyezaliwa utumwani, aliishi huko Pineville, Lousioana Marekani na alizaliwa mwaka 1865 na kufariki mwaka 1937. Machapisho mbalimbali yamemuandika Page kama miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa katika uvumbuzi wa ndege hii ni kutokana na ufuatiliaji uliofanywa na mwanahistoria Mike Wynn.
Baadhi ya watu wamewahi kuandika pia kuhusu madai haya. Mathalani, madai ya watu wawili kuhusu uvumbuzi wa page kwenye Mtandao wa X yamehifadhiwa hapa na hapa.
Ukweli upoje kuhusu Charles Page na uvumbuzi wa ndege?
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa taarifa hiyo na kubaini kuwa ni ya kweli ambapo machapisho, makala na tafiti mbalimbali wamemuelezea kwa kina Charles Page na uvumbuzi wa ndege.
Tovuti ya the advocate inaeleza kuwa Charles Page hatajwi na taarifa nyingi kuhusu mchango wake na hamu yake aliyokuwa nayo kuhusu uvumbuzi wa ndege na badala yake taarifa na kumbukumbu nyingi zinawataja ndugu wawili maarufu kama Wright brothers kama wavumbuzi wa ndege.
Idara ya utalii na utamaduni ya jimbo la Louisiana ilichapisha katika tovuti yake kuwa Makumbusho ya Jimbo la Louisiana na Bodi ya Ushauri ya Makumbusho ya Haki za Kiraia ya Louisiana itazindua maonyesho mapya, ambayo yaliyafanyika kuanzia 03-07-2024 na kumalizika tarehe 30-09-2024 katika uwanja wa ndege wa New Orleans International Airport.
Maonesho hayo yalijulikana kwa jina la Pioneer Skies: From Freedom to Flight, the History of Charles Frederick Page yaliyokuwa na lengo la kuonesha utajiri wa historia ya usafiri wa anga.
Mabango yaliyowekwa kwenye maonesho ya Pioneer Skies: From Freedom to Flight, the History of Charles Frederick PageMaonesho hayo pia yalikuwa na lengo la kumuangazia Charles F. Page, mwanamume aliyekuwa mtumwa kutoka Pineville ambaye alivumbua kifaa kirukacho angani na, mwaka wa 1906, wakati wa enzi ya Jim Crow, alipokea hakimiliki ya usafiri wake wa anga, kabla ya Wright Brothers. Hii ilikuwa ni kutambua mchango wa Charles Page katika historia ya usafiri wa anga.
Tovuti ya Towntalk wameandika kuwa Charles Page alikuwa ni muafrika wa kwanza kumiliki hakimiliki ya ndege ambapo wazo la kuunda ndege alilipata mwaka 1898, na miaka mitano baadaye yani mwaka 1903 Page aliunda ndege inayofanya kazi nyuma ya nyumba yake katika eneo ambalo kwa sasa ni kona ya Edgewood Drive na Highway 28 East.
Mwaka 1904 Page aliamua kutumia akiba yake yote kutengeneza kielelezo kamili cha ndege yani (full-scale model of the airplane) na kuisafirisha hadi kwenye maonyesho ya ununuzi ya Louisiana huko St. Louis, Missouri ambapo mshindi angeshinda Dola za kimarekani laki moja lakini kwa bahati mbaya ndege hiyo haikufanikiwa kufika katika maonesho hayo na haijulikani nini kilitokea wakati wa usafarishaji.
Licha ya ndege yake hiyo ya kielelezo kupotea lakini bado alifanikiwa kupata hakimiliki mwezi wa nne mwaka 1906 na alipata hatimiliki hiyo kabla ya wavumbuzi wengine yaani Wright brothers hawajapata ya kwao ambao ndio wanatambulika kama wavumbuzi wa awali katika historia na kumbukumbu nyingine. Licha ya kupata hati miliki hiyo Charles hakuendelea tena kutengeneza ndege na kuipotezea hati miliki aliyopewa na kisha kuendelea na shughuli nyingine.
Mchoro wa uvumbuzi wa ndege uliofanywa na Charles Page
Kwa mujibu wa tovuti ya makumbusho ya jimbo la Lousiana wanaeleza kuwa licha ya Charles Page kukutana na vikwazo vyote hivyo lakini bado pia mafanikio yake kwa kiwango kikubwa yaliendelea kutotambuliwa kutokana na kipindi hiko watu weusi walibaguliwa na kutengwa.