Mwafrika: Alizaliwa paradiso sasa anaishi jehanamu

SpK

Member
Jun 14, 2008
40
4
MWAFRIKA: ALIZALIWA PARADISO SASA ANAISHI JEHANAMU

Afrika ni bara lenye utajiri mwingi, lakini ni bara masikini kuliko yote duniani. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, kati ya nchi 48 masikini sana duniani, 33 zinatoka Afrika, ikiwamo Tanzania.

Zaidi ya hilo, Afrika ndilo bara pekee lenye deni kubwa la nje kuliko mabara yote duniani ambapo mpaka sasa deni hilo limefikia dola za Marekani bilioni 980 [ukiondoa riba], na linazidi kuongezeka. Katika deni hili, Tanzania inadaiwa dola bilioni 40, kabla ya riba.

Huo ni upande mmoja wa hadithi hii ya kusikitisha. Lakini hebu tujiulize: Je, Afrika imechangia nini katika ustaarabu wa dunia, sayansi na teknolojia?. Bila shaka jibu ni: “HAKUNA”, licha ya kwamba Afrika ndipo mahali “alipoumbwa” na kuishi binadamu wa kwanza, maarufu kwa jina la “Zinjathropus”.

Tujiulize tena: Je, Afrika imechangia nini cha maana na cha kukumbukwa, katika nyanja za maendeleo, elimu na utamaduni wa dunia?. Hapa tena jibu ni: “HAKUNA”, licha ya kwamba Waafrika wa kale wanajulikana kuwahi kuongoza duniani katika fani za madawa na tiba, sheria, mahesabu na utawala enzi za dunia ya kale, kabla watu weupe hawajaamka, wakigwaya kwa umbumbumbu.

Kwa mfano, Ethiopia [Uhabeshi au Absaynia] ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na mfumo madhubuti wa utawala, na watu wake walikuwa wa kwanza kuanzisha utaratibu wa “kuabudu” Mungu kabla watu wengine hawajamjua Mungu mmoja. Hadi kufikia karne ya 17, Ethiopia ilikuwa ikijulikana kwa “Wavumbuzi” kama nchi ya Mtakatifu Prester John.

Wataalam wa kwanza wa sayansi ya nyota na anga duniani [astronomers] walikuwa Waethiopia [Afrika]. Nao Wagiriki wa kale walijifunza elimu ya hesabu za maumbo [geometry] kutoka Ethiopia. Wanahistoria ya kale wanakubaliana kwamba Wamisri na Waethiopia wa enzi za kale walikuwa “weusi ti kama mkaa”.

Mwanahistoria Fabre d’Olivet anatanabahi kwamba hapo zama za kale ya kale, “Waafrika walitawala na kuongoza ulimwengu na dunia karibu katika nyanja zote [sayansi, teknolojia, nguvu na uwezo], na walidhibiti Afrika na sehemu kubwa ya bara la Asia”.

Fabre anafafanua kuwa, wakati Waafrika wakiongoza katika nyanja hizo, kabila la watu weupe lilikuwa lingali legelege, lisilo na ustaarabu kiwango cha kufananishwa na wanyama [savage]; hawakuwa na uwezo wa kufikiri wala kuwa na matumaini katika maisha.

Kuhusu uvumbuzi wa nchi mpya [New lands], ni Waafrika waliovumbua Amerika na Visiwa vya “West Indies”, na si Vespucci Amerigo na Christopher Columbus, kama inavyoelezwa na Wanahistoria wa Kizungu.

Profesa Leo Weiner, katika kitabu chake kiitwacho “Afrika na Uvumbuzi wa Amerika” [Africa and the Discovery of America], anabainisha kuwa Waafrika walizifikia nchi za Magharibi mapema kabla ya Wavumbuzi wa Kizungu, na huko waliendesha biashara na wenyeji wa nchi hizo kwa mafanikio.

Profesa Weiner anatoa ukweli kwa kusema kwamba, Waafrika waliwahi kuifanya Amerika koloni lao na kuitawala kama Wazungu walivyokuja kutawala nchi zetu baadaye.

Vivyo hivyo, “Wavumbuzi” wa Kihispaniola wanakiri kwamba, walipofika kwenye “nchi mpya” [Amerika na West Indies], walikuta makazi na himaya za Kiafrika katika nchi hizo ambapo Makao Makuu ya Kudumu ya Himaya ya Waafrika yalikuwa katika mji wa Darien, mwaka 1513.

Naye mwanahistoria Harold G. Lawrence, katika kitabu chake kiitwacho, “Wavumbuzi wa Kiafrika wa Dunia mpya” [African Explorers of New World], anaeleza kuwa, alipofika katika visiwa vya “West Indies”, Christopher Columbus alifahamishwa na wenyeji wa visiwa hivyo juu ya uhusiano wa kibiashara uliokuwapo, kati yao na Waafrika. Lawrence ameandika ukweli huu kwa kutumia shajara [diaries] za Columbus za enzi hizo zilizohifadhiwa hadi leo. Kwa hiyo, hizi sio habari za kubuni au kubahatisha, bali ni historia sahihi kuhusu ukuu na ustaarabu wa Mwafrika dhidi ya, na kabla ya ustaarabu wa Mataifa mengine duniani.

Si hivyo tu, nafasi ya Mwafrika katika kuustaarabisha ulimwengu ilitambuliwa pia na Wafalme wengi miaka mingi kabla ya Kuzaliwa Kristo [BC].

Alexander the Great, Mtawala na Jemadari Mkuu wa himaya ya Rumi ya kale, alikuwa na Jenerali Kiongozi wa Jeshi Mwafrika katika jeshi lake, miaka ya 330 Kabla ya Kristo. Jenerali huyu aliitwa “Clitus the Black”. Vivyo hivyo, jeshi la Wagiriki la enzi hizo liliongozwa na Majenerali na Ma- “Brigadier” wa Kiafrika.

Katika historia ya hivi karibuni, [karne ya 18], Mwafrika aliyeitwa Abraham Hannibal, alikuwa Amiri Jeshi Mkuu [General-in-chief] wa Jeshi la Urusi chini ya Binti wa Mfalme [Empress] Elizabeth; na aliendelea kushika cheo hicho cha ukuu wa jeshi hadi utawala wa Mfalme “Peter the Great”. Kwa ushujaa wake alitunukiwa nishani na medali ya “The Red Ribbon of Order of Saint Alexander Newski”. Mmoja wa watoto wake aliongoza majeshi na kushinda vita kati ya Warusi na Waturuki huko Navarin, mwaka 1770.

Mwafrika mwingine, Michael Egypteous, alikuwa Meja Jenerali katika Jeshi la “Peter the Great” ambaye, bila mipango yake, sayansi na mbinu zake za kisheshi, Jeshi la Urusi halikufanya kitu.

Kuhusu uongozi wa kanisa Mwafrika hakuwa nyuma. Kati ya mwaka 189 na 496 Baada ya Kristo [BK], Kanisa Katoliki, ambalo ndilo lilikuwa Kanisa pekee la Kikristo duniani enzi hizo, liliongozwa na Ma-papa [Popes] Waafrika. Hawa walikuwa ni Papa Victor, aliyeongoza Kanisa kati ya mwaka 189 na 199; Papa Melchiades, 311 – 312; na Papa [Mtakatifu] Gelasious, mwaka 496.

Katika kipindi kifupi cha utawala wake, Papa Gelarious anakumbukwa kwa kufanya mabadiliko makubwa katika utawala wa Kanisa. Alirekebisha kalenda ya Watakatifu baada ya kutafakari upya nafasi za Watakatifu kwa waumini na Kanisa, akaondoa katika orodha hiyo majina ya Watakarifu Magreth na Mtakatifu George.
Aliingiza katika Biblia Takatifu vitabu vipya vya “Hekima [ya Mfalme Sulemani]”, Yudith, Makabayo, Tobit, na Mhubiri ambavyo viliachwa na kutumiwa na Mapapa waliomtangulia. Alipiga marufuku sherehe za kipagani kuhusishwa na Kanisa [Soma: Book of the Popes: Liber Pontificulis].

Leo, inahesabiwa ni “dhambi” kwa Papa kutoka Afrika alikotokea binadamu wa kwanza “Zinjanthropus”, kwa sababu tu Afrika ni bara la “giza”, na kwamba Papa wa kweli lazima atoke nchi za Weupe kwa uteuzi kwa njia ya “moshi mweupe”. Ni kufuru gani hiyo kwa binadamu, ubinadamu na uumbaji?

Nao Wafalme wa Ufaransa wa karne ya 18 walikuwa na madaktari wa Kiafrika wa kupima, kutibu na kutunza afya zao; kwa maana kwamba Madaktari weupe hawakufua dafu kwa Madaktari weusi kwa ujuzi na taaluma.

Wakati Mfalme Charles wa VII alihudumiwa na daktari Mwafrika aliyeitwa Aden Ali, Mfalme Louis wa XI alikuwa na daktari Mwafrika aliyeitwa Antoine de Negrie, au “Anthony Mweusi”.

Haya ni matukio yaliyo wazi na ambayo waliokuwa Wakoloni wetu hawawezi kujifanya kutoyafahamu bila ya aibu. Hawa Waingereza wanaojitapa kwa ustaarabu [wao?] wa Magharibi walioupandikiza kwetu, si lolote bali ni mbinu tu ya kuficha historia ya ukuu na utukufu wa Mwafrika. Hebu angalia ukweli ufuatao juu ya hiki tunachosema: Kati ya mwaka 208 na 211 [BK] Uingereza ilitawaliwa na Mfalme Mwafrika aliyeitwa Septimus Severus, na Makao Makuu ya Serikali yake yalikuwa katika mji wa York.

Si huyo tu aliyeongoza Uingereza, kwani mapema kabla ya hapo, karne ya saba, Ireland nayo ilikuwa na Askofu Mwafrika, aliyeitwa [Mtakatifu] Diman “the Black” au “Dimani Mweusi” aliyefariki mwaka 658.

Ni vyema pia kufahamu kwamba, karibu uzao wote wa familia za Kifalme barani Ulaya, ni chotara wenye damu ya Kiafrika; wote hawa ni wa asili ya ukoo wa Mfalme John wa VI wa Ureno na mwanzilishi wa nchi ya Brazil ya sasa, ambaye alikuwa ni Mwafrika.

Mwanae mfalme John, aliyeitwa Pedro wa I, alifanywa Mfalme wa Brazil mwaka 1822; akamwoa dada yake na mke wa pili wa Napoleon, mfalme na Jemadari machachari wa Ufaransa, na kupandikiza damu ya Kiafrika katika ukoo wa Kifalme wa Ufaransa.

Binti ya Pedro, aliyeitwa Gloria, alifanywa Malkia wa Ureno na alikuwa wifi yake na Malkia Victoria wa Uingereza.

Katika mlolongo huu wa kurithi na kurithishana falme, ni dhahiri kwamba, hata Malkia [wa sasa] Elizabeth wa II wa Uingereza ana damu ya Kiafrika atake asitake. Kwa jinsi hii Waafrika ni mababu wa Waingereza na Wazungu wengine wenye damu ya Kifalme.

Kwa nini urithi huu wa Mwafrika umefagiwa na kufunikwa chini ya zuria, na historia kupotoshwa. Ni kwa sababu ya biashara ya utumwa iliyoanzishwa na kusimamiwa na Wazungu wenyewe. Wazungu hao walitaka kuhalalisha unyama wao kwa Waafrika kwa kupotosha historia kwa kudai kwamba, kihistoria, Mwafrika alikuwa binadamu asiyestaarabika aliyeishi katika bara la “giza”.
Inakadiriwa kuwa, Waafrika kati ya milioni 10 na 20 waliuzwa utumwani nchi za nje, na wengine kati ya milioni 60 na 150 walikufa katika vita vya kukamata watumwa; au walifia njiani wakipelekwa kuuzwa nje ya Afrika.

Walipokuja Afrika, Wakoloni waliharibu kumbukumbu zote za historia na mifumo ya Kijamii ya Kiafrika ili kujenga na kuthibitisha dhana yao potofu kwamba, Mwafrika hakuwa na historia hadi alipokuja Mzungu, na sisi mpaka sasa tuko kimya kwa hilo.

Kama Afrika limekuwa bara kiongozi katika maendeleo ya historia ya binadamu tangu kale na sasa ni kinyume chake; limefanywa “jamvi” la Wageni kutoka nchi za Magharibi. Na kwa sababu Mwafrika amekubali kufanywa jamvi la wageni, amekosa kauli katika nyanja za maendeleo Kimataifa, alizaliwa Paradiso, sasa anaishi Jehanamu!.

Afrika iliumba binadamu wa kwanza [Zinjanthropus] ambaye ndiye chimbuko la binadamu na mataifa yote; binadamu huyo alitokea Oldvai George nchini Tanzania. Nao Wasemiti [Semites], kabila linalojumuisha Waarabu na Wayahudi, waligundua Mungu [aliyemuumba Zinjanthropus?] katika mlima Sinai na huko Makka.

Ni kitu gani walichofanya watu Weupe wa Ulaya Magharibi hata kuteka fikra, historia na uwezo wetu sisi Waafrika na Wasemiti?

Ulaya iliunda dunia [anamoishi Zinjanthropus?] kwenye mstari wa Greenwich Meridian. Ni Wazungu hao hao walioyapa majina mabara yote ya dunia, bahari zote, mito mikubwa yote na nchi zote.

Ni Wazungu hao walioamua ramani ya dunia iwe ilivyo sasa na kushinikiza tufikiri na kuamini kwamba bara la Ulaya liko juu ya Afrika badala ya Afrika kuwa juu ya bara la Ulaya.

Wazungu ndio walitoa na kupanga muda na majira ya dunia kwa kushinikiza kwamba, mstari wa Greenwich Meridian ndio unaoamua mida na saa za nchi na mataifa.

Zaidi ya hayo, ni Wazungu walioamua bara lipi lianzie wapi na liishie wapi. Kwa Afrika, ni wao walioamua bara hili liishie bahari ya Shamu [Red Sea] badala, kwa mfano ya kuishia Ghuba ya Uajemi/Uarabu.

Je, huu ndio mchango pekee unaoipa Ulaya haki ya kutawala na kuheshimiwa na watawala wa mabara mengine ya dunia, badala ya heshima hiyo kwenda kwa bara lililoumba binadamu wa kwanza, au lile lililovumbua Mungu?

Hatudhani kwamba hivyo ndivyo, bali ni ujinga wetu na akili tegemezi ya kitumwa inayotufanya tufungue milango kirahisi kwa “utumwa mpya”. Haiingii akilini, kwamba sisi ambao ndio chimbuko la binadamu wa kwanza na mataifa, leo tunakubali kupokea historia tofauti ya binadamu, kwa kufanywa binadamu wa mwisho katika mataifa.

Tatizo la Afrika ni uongozi. Hatujapata kina Mussa, kina Julius K. Nyerere au Kwame Nkrumah, wa kutuongoza kutoka utumwani “Misri”, kutuvusha jangwa kwenda nchi ya ahadi – Kanaani mpya.

Wako wapi kina Mussa na Haruni wetu kuweza kukata minyororo ya Farao kwa sauti ya mamlaka na nguvu “Waache watu wangu waende”?

Kiongozi mtumwa hawezi kuwakomboa watumwa wenzake kutoka utumwani. Viongozi wengi wa Kiafrika ni watumwa wa mfumo wa dunia unaomilikiwa na Ulaya Magharibi. Angalia ilivyo: Afrika huru inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watawala madikteta kuliko bara lingine duniani; Afrika imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na majanga mengine ya kujitakia mengi kuliko bara lolote katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Kutoka Algeria hadi Zimbabwe, hakuna Kiongozi wa nchi aliye tayari kukaa meza moja na Wapinzani wakuu wa Kisiasa nchini mwake ili kutatua matatizo muhimu ya kitaifa. Lakini Viongozi hao hao wako tayari kukutana na Mamluki, vibaraka na mashirika mumiani ya kimataifa na “Wafadhili” nje ya nchi zao, eti kujadili kile kinachoitwa “mambo muhimu ya kitaifa”, kwa mtazamo wa nchi za Magharibi, ambapo ukweli lengo kuu ni kuziuza nchi zao na watu wao kwa “Washirika” hao kwa manufaa binafsi ya kisiasa.

Afrika imefungua milango kwa sera za utandawazi bila kuelewa maana yake na athari zake. Utandawazi si dhana mpya, bali ni aina Fulani ya ukoloni mkongwe ulioanzishwa karne nyingi zilizopita. Ni mtindo uliojikita katika dini, ujenzi na upanuzi wa himaya, uchumi na teknolojia tegemezi.

Azma kuu ya Utandawazi leo ni kuhakikisha ushindi kwa ubepari na nguvu ya soko kwa kilio na kusaga meno kwa mafukara wa dunia hii. Utandawazi ni silaha ya kiuchumi kwa nchi tajiri dhidi ya nchi masikini, basi.

Ni bahati mbaya [na ilishangaza pia] kwamba Mwenyekiti Mwenza wa Tume ya Kimataifa ya Utandawazi alitoka Tanzania, moja ya nchi masikini sana duniani ambapo pia ndipo chimbuko la binadamu wa kwanza – Zinjanthropus wa Olduvai George. Tayari Tanzania inasifiwa kwa “kuongoza” kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji barani Afrika. Kama hiyo ni sifa ya kweli au kejeli, wanaojishughulisha kujua wanaelewa. Je, si kweli kwamba Tanzania inaongoza katika Afrika kwa kuibiwa rasilimali zake bila ya udhibiti wa kutosha?.

Tanzania sasa inaongoza duniani kwa uwekezaji huria [bila udhibiti] katika sekta ya madini na Viwanda vya Pombe. Je, si kweli kwamba Mtanzania wa mwaka 2004 ni masikini zaidi kuliko Mtanzania wa miaka 50 iliyopita? Je, si kweli kwamba Tanzania imekosa dira ya uchumi tangu “Ujamaa” utundikwe msalabani huko Zanzibar, mwaka 1992?.

Kama hali hii ndivyo ilivyo, hofu yetu ni kwamba, kama [Tanzania] ilivyokuwa chimbuko la binadamu wa kwanza duniani, basi Tanzania hiyo hiyo inaweza kugeuka chimbuko la angamio la Mwafrika na kupotea kwa “Paradiso” ya Zinjanthropus kwa laghai ya Utandawazi.
 
Deodat

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
1,275
271
Hiyo historia imeshiba. Nimependa jinsi ulivyoweza kuunganisha chimbuko la Mwafrika mpaka kwenye changamoto zinazotukabili leo, ukweli ni kwamba wazungu sasa wanatuona siye mavuvuzela fulani hivi ndio maana wanatuendesha watakavyo na viongozi wetu wapo wanachekacheka tu!
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,984
5,920

Kufuatia heading ya hii thread maanake amekwisha kufa, na wala Mbinguni haendi; halafu ile hukumu ya mwisho kwa mujibu wa maandiko ya dini ilishafanyika!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom