Mwafaka wawa mwiba Butiama

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Mwafaka wawa mwiba Butiama
Mwandishi Wetu, Butiama
Daily News; Saturday,March 29, 2008 @19:01

SUALA la Mwafaka ambalo ni ajenda kuu kati ya nne zilizowakutanisha wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kijijini Butiama linaonekana kuwa gumu kutokana na baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar kupinga baadhi ya yaliyokubaliwa na pande zote.

Habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM ambayo ilikutana jana kwa saa sita, zilieleza kuwa mvutano huo unatokana na wajumbe wa Zanzibar hasa waafidhina kupinga wazi kuundwa kwa serikali ya mseto kama ilivyoafikiwa na wajumbe wa CCM.

Mvutano huo ndiyo uliochelewesha kumalizika kwa kikao hicho cha Kamati Kuu ambacho ndicho kinachoandaa ajenda kwa ajili ya kikao cha NEC. Kutokana na mvutano huo kikao hicho cha Kamati Kuu ambacho kilitarajiwa kuwa kifupi kilijikuta kinamalizika saa 10 jioni baada ya kuanza saa 4 asubuhi.

Kutokana na hali hiyo hata kikao cha NEC kilichelewa kuanza badala yake kikaanza jana saa 11 jioni. Ajenda nyingine zitakazojadiliwa kwenye kikao hicho ni ripoti juu ya ufisadi wa Richmond na wa Benki Kuu na hali ya uchumi.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu vilisema kuwa wajumbe wa Zanzibar walionyesha wazi kutoafikiana na kuingizwa kwa CUF ndani ya serikali inayoongozwa na CCM visiwani humo.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad aliwahakikishia wanachama wa chama chake kuwa tayari mazungumzo hayo yamekamilika na wamekubaliana kuunda serikali ya mseto kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Maalim Seif alisema pia kuwa wamekubaliana kimsingi kuwa katika uchaguzi ujao chama kitakachoshinda kwenye uchaguzi mkuu kitakuwa na rais huku chama cha siasa kinachofuatia kwa idadi kubwa ya kura kitatoa waziri kiongozi.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa CUF makubaliano hayo tayari yameshaafikiwa na chama chake na yanasubiri kauli ya CCM. Vyama hivyo vilianza majadiliano ya kutafuta dawa ya mpasuko wa siasa Zanzibar Januari 17 mwaka juzi.

CUF ambacho kimeonekana kuwa wazi kuzungumzia yaliyokubaliwa kwenye mwafaka huo kimekuwa kinawasihi viongozi wa CCM hasa wale wa Zanzibar kukubaliana na makubaliano hayo kuleta utengamano wa siasa visiwani humo.

Baada ya kauli hiyo ya CUF, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba alisema atatangaza makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo hayo ya mwafaka katika kikao hicho cha Butiama.

Katika kipindi chote cha mazungumzo Makamba hajawahi kuwa wazi na masuala ambayo yamekubaliwa katika vikao hivyo ambavyo vyama vyote vinawakilishwa na wajumbe sita.

Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyeamua kuanzishwa kwa mazungumzo baina ya vyama hivyo kwa kile alichoamini kuwa matatizo ya ndani ya visiwa hivyo yanamalizwa na vyama hivyo bila kushirikisha watu kutoka nje ya nchi.
 
Ni wazi kwamba kuafikiana(muafaka) hakujawepo bado na sababu za hali hiyo ziko nyingi sana,ikiwemo na kutoeleweka vyema kwa dhana yenyewe ya mpasuko wa kisiasa.

Wapo watu hususan ndani ya CCM, wanaoona kwamba kwa kuafikiana kwao kuunda serikali ya pamoja kutapunguza nafasi zao za ulaji.

Vile vile si rahisi kwa CCM kukubali uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa maana licha ya kwamba chama hicho hakina sera hiyo hata viongozi wake hawana nia hata kidogo.

Aidha hata wangeafikiana,bado jambo hilo lingekuwa na utata kwani si la wazanzibari wote/waliowengi. Fikiria kwa mfano,huko mbele ya safari chama kingine tofauti na hivyo viwili kikatokea kushinda uchaguizi huko visiwani,kitaukubalije utaratibu wa chama kilichofuatia kwa kura kumtoa waziri kiongozi wakati hakikushirikishwa katika makubaliano hayo. Hapana budi mswada wa muafaka huu ukavishirikisha vyama vyote vya siasa.
 
Muafaka, muafaka ! jamani kwani siku zote tulikuwa tunaishi vipi ? vitu vingine bana vinachefua na kuongeza matatizo tu !
 
Muafaka, muafaka ! jamani kwani siku zote tulikuwa tunaishi vipi ? vitu vingine bana vinachefua na kuongeza matatizo tu !

Ama kweli wewe umekunywa maji ya bendera ya CCM. Yaani hadi leo 2008 hujui kinachoendelea duniani???? Jamani wewe unaishi CUBA au ndo zile sera za Mugabe kuwa Mpinzani hawezi kuongoza serikali. Labda nikusaidie kidogo, nafikiri ingekuwa jambo la busara kama ungemuuliza Mwanachama mwenzako Rais mstaafu A.H. Mwinyi kuwa sasa hivi tunaishi katika mazingira gani. Akishindwa kukujibu basi kwa manufaa ya wale wote ambao hawajui kuwa tuko katika kipindi gani nitatoa jibu hapa. Hata Mwenyekiti wako Taifa anajua hilo, hivyo kama unaweza vilevile kuuliza hilo swali kwake kama hutajali.
 
suala nadhani sio kuishi cuba au hawaii, bali ninachojaribu kuuliza ni kwamba, kabla ya kusikia malalamiko ya muafaka hapo awali, tulikuwa tumeweza kuishi vipi iweje sasa hivi kuwe kugumu kiasi hiki bila ya kupita siku 2 tukasikia tena the same kind of shi*tty arguments kama hizi za muungano ? this argument is taking a toll on our people. Hili ni suala muhimu but at the same time shitty as well, kama sio watu kujinufaisha kisiasa basi ni umbumbumbu tu wa viongozi wetu ! Get together and finish this argument up nyinyi viongozi tanzania !
 
this argument is taking a toll on our people. Hili ni suala muhimu but at the same time shitty as well, kama sio watu kujinufaisha kisiasa basi ni umbumbumbu tu wa viongozi wetu ! Get together and finish this argument up nyinyi viongozi tanzania !

Afadhali umegundua kuwa kuna aina fulani ya usanii unaofanywa na viongozi wetu (lakini si kutokana na umbumbu kama ulivyosema kwani wanajua wanachokifanya).
Kama wasipopashwa, sioni wataamka namna gaani na kulimaliza suala hili once and for all kwa sababu wananufaika nalo na kama litaisha ina maana manufaa yatakwisha pia. Inabidi itafutwe namna ya 'kuwalazimisha walimalize ili tuangalie na mengine yaliyo muhimu pia
 
Kada haupo TZ,nakama upo TZ then sias ya TZ iko pembeni,hivi hujui matatizo ya ZNZ uje ulize leo eti kwani walikua wanaishije,hivi huji kama kulikua na wizi wa kura ktk uchaguzi wa 2005?Hujui kama kuna watu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa?Sema lingine lakini sio suala la kwanini muafaka babdo unahitajika.

Hili suala la Muafaka tulisema mapema kabisa kwamba kwa sisiem hii itakua ngoma nzito si tunawajua CCM bwana.
 
Attachments

  • kp 44.jpg
    kp 44.jpg
    13 KB · Views: 44
Kada haupo TZ,nakama upo TZ then sias ya TZ iko pembeni,hivi hujui matatizo ya ZNZ uje ulize leo eti kwani walikua wanaishije,hivi huji kama kulikua na wizi wa kura ktk uchaguzi wa 2005?Hujui kama kuna watu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa?Sema lingine lakini sio suala la kwanini muafaka babdo unahitajika.

Hili suala la Muafaka tulisema mapema kabisa kwamba kwa sisiem hii itakua ngoma nzito si tunawajua CCM bwana.

Sisi tunao fuatilia mambo tunakumbuka siku za nyuma hawa wana CCM walisema kwa viapo kwamba CUF hawatakaa washike dola ama washiriki basi naona kama CCM bara ama NEC wanataka kusema kuweopo mseto hawa walio toa haya matamshi na leo kabla hawajafa wanataka kuona CUF iko nao katika madaraka wanaumia so wanaleta zengwe lakini wajue kwamba Tanzania si mali ya CCM ni yetu sote na kuanzia hapo majeshi yajue kwamba yapo kwa Tanzania na si CCM .Ni bora wakaamua maana maamuzi ya CUF yako clear kabisa sasa wacha CCM wajikanyage
 
Jamni nasikia kuwa Mkapa,Mzee Mwinyi, Salim na Salmin hawajahudhuria huko?kwa nini iwe hivi?
 
Jamni nasikia kuwa Mkapa,Mzee Mwinyi, Salim na Salmin hawajahudhuria huko?kwa nini iwe hivi?

salmini mgonjwa, hao wengine sijui vipi.

sasa wakuu wamefikia wapi kuhusu suala hili?

kwa kweli bila ya kutafuna maneno ccm zanzibar kwao hili ni gumu kulikubali. na wakilazimishwa kulikubali kazi ktk utekelezaji.

hata hivyo mwanzo huwa mgumu lkn baadae hali itazoweleka.

hatua zetu nyngi za mwanzoni huwa ngumu hata kwenye maisha baadae huwa sawa tu
 
..wana udhuru!

kwa kiswahili sanifu tunasema wamejikata na mapema maana kuna hatari ya mtu kuumbuliwa na kundi lake na ikawa mwanzo wa kukurupushwa ,hivyo kutokuwepo kwao kutapunguza kasi hasira na nguvu za kundi la wahenga.
 
..si unajua tena,mkubwa haambiwi toka!
 
Muafaka, muafaka ! jamani kwani siku zote tulikuwa tunaishi vipi ? vitu vingine bana vinachefua na kuongeza matatizo tu !

Badala yakuweka signature ya picha ya Passport kuonyesha UmTZ ni bora uweke kadi yako ya CCM tu hapo chini kwani mawazo yako si ya MTZ anayeitakia KHERI nci kama walivyo CCM wote.
 
suala nadhani sio kuishi cuba au hawaii, bali ninachojaribu kuuliza ni kwamba, kabla ya kusikia malalamiko ya muafaka hapo awali, tulikuwa tumeweza kuishi vipi iweje sasa hivi kuwe kugumu kiasi hiki bila ya kupita siku 2 tukasikia tena the same kind of shi*tty arguments kama hizi za muungano ? this argument is taking a toll on our people. Hili ni suala muhimu but at the same time shitty as well, kama sio watu kujinufaisha kisiasa basi ni umbumbumbu tu wa viongozi wetu ! Get together and finish this argument up nyinyi viongozi tanzania !

KM

bana acha hizo,nenda kuleeeeeee kijiwe cha BITOZI/BRAZAMEN kuna mambo mapya ameweka,mie mwenzako nimeshazichoma hapa zile vituzs ahhhhh taratibu naburudika roho.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom