BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,847
Mwafaka wawa mwiba Butiama
Mwandishi Wetu, Butiama
Daily News; Saturday,March 29, 2008 @19:01
SUALA la Mwafaka ambalo ni ajenda kuu kati ya nne zilizowakutanisha wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kijijini Butiama linaonekana kuwa gumu kutokana na baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar kupinga baadhi ya yaliyokubaliwa na pande zote.
Habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM ambayo ilikutana jana kwa saa sita, zilieleza kuwa mvutano huo unatokana na wajumbe wa Zanzibar hasa waafidhina kupinga wazi kuundwa kwa serikali ya mseto kama ilivyoafikiwa na wajumbe wa CCM.
Mvutano huo ndiyo uliochelewesha kumalizika kwa kikao hicho cha Kamati Kuu ambacho ndicho kinachoandaa ajenda kwa ajili ya kikao cha NEC. Kutokana na mvutano huo kikao hicho cha Kamati Kuu ambacho kilitarajiwa kuwa kifupi kilijikuta kinamalizika saa 10 jioni baada ya kuanza saa 4 asubuhi.
Kutokana na hali hiyo hata kikao cha NEC kilichelewa kuanza badala yake kikaanza jana saa 11 jioni. Ajenda nyingine zitakazojadiliwa kwenye kikao hicho ni ripoti juu ya ufisadi wa Richmond na wa Benki Kuu na hali ya uchumi.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu vilisema kuwa wajumbe wa Zanzibar walionyesha wazi kutoafikiana na kuingizwa kwa CUF ndani ya serikali inayoongozwa na CCM visiwani humo.
Hivi karibuni Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad aliwahakikishia wanachama wa chama chake kuwa tayari mazungumzo hayo yamekamilika na wamekubaliana kuunda serikali ya mseto kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010.
Maalim Seif alisema pia kuwa wamekubaliana kimsingi kuwa katika uchaguzi ujao chama kitakachoshinda kwenye uchaguzi mkuu kitakuwa na rais huku chama cha siasa kinachofuatia kwa idadi kubwa ya kura kitatoa waziri kiongozi.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa CUF makubaliano hayo tayari yameshaafikiwa na chama chake na yanasubiri kauli ya CCM. Vyama hivyo vilianza majadiliano ya kutafuta dawa ya mpasuko wa siasa Zanzibar Januari 17 mwaka juzi.
CUF ambacho kimeonekana kuwa wazi kuzungumzia yaliyokubaliwa kwenye mwafaka huo kimekuwa kinawasihi viongozi wa CCM hasa wale wa Zanzibar kukubaliana na makubaliano hayo kuleta utengamano wa siasa visiwani humo.
Baada ya kauli hiyo ya CUF, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba alisema atatangaza makubaliano yaliyofikiwa katika mazungumzo hayo ya mwafaka katika kikao hicho cha Butiama.
Katika kipindi chote cha mazungumzo Makamba hajawahi kuwa wazi na masuala ambayo yamekubaliwa katika vikao hivyo ambavyo vyama vyote vinawakilishwa na wajumbe sita.
Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyeamua kuanzishwa kwa mazungumzo baina ya vyama hivyo kwa kile alichoamini kuwa matatizo ya ndani ya visiwa hivyo yanamalizwa na vyama hivyo bila kushirikisha watu kutoka nje ya nchi.