Mwacheni Rais afanye kazi yake kwa mujibu wa Katiba JMT

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,195
1,417
Nimefatilia mijadala inayoendelea kwenye vyombo vya habari hususan wapinzani nikagundua kuna upotoshwaji mkubwa.

Kwanza naomba kuwakumbusha Rais wa JMT Mhe. Samia Suluhu Hassan anafahamu mambo mengi kwani alikuwa msaidizi namba moja wa Hayati Dr. Magufuli.

Wakati huo huo chama kinachotawala ni kilekile CCM! Hivyo basi, tumuache Rais wetu afanye kazi bila kupandikiza chuki ya namna yoyote ile kwa mtangulizi wake.

Tukumbuke kama ni kutumbua hata mtangulizi wake alikuwa anatumbua kuonesha wanaosimamia ni wanadamu na sio malaika. Sio kila uovu utakaobainika iwe ni lazima Hayati Magufuli alihusika.

Ukisoma hasara ya mashirika mbalimbali ya ndege ikiwemo Kenya Airways, iliyopata hasara ya zaidi ya bil 330, utagundua ni changamoto ya dunia.

Ukija Bandari tumeona hata Mhe. Mwinyi kule Zanzibar akitumbua, hata hivyo hakuwa na maana Mhe. Shein hakufanya kazi. Pia TL akumbuke PM, Mhe. Majaliwa alifanya uchunguzi TPA na alimsimamisha kazi mpaka DF nk. Hivyo huu ni mwendelezo tuache kebehi ndg zangu wapinzani.

Mwisho TL akumbuke alituambia waliompiga risasi anawajua. Na akumbuke sio lazima kuwa walitumwa na Rais, kwanini hawataji? Neno la Mungu linasema mtaijua kweli na hiyo kweli itawaweka huru.

Mwisho, nawashauri ndg zangu JF, tumpe ushirikiano wote Rais wetu wa JMT kwa kufichua uovu na hakika ataufanyia kazi mwana ni msikivu.

JF ilikuwa zaidi ya huyo mtufulani huko tuita, ni wakati sasa JF yetu irudi. Kikubwa admns au moderators muwe wakali hatutaki lugha za kuudhi au matusi!

Kazi inaendelea hakuna kulala.
Viva Rais Samia Vivaaa!
Viva Tanzania Vivaaaa!
Viva JF Vivaaaaa!
 
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
umeamua kubadili gia angani?that's very nice
emoji108.png
ngoja na wengine waje sisi kama wapinzani tumefurahia Mama Rais alivyoanza kazi yake siku ya leo muda wa kuabudu mtu ushaisha muda wake
 
umeamua kubadili gia angani?that's very nice ngoja na wengine waje sisi kama wapinzani tumefurahia Mama Rais alivyoanza kazi yake siku ya leo muda wa kuabudu mtu ushaisha muda wake
Mwenye akili yoyote anafahamu hili na halihusu kubadili gia angani. Kumbuka Mhe. Samia anatokana na CCM!
 
Back
Top Bottom