Mwacheni Dk. Slaa, jibuni hoja - Mwanahalisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwacheni Dk. Slaa, jibuni hoja - Mwanahalisi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kizimkazimkuu, Sep 9, 2010.

 1. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Ifuatayo ni sehemu ya makala iliyoandikwa na mwandishi maalum na kuchapishwa na gazeti la mwanahalisi la tarehe 8-14,Septemba 2010..nimechagua baadhi ya vipengele vilivyonigusa

  ''wapo tunawaowajua hata kwa majina ambao hawaaminiwi na wake zao kukaa karibu na mabinti zao wa kuwazaa!Tunawajua wanaotunza watoto wanaodai ni wa mitaani,lakini mama zao wa mitaani wanasema ''ni watoto wa hao wanaowatunza'.


  Nina uhakika kabisa baadhi ya wa urais hawawezi kujibu maswali ya maisha binafsi aliyoulizwa Dk. Slaa:wathubutu tuone.

  Kama masuala ya maadili binafsi na hali ya ndoa za wanasiasa wetu ndio yatakaayoamua kinyang'anyiro hiki basi tujiandae kwa makubwa.Hii ni kwasababu baadhi ya wanasiasa,wanaishi maisha ya shaka kuhusu afya zao na afya za ndoa zao.Wengi wanaishi kwa matumaini na ni suala la muda tu kusubiri tutangaziwe msiba wa kitaifa (Mola apishe mbali)

  Hakuna linalofichika chini ya mbingu,na hata hatua chafu ya kuwatoa roho baadhi ya wasichana ili kufichwa yasiyofichwa yanajulikana na baadhi ya wasichana wameonana na wanasheria kuandikisha maelezo ili likitokea la kutokea wauaji hao wajulikane


  Ninawashauri wana CCM wenzagu,mwili wangu uko CCM lakini roho haiko huko,wajikite katika kujibu hoha za dr. Slaa,na kuachana na mambo ya ndani ya suruali na sketi za watu. Maana tulio na taarifa za kina kuhusu maisha binafsiya vigogo wa CCM tutalazimika kuingia hadharani endapo gazeti la serikali na yale yanayomilikiwa na watuhumiwa wakuu wa ufisadi yataendelea kutuchelewesha kwa kujadili masuala binafsi badala ya masuala ya maendeleo.

  soma mara mbili kwenye maandishi ya rangi nyekundu
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  tunajua mengi ila tunaona sio busara kuzungumzia maisha binafsi mhasa ya kindoa na mahusiano kwani haitusaidii na zaidi ni kwamba watu tukiamua kuwaweka hadharani basi wengine badala ya kuanguka tu watazimia kabisa kwa kutoamini macho yao kuwa tunayajua mengi yao........
   
 3. p

  pierre JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kiujazacho moyo wa mtu ndicho kimtokacho.Mnaweza kuona kuwa wenzao wakati wanatafuta jinsi ya kulikomboa taifa,wao wanaona kuwa anafaidi,hivyo wanaongelea ngono.Hayo ndio mawazo yao,Sophia akasema wanyimwe unyumba,mwingine akasema shuka kwa shuka,sasa wanawataka wake za wana CHADEMA,hamtosheki na wake zenu???????Tuongelee mustakabali wa Taifa na sio vimada yupi kamchukua yupi na kuanza kugombania vimada.
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mwacheni Dk. Slaa, jibuni hoja


  Na Mwandishi Maalum


  TUKIWA bado tunasoma ilani za vyama vinavyogombea uongozi katika uchaguzi mkuu ujao, gazeti la serikali, Habari Leo limeendelea kuandika habari zinazohusu maisha binafsi ya mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.

  Gazeti la serikali linatutaka tuache kuangalia hoja za wagombea, ilani zao na rekodi zao za utendaji, badala yake, tuanze kuangalia nani kati ya wagombea anajua kumfinya mkewe au mmewe vizuri.

  Mgombe yupi anavaa vizuri; nani anavaa soksi zilizotoboka na kati ya wagombea waliojitokeza, yupi anayeendeshwa na mkewe.

  Kwa gazeti la serikali kuziba masikio na kuteketeza maadili ya uandishi wa habari, ni mfano mbaya kwa magazeti mengine na hatari kwa mustakabali wa taifa.


  Tukikubali kuangalia ubora wa wagombea kwa kuongozwa na kipengele cha ubora wa ndoa, tutaumizana na bila shaka siku ya mwisho, mchokozi atalazimika kushika filimbi ili awe mwamuzi, maana mchezo hatauweza. Hii ni kwa sababu wagombea wetu wana mambo mengi, tena si ya kale, bali yanayowaandama hata baada ya kukabidhiwa dhamana kubwa ya uongozi. Wapo ambao hata ukiwauliza wana wake wangapi watashindwa kukujibu kutokana na kupoteza kumbukumbu kunakotokana na wingi wao.


  Wapo watakaokujibu kwa kukuuliza, “una maana gani unaposema wake?” Wapo ambao hawajui kama wameoa au wameolewa. Wapo ambao watakuonyesha wake zao kumbe ni watoto wao.

  Wapo wanaojua kuwa walioa, lakini wamesahau ni lini na walimwoa nani? Wapo watakaokujibu kutegemea ni nani anawasikiliza wakati huo; na wapo ambao watakuambia uwasiliane na wahasibu wao, maana ndiyo wanatunza idadi yao kwa sababu ndio wanaowalipa kila mwezi.

  Wapo na tunawajua hata kwa majina ambao hawaaminiwi na wake zao kukaa karibu na mabinti zao wa kuzaa! Tunawajua wanaotunza watoto wanaodai ni wa mitaani, lakini mama zao wa mitaani wanasema “ni watoto wa hao wanaowatunza.”

  Hali hii si njema kuichanganya na mjadala mzito wa kumchagua rais wa nchi. Ndiyo maana, Dk. Slaa mwenyewe anayetafutwa katika mchezo huu mchafu, amejibu kwa kifupi kuwa hagombei
  “uaskofu wala ushehe, bali nagombea urais wa Tanzania, yenye mila na desturi zake iliyosheheni dini mbalimbali na hata wale wasiokuwa na dini.”


  Kumhukumu kwa kutumia itikadi fulani kuhusu suala la ndoa, si sahihi, licha ya kwamba suala lake linaeleweka na lina vielelezo kama alivyonukuliwa katika mahojiano na vyombo mbalimbali vikiwamo vile vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake.

  Nina uhakika kabisa, baadhi ya wagombea wa urais hawawezi kujibu maswali ya maisha binafsi aliyoulizwa Dk. Slaa: Wathubutu tuone.

  Kama masuala ya maadili binafsi na hali za ndoa za wanasiasa wetu ndiyo yatakayoamua kinyanganyiro hiki, basi tujiandae kwa makubwa.

  Hii ni kwa sababu baadhi ya wanasiasa, wanaishi maisha ya shaka kuhusu afya zao na afya za ndoa zao.


  Wengi wanaishi kwa matumaini na ni suala la muda tu kusubiri tutangaziwe misiba ya kitaifa (Mola apishe mbali!) Baadhi yao imewachukua muda kuamua kama wagombee au waache kwa sababu ya migogoro mikubwa inayozikumba afya zao.

  Nina maana ya kuugua kunakohusiana na mgogoro mkubwa wa maadili binafsi ya wagombea wetu. Tunawajua waliozimia waliposikia baadhi ya watu wamekufa kwa ukimwi!

  Tunawajua hata wale waliolazimika kutumia nguvu ya dola ili kuzima zahama za kimaadili zilizokuwa zinaelekea kulipuka. Tunawajua ambao hata leo hawana amani ndani ya nyumba zao kwa sababu tu, wake zao wanajua wanachokifanya.

  Wanajua kuwa wanakula sahani moja na mabinti wadogo walio katika nafasi nyeti na hata wake
  zao wamediriki kushinikiza mabinti hao kamwe wasionekane wanachaguliwa au kuteuliwa kuwa wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa.

  Nafuu ya Dk. Slaa anayedaiwa kuchukua mke wa mtu. Je, hao wanaojulikana mbona hawasemwi?

  Hakuna linalofichika chini ya mbingu, na hata hatua chafu ya kuwatoa roho baadhi ya wasichana ili kuficha yasiyofichwa yanajulikana na baadhi ya wasichana wameonana na wanasheria kuandikisha maelezo ili likitokea la kutokea wauaji hao wajulikane.

  Yarabi tupe salama! Baadhi ya mambo yanayoendelea ndani ya serikali ni ya kukalia matanga. Wapo wanaochekelea kwa kufikiri kwa kuwa wapenzi (nyumba ndogo) wao wametangulia mbele ya haki, basi siri yao itabaki ufichoni. Wanajidanganya! Wamwulize Monica Lewinski na Paula Jones kule Marekani.

  Miaka ilipita, lakini siku ya nyani kufa ikafika na miti yote ikateleza ikiwamo mibuyu! Viapo vilikiukwa, amri za kutosema zilibatilishwa, viapo vya migongano ya maslahi vilivunjwa, viapo vya maslahi ya uteja viliondolewa ili kuujua ukweli kwa maslahi ya taifa.

  Naam, wote tunajua kwa hakika kuwa kinachotafutwa hapa ni kupunguza nguvu ya Dk. Slaa kwa nguvu yoyote ile. Kinachowaogofya si kingine bali ni rekodi yake ya kutanguliza si mke wake, mtoto wake, chama chake, rafiki zake wala ndugu zake, bali taifa lake.

  Inawashangaza wengi kusikia Dk. Slaa amediriki kumpigia kampeini mgombea wa NCCR-Mageuzi mahali fulani kudhihirisha hilo. Natamani kumsikia Kikwete akimnadi mgombea asiye wa CCM ikiwa anafika mahali pa kuhoji uwezo wa mgombea wa CCM. Nyerere alifanya hivyo na tungali tunakumbuka.

  Umaskini wa Watanzania haukutokana na ndoa ya Dk. Slaa. Umetokana na ufisadi wa baadhi ya na viongozi CCM na serikali yake. Ufisadi unakihusu chama chao chote, familia zao, nyumba ndogo pamoja na zile kubwa.

  Ninawashauri wana CCM wenzangu – mwili wangu uko CCM, lakini roho haiko huko, wajikite katika kujibu hoja za Dk. Slaa, na kuachana na mambo ya ndani ya suruali na sketi za watu.

  Maana tulio na taarifa za kina kuhusu maisha binafsi ya vigogo wa CCM tutalazimika kuingia hadharani endapo gazeti la serikali na yale yanayomilikiwa na watuhumiwa wakuu wa ufisadi, yataendelea kutuchelewesha kwa kujadili “masuala” binafsi, badala ya maendeleo.

  Nasema hivi kwa sababu wahuni walewale ndio wanaofanya ujinga huuhuu ndani ya chama wakati wa michakato yetu ya ndani na kusababisha mipasuko isiyoisha. Sasa wamejipatia ajira kwa kushinda mitaani wakiandika habari za kuchafuana na kuwachafua wanaowaita “maadui” zao kisiasa. Huu ni wakati wa kujibu hoja si vinginevyo.

  SOURCE; MWANA HALISI WIKI HII
  =========

  My take: This is a gathering storm if it is truly said by a CCM member.
   
 5. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Hii mada ina mambo mawili mazito, moja ni hili la kutaka kutuyumbisha kwenye hoja ya msingi kuhusu uchaguzi hususani ujuzi na utashi wa Mh Slaa, ya pili ni huo ufichuo (revelation) ya kwamba wapo mabinti wanatesa wananyanyaswa na wanalazimishwa nahisi kutoa mimba au hivi kwa sababu ya tamaa ya mwili ya wanasiasa (na hapa mwandishi anaelekeza kwa CCM) na kumbe wao wengine wanalelewa kama vile watoto wa mitaani kumbe ni vimada. Sasa hili nadhani ni baya kuliko yote. UTAWAFANYAJE WATANZANIA WENZAKO WATUMWA KARNE HII! MAKAMBA NA WENZIO HAMUMWOGOPI HATA MUNGU!
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka nikiwa secondary tulijifunza moja uzuri wa ushindani wa kibiashara ni kuimarika kwa bidhaa.
  Ukosoaji na kuweka bidhaa yako ktk hali ya kununulika
  Sasa leo tunapata habari za ndani sana katika hivi vita vya wana siasa.
   
 7. S

  Sylver Senior Member

  #7
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is not what we need, hayo maisha ya kibinafsi .

  CCM na Chadema wache hii ,ingawa wanasiasa huweza fanya vyovyte kushinda ila wananchi inabidi tuwaeleze hatuhitaji kujua haya .

  Tunajua wengi wana matatizo so no one to fool mwananchi ktk hili na hatutaki sikia .
   
 8. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapana Sylver ! Tunahitaji na tunastahili kujua maisha binafsi ya viongozi wetu. Hatuhitaji kuwa vipofu wa kutoona madudu yao. Viongozi wenye udhaifu wa hali ya kutisha namna hiyo..hatuwahitaji. Viongozi wanaolazimika kuua raia zao ili kuficha madudu yao..hatuwahitaji. Lazima tuwajue ili tuamue vizuri namna ya kuwakubali au kuwakataa.

  Lakini kwa upande wa pili ni kwamba, uongozi dhalimu hukataliwa na Mungu kwanza na kisha raia nao hufuata. Mimi sasa hivi nimeanza kufanya maombi ya kuombea nchi yetu na uchaguzi ujao. Tunahitaji haki yetu, ya kuchagua na kutawaliwa na kiongozi bora. Mungu hutoa viongozi bora na kuwaondoa viongozi wabovu. Hatuwezi kupata viongozi bora kwa kufumbana macho ili tusijue mambo ya watu wanaotutawala. Kuna hatari ya kutawaliwa na watu wanaoabudu shetani na kutoa sadaka za watu..je wewe unataka hilo? Mimi sitaki kabisa. Naomba wenye taarifa zaidi za udhaifu wa viongozi wetu watupatie ili tuwajue na hatimaye tushirikiane na Mungu kuwakataa kuongoza nchiyetu.
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Hapo kwenye blue ndipo panaleta shida, maana ni suala la kitaifa. Mengine naona ni mambo binafsi.
   
 10. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  spill the beans
   
Loading...