Mw/kiti BAVICHA wilaya ya Arusha apigwa na Green guard

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Mw/kiti wa BAVICHA wilaya ya Arusha mjini amepigwa vibaya sana na kikundi cha green guard ambacho kikochini ya CCM..tukio hilo limetokea mchana huu akiwa anaelekea kwenye kampeni huko Engototo ambapo kuna kampeni zinaendelea kwaajili ya kumchagua diwani wa kata hiyo uchaguzi utakao fanyika tarehe 2-10-2011, Edero Edero ni mratibu wa kampeni hizo kwa upande wa chadema, Odero odero pamoja na mgombea wa kata hiyo Bw. Maganga walitekwa na vijana hao waliokuwa na rav 4 nyeupe kwa bahati nzuri Maganga alifanikiwa kuwa toroka na kwenda kutoa taarifa polisi ndipo polisi walipo anza kufanya msako wa kumtafuta Odero pamoja na watekaji walifanikiwa kumkuta Odero pori moja huko Engototo akiwa hoi huku watekaji hao wakiwa wamechukua makabulasha yote...
 
siasa za Monduli ni za Kishenzi saana mi nazifahamu, hata wanaofanya hivo sio kwamba hawajulikani, wanajulikana na wala hawatafanywa lolote hata kama wakikamatwa, subiri uuone.
 
Lowasa yupo kazini. Lakini kwa sisi wanamapinduzi ni dalili za mwisho kabla wakoloni hawajasalimu amri. Siku hii iko karibu sana kuwadia. Wakoloni ccm tutawapoteza.
 
Pole zake. Sishabikii sana fujo ila nadhani umefika wakati wa kujihami pia. Green guard ni viumbe gani hao. I swear kama wakiendelea ntakuwa nawawinda na manati. Hawa vijana wapuuz na wanaowa2ma pia.
 
Hv hawa Magamba watawanyanyasa watz hadi lini? Yani natamani magamba wote wangekufa hata leo. Siku zao za mwishi ziko jirani, kwani kila jambo lina wakati wake.Let us wait their days are countable............
 
Ameweza kuwatambua kuwa ni green guard akashindwa kupata namba za Rav4, hata aliyefanikiwa kutoroka nae hakufanya usmart wa angalau kusoma namba,, anyway wajitahidi kuelezea wasifu wa hao watekaji na gari ilivo inaweza warahisishia polisi kukamata
 
Hawa magamba walaaniwe kabisa, wanajua wananchi washawachoka wanawalazimisha kuwatawala.
 
Ameweza kuwatambua kuwa ni green guard akashindwa kupata namba za Rav4, hata aliyefanikiwa kutoroka nae hakufanya usmart wa angalau kusoma namba,, anyway wajitahidi kuelezea wasifu wa hao watekaji na gari ilivo inaweza warahisishia polisi kukamata
Mw/kiti Bavicha yuko tabani ameumezwa vibaya sana alietoa maelezo ni Mgombea ambae ni Bw. maganga....
 
Kwa hali hii kama tutafka mwaka 2015 salama basi kampeni na uchaguzi huo sipati picha angekuwepo sheikh yahaya angetabiri.....
 
Lengo la Green Guard mbona haieleweki? Au walikuwa wanapiga tu bila sababu? Kweli ccm wamekosa hoja!
 
Lengo la Green Guard mbona haieleweki? Au walikuwa wanapiga tu bila sababu? Kweli ccm wamekosa hoja!
CCM kimsingi wameishiwa mbinu zamajukwaani wamebaki na mbinu chafu za nje ulingo mbaya zaidi ni chafu...
 
Hii ni hatari, kama hali hii ya kupigana itaendelea bila wahusika kuchukuliwa hatua mahsusi, watu wataanza visasi jambo ambalo litakuwa gumu kulizuia.
 
Nampa pole sana ndugu, kiongozi, rafiki, kamanda wangu Mh. Diwani Efatha Nanyaro, m/kiti wa vijana mkoa wa Arusha! Nimesikitishwa sana na taarifa hii. Ni uhuni na uharamia uliofanyika!
Kimsingi mapambano yanaendelea. Tunamuombea apone haraka na sasa tutajiongezea ulinzi na kushambulia kwa kupanda na kushuka hadi kieleweke.
Wito wangu kwa wananchi wa Engutoto ni kuwadhibu hao magamba kwa kuichagua cdm ili liwe funzo kwa wengine wote!?
 
Mkuu aliyeshambuliwa ni diwani Ephata Nanyaro ama ni odero odero?
 
Back
Top Bottom