Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, amesema wimbi la vijana wa CCM kukikimbia na kujiunga na Chadema ni dalili mbaya na kukitaka chama hicho kuwavua magamba wanachama wao wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya ufisadi badala ya kusubiri wajivue wenyewe.
Dk. Bana, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam pembeni mwa mkutano wa mtengamano wa kisiasa wa Afrika Mashariki.
Alisema kuna watu wengi wanaotaka kukihama CCM na kujiunga na Chadema hivi sasa, lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na ugumu wa mioyo yao kisiasa.
CCM isisubiri wanachama wao wenyewe kujivua gamba na kisha vigogo kuanza kusema kwamba watu wa aina hiyo walikuwa hawawahitaji badala yake chama kiwavue kabla, alisema Dk. Bana.
Alifafanua kuwa wimbi hilo la vijana pamoja na watu wengine kutamani kuhama CCM na kujiunga na Chadema linatokana na chama hicho cha upinzani kwa sasa kuonekana kuwa na mvuto.
Aliongeza kuwa ni vigumu kwa baadhi ya wanachama wa CCM kukubali ukweli huo kwamba Chadema kina mvuto, lakini alisema watu wenye akili ndani ya CCM wanaijua dhana hiyo.
Watu wenye akili ndani ya CCM wanajua Chadema kina mvuto na hili wimbi la vijana na watu wengine kukihama CCM siyo dalili nzuri hususani utakapofika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alisema.
Alisema Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ulidhihirisha kwamba Chadema kilipata mvuto mkubwa kwa wananchi baada ya kuibuka na ushindi katika majimbo mbalimbali na kuongeza idadi ya wabunge wake.
Mwaka 1995 hadi mwaka 2000 wanachama wa upinzani walikuwa wanahama katika vyama vyao na kujiunga na CCM, lakini hivi sasa upepo umebadilika ambapo sasa wanahama kutoka CCM na kwenda Chadema, hii ni dalili kwamba wanakiona kama chama mbadala, alisema.
Source:Nipashe