Mvuto na upepo wa Magufuli umepotea au mitandao tu?

Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
454
1,264
Nakumbuka kipindi anaingia madarakani kabla hajateua baraza la mawaziri mkuu alikuwa anakubalika sana hasa zile safari za kushitukiza kama Muhimbili, TRA na Bandari. Matumaini mapya kwa huyu Jamaa.

Magufuli wa sasa anapingwa kila siku. Kwenye watu kumi, saba wanampinga Magufuli. Wadau tatizo nini, ugumu wa maisha, kauli zake au ubabe?

Binafsi nilimkubali sana mkuu huyu kipindi anaanza but leo sioni matumaini tena na ni mwaka sasa amemaliza lakini akisimama jukwaani hana anachoongea zaidi ya kuponda mtangulizi wake na kutoa lawama kwa kila mtu.

Sijaona vision au strategic planning yeyote. Leo watumishi wa umma wanalia, wafanyabiashara wanalia, wakulima wanalia, kila MTU magufuli ..magufuli..kila MTU.

Ukiona unapingwa sana na watu ujue unatatzo. Mzee mwaka wa kwanza haukuwa mzuri kwako. Tengeneza mazngira rafiki kwa private sector watu waajiriwe.
 
Kweli mzee.mbn anapondwa sana
Mvuto gani unaosema wakati Rais Magufuli alikataliwa na wapiga kura asilimia 42.

Unashangaa kwa Rais Magufuli kupondwa lakini kwa fikra zao nadhani huwezi kushangaa kwa mitume kupondwa mpaka wengine kuuwawa pamoja na kuonyesha miujiza mbali mbali.

Eti katika watu 10 unapata 7 wanaomponda. Huu utafiti wako uliufanyia kwenye keyboard yako?

Magufuli ni mmoja wa viongozi ambao wanaitwa kwa kiingereza statesman.

Moja ya sifa ya Statesman sio kuangalia uchaguzi ujao bali kuangalia kizazi kijacho.

Moja ya uwezo wa Rais Magufuli ni uthubutu katika maamuzi bila kujali kama yanafurahisha wengi au la.
 
Ikifika 2020 sijui atafanyaje walahi....labda aibe na wabadilishe number zote kwenye karatasi za kura! Sijui atapata za boda boda tuuuuu sio zingine
 
Pinga pinga wanatoka mapovu balaa.
Kikwete alikuwa hatumbui mkasema analipa fadhila.
Kikwete alikuwa anasafili sana mkasema apunguze safali na abane matumizi.
Magufuli kafanya oposite , mnataka afanye kama alivyofanya Kikwete.
Save it Mbs
 
Nakumbuka kipindi anaingia madarakani kabla hajateua baraza la mawaziri mkuu alikuwa anakubalika sana hasa zile safari za kushitukiza kama Muhimbili, TRA na Bandari. Matumaini mapya kwa huyu Jamaa.

Magufuli wa sasa anapingwa kila siku. Kwenye watu kumi, saba wanampinga Magufuli. Wadau tatizo nini, ugumu wa maisha, kauli zake au ubabe?

Binafsi nilimkubali sana mkuu huyu kipindi anaanza but leo sioni matumaini tena na ni mwaka sasa amemaliza lakini akisimama jukwaani hana anachoongea zaidi ya kuponda mtangulizi wake na kutoa lawama kwa kila mtu.

Sijaona vision au strategic planning yeyote.

Pesa ya deal au makongamano na safari zisizo na tija ikitoweka mifukoni lazima utasikia kila aina ya kelele. Huyu atalia njaa, huyu atasema Mkulu mbabe, huyu utasikia ameota mkulu atapatwa na umauti, mwingine utasikia umaarufubwa mkulu umepotea, mwingine utasikia hotuba zake hazina jipya. Hizi kelele zote chorus yake ni moja tu - watu wanalazimika kuishi kwa kipato chao halali (within valid means).

Kunachotakiwa sio hotuba nzuri (maneno matamu ya ahadi za kusadikika), wala kuonekana kwenye TV. Kinachotakiwa ni matokeo.

Katika kupata matokeo hayo, process inayotumika ndio inawaumiza wengi hasa waliozoea "vya kunyonga" na unyonyaji.

Uthubutu alio nao Magufuli hata ukikataa leo, kimoyo moyo utakubali kuwa ni viongozi wachache sana Africa wana dhamira hiyo. Wachache. Na aina hii ya kiongozi mara nyingi huwa hapendwi. Anaonekana katili au asiye na huruma au hana plan kama unavyosema. Pamoja na mapungufu ya kibinadam aliyonayo, ambayo hata wewe unayo maana si malaika, huyu ndiye kiongozi anayefaa hasa kwa kipindi hiki ambacho nchi ilikuwa imefikia hatua watu wanaweka serikali mfukoni. Unakuwa unasikia majina ya watu hata kumi hawafiki ndio wanaendesha nchi kibiashara jinsi wanavyotaka. Hii hapana. Sasa, kwa asiyependa, ajue ana miaka mingine 9 ya kuwa na huzuni "ya kujitakia" kutokana na mtazamo wake hasi au wenye ubinafsi.
 
Back
Top Bottom