Mvutano waibuka Singida madiwani wa CHADEMA watolewa meza kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvutano waibuka Singida madiwani wa CHADEMA watolewa meza kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 27, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  [​IMG]
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singidan Selestine Yunde akifungua kikao cha baraza la madiwani. Kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Illuminata Mwenda na kushoto ni Makamu Mwenyekiti Higa Mnyawi.

  Na Nathaniel Limu
  Bundi bado anaendelea kuunguruma ndani ya vikao vya baraza la madiwani (full council) katika halmashauri ya wilaya ya Singida, baada ya kikao cha kawaida cha baraza kusimama kwa takribani saa moja, kuruhusu madiwani wawili wa CHADEMA kuondolewa meza kuu.
  Madiwani walio ondolewa kwenye meza kuu ni Christowaja Mtinda na Christina Mughwai ambao wote hao ni wabunge wa viti maalum.
  Madiwani hao walikubana na dhahama hiyo baada ya Christowaja kuuliza swali juu ya mapato na matumizi.
  Swali hilo lilipelekea madiwani wa CCM wapato 63 (madiwani wa CHADEMA wapo sita tu) kupinga swali hilo kuulizwa na kiongozi ambaye amekaa meza kuu, wakidai kuwa itifaki hairuhusu mjumbe kukaa meza kuu na kuuliza maswali, badala yake anatakiwa kujibu maswali.
  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Illuminata Mwenda, aliingilia kati na kukieleza kikao hicho kuwa madiwani hao wawili wa CHADEMA, hawakujipeleka meza kuu isipokuwa walitengewa viti kwenye meza hiyo na uongozi wa halmashauri.
  hata hivyo, hoja hiyo ilipigwa vikali na madiwani wa CCM huku wakipiga piga kwa nguvu meza zao na kupaza sauti kuwa “watoke huko meza kuu waje waungane na sisi huku chini”.
  Baada ya hapo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Selestian Yunde aliagiza madiwani hao watengewe meza sawia na wenzao wa kata na wa viti maalum ambao sio wabunge.
  Bundi huyo alianza kuunguruma mapema tu mara mwenyekiti Yunde alipomaliza hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho na kumruhusu msemaji wa kwanza, ambaye alikuwa ni diwani wa kata Mujughuda Frank Nyekele kuuliza swali.
  Nyekele aliomba kuelezwa ni hatua gani zizochukuliwa dhidi ya diwani Christowaja kutokana na kitendo chake cha kutamka kuwa madiwani wa CCM, shida yao ni kulipwa posho tu na hawako kwa maslahi ya wananchi, swali ambalo liliungwa mkono na madiwani wa CCM kwa kupiga piga meza kwa nguvu kama kawaida yao.
  Christowaja alijibu mapigo kuwa hatafuta wala kuomba radhi kwa matamshi yake hayo, kwa madai kwamba, madiwani wa CCM wametafsiri vibaya matamshi yake hayo.
  Kama hiyo haitoshi, wakati Makamu Mwenyekiti Higa Mnyawi akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu, alitamka kuwa yupo diwani mmoja anayejifanya yeye ni ‘diwani sanaa’, kwa malidai kuwa anaikwamisha halmashauri kukusanya mapato yake ya ndani.
  Alidai kuwa ‘diwani sanaa’ huyo, amewakataza wananchi wa jimbo lake kulipa ushuru mbalimbali ukiwemo wa mazao.
  Baada ya Mnyawi ambaye ni diwani wa kata ya Ikhanoda kumaliza kutoa taarifa yake, Christowaja alisimama na kuomba ufafanuzi wa maana halisi ya ‘diwani sanaa’ ili hali yeye anavyofahamu, ni kwamba madiwani wote wako sawa.
  Ghafla mwenyekiti Yunde, aliingilia kati huku akionyesha wazi kukerwa na malumbano hayo na kusema “sasa naona mnataka kuanza kuniletea matatizo yenu, hapa hakuna diwani sanaa, madiwani wote tupo sawa, sitaki kusikia tena diwani yo yote anatamka ‘diwani sanaa”.
  Katika kikao cha baraza la madiwani cha bajeti kilichopita hivi karibuni, kulitokea songombingo ya aina yake kati ya madiwani wa CCM na CHADEMA na kusababisha bajeti kupitishwa bila ya kusomwa kifungu kwa kifungu.
  Kitendo cha kuwatoa meza kuu madiwani wa CHADEMA ambao ni wabunge, kimewagawa madiwani wa CCM katika makundi mawili, moja likidai kutolewa kwa wabunge hao ni sahihi, huku wengine wakidai kuwa wabunge hao wameonewa.
  Wamedai kuwa miaka yote wabunge wa CCM wamekuwa wakikaa meza kuu na kuuliza maswali kama alivyofanya Christowaja.


  [​IMG]
  Diwani Christowaja akiuliza swali mbele ya baraza la madiwani.
  [​IMG]
  Diwani Christowaja Mtinda (wa pili kutoka kulia) na Christina Muhwai (wa kwanza kulia)wakitolewa meza kuu.
  [​IMG]
  Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida waliohudhuria kikao cha baraza cha la madiwani.
   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Usipotoshe watu Madiwani wa Chadema walitoka meza kuu ili waweze kuuliza maswali kwa vile hawawezi kuuliza swali wakiwa meza kuu Mkurugenzi aliaanza kuwabembeleza kurudi lakini wakakataa.
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kuna tofauti gani kuuliza huku ukiwa umekaa mbele au hata nyuma kwani haitobadilisha maana ya swali cha msingi ni wahusika kuwafafanulia madiwani maswali yao. umeshindwa pia kueleza kuwa madiwani wa ccm wanaowatetea wale wa chadema wanasema kwamba madiwani wa ccm walikuwa wakiiuliza maswali huku wakiwa wamekaa mbele iweje chadema wasiulize huku wakiwa wamekaa mbele huoni kuwa kama hapo kuna uonevu au double standard ??
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  By the way namuunga mkono diwani christowaja kuwa madiwani wa CCM wapo kwa ajili moja nayo ni kula posho za vikao tu na siyo kuwalikilisha maslahi ya wananchi na ushahidi mkubwa ni kitendo chao cha kupitisha budget bila hata kuisoma na kujua kuna nini ndani hiyo ni kinyume cha kazi yao ambayo ni kuakikisha kila kinachopitishwa na kikao kweli kina reflect maslahi ya wananchi wao kwa kitendo chao cha kupitisha bila kusoma kilichomo ndani kinadhiirisha kuwa wanafilkiria zaidi kwa kutumia matumbo yao badala ya ubongo wao ambao wamekataa kuutumia.
   
 5. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  duuh hii vita ya Cdm na ccm ina tija kweli? Mi naona ccm waache kulumbana wao wafanye kazi kwani wao ni chama tawala malumbano yao yawe kwa vitendo, CDM ni wapinzani na wanachofanya ni kuonesha udhaifu kwa ccm na hiyo ndo role ya upinzani. CCM since ni watawala ni ka mti wenye matunda sasa unapopigwa mawe hautakiwi kujibu kwa kuwaponda wanaorusha mawe kwa matunda, hutawakomoa sana sana utakuwa umewapa matunda ya bureee, na ccm ndo wanachofanya hawajui ka wanavyohangaika nao ndo wanawapa umaarufu wa bureee. Anyway niwaache sababu waswahili walisema sikio la kufa....... Ndo hao cccm
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wabunge 10 CCM= na mbunge 1 wa CDM??
  Na bado CCM kamasi zinawatoka.
   
 7. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru sana mwanajamvi kutujuza hayo kwani tungejuaje? Moto wa mafisadi kutafuna pesa za wananchi zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo unaelekea kuzima. Kinachohitajika ni hao wenzetu (madiwani na wabunge hasa wa upinzanni) kuendelea kututetea kwa nguve zote!!! Kwani madiwani na wabunge wa CCM = ufisadi na ufisadi = na wabunge na madiwani wa ccm!!
   
 8. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,915
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Style ya madiwani wa CDM inatia mashaka, kila sehemu ni kuanzisha shari tu, LINI watakaa chini na kuanza kuwafikilia wananchi waliowapa kura????
   
 9. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  naona umezungumzia vitu viwili tofauti.kuna sehemu unazungumzia wabunge sehemu nyingine madiwani.kipi ni kipi?au umekosea katika kuandika?kuna wabunge waliokuwepo?
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,848
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280

  .duuu hawa ndio aina ya watanzania...kwahiyo wewe unaona taratibu zikiukwe..tu..bajeti zipitishwe bila kusomwa ...kweli....?
   
 11. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,338
  Trophy Points: 280
  Hawaanzishi shari mmezoea vya kunyonga lazima akili ziwakae sawa sasa hivi badala ya kufikiria kwa akili mnafikiria kwa ******
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kazi ipo huko Tanganyika. mafahali wawili
   
 13. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tofauti kati ya madiwani wa CDM na CCM ni kuwa:
  1.Madiwani wa CDM wamefundishwa majukumu wakati wale wa CCM mwalimu wao yupo ICU.
  2.Madiwani wa CDM wametumwa na wananchi pamoja na CDM lakini wale wa CCM wametumwa na matumbo yao na CCM yao.

  Hizo tofauti kubwa ndizo zinazowafanya mara zote madiwani wa CDM na CCM wawe katika malumbano.
   
 14. m

  mndeme JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kuna madudu mengi sana kwenye halmashauri nyingi nchini na hilo liliendekezwa na kuwa na madiwani wote kutoka chama cha magamba, linapokuja suala lakuhoji wanasema CDM wakorofi, sio wazalendo, wanapinga kila kitu yaani ni maneno chungu zima.

  Tunahitaji macho ya ziada kwnye matumizi ya fedha za wananchi
   
 15. 1

  19don JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  soma maelezo vzr hoja ni kuuliza swali wakiwa wamekaa meza kuu sio kuanzisha fujo kama ulivyo elewa, walihoji kuhusu mapato na matumizi , ukiulizia vitu hivyo ndio unaanzisha fujo?
   
 16. K

  Kiguu na njia Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sasa madiwani wa CCM Singida mnadumisha umaskini kwa kuogopa hoja za CDM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  hali hii itazidi kututia umaskini zaidi. fact in issue ilikuwa ni lile swali alilouliza no matter kaulizia toka upande gani wa ukumbi (meza kuu)ama kwingineko, ajabu sasa hata baada ya kushuka still swali hilo halikujadiliwa/kujibiwa. inaonekana madiwani hata wanachama wa kawaida mitaani wa ccm hawako tayari kujadili issue tangible kwa maslahi ya taifa/wananchi maadamu tu itakuwa imewasilishwa/kuulizwa na diwani/mtu wa chadema
   
 18. I

  Isekuu Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiri wanyaturu sasa tunaamka na bado mambo yataenda vzuri 2 tumechoka mfumo huu wa kiutawala. Singida cdm itachanua tu.
   
 19. I

  Isekuu Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We zoba nini, cdm wanauliza vtu vya maana sio kama ccm wanaulizia posho tu. Sehem yeyote wakiwepo cdm ccm wanakosa ganji ndo mana wanakuwa wakali.
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sio hivyo walifukuzwa meza kuu ! na baada ya kitendo hicho walitoa na machozi kuwa wameonewa
   
Loading...