Mvutano waibuka kati ya Kikwete na Magufuli juu ya ukatibu wa bunge, asita kuachia madaraka

JK aondoke tu hatumtaki. Katuharibia chama yeye na familia yake. Huyu naye wa nini? Atimuke tu na uislamu wake. Ukiangalia sana kwenye chaguo lake la Mama Chatanda au Ulega kuna mchepuko au uislamu tu. Chunguzeni sana mtaona.

Hata kama ulikuwa na hoja ya kutomkubali J.Kikwete ulikuwa umeeleweka na ungestahili kuishia hapo hapo.Hayo mengine ya uswahili na uislamu hauna nafasi wala hauungwi mkono na ukristo na niwaombe wote wenye kuitakia nchi mema na amani mpuuze mchango/michango yote yenye mielekeo ya hivyo.
 
Kutamani watu waliwatamania yawafike Mabaya kuliko hayo ya kupigana! Kumbuka CCM kadri itikisikavyo ndivyo iimarikavyo
CCM inayopoteza majimbo mengi kila uchaguzi kutokana na minyukano ya ndani inaimarika??! Una uhakika chama hakijapasuka? Una uhakika Magufuli kama 'hatabadikika' hatakipasua Chama? Unafahamu kuwa Kolimba alitabiri kuwa Chama Kimeoza? Huuoni Uozo? Ziko wapi Assets za Chama? Magufuli sio swahiba wa wafanyabiashara, yeye ni kazi tu na anataka kodi, Chama kimeshikwa na wenye fedha wezi, majangili, waporaji wa rasilmali na wasiotaka kulipa kodi halali. Huoni mpasuko hapo? Acha utani Wewe. Chama kipo kwenye bonde la uvuli wa mauti
 
Jk kama kafanya hayo amekosea sana lazima apingwe kwa nguvu zote.
 
Ndugu zangu wana JF tayari kuna msuguano mkubwa umeibuka ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) baina ya katibu mkuu Kinana na mwenyekiti JK chanzo kikitajwa kuwa ni nafasi ya ukatibu mkuu wa bunge wa chama cha mapinduzi.

Hii ni baada ya kuibuka mvutano mkubwa mwingine baina ya Mh RAIS JPM NA JK kwakuwa kila mmoja kuwa na chaguo lake.Huku JPM akitaka Mh Rweikiza ndio awe katibu na JK akitaka awe kati ya mama Chatanda ama Mh Ulega

Kutokana na mvutano huo uliojitokeza Katika kikao hicho kilichofanyika jana Mh JK kasita kutangaza siku ya Mkutano Mkuu Maalum wa kuachia madaraka ya Uenyekiti

Kutoka kwa vyanzo vya ndani ya CC jana walikua na ajenda ya tarehe ya mkutano mkuu ila kabla ya mkutano kuanza ndio kilifanyika kikao kidogo likichohudhuriwa na watu 4 ambao ni JK,MAGU,MAMA SAMIA NA KINANA.

Na ndipo baada baada ya kikao hicho JK alirudi kuondoa ajenda hiyo kwa hoja kuwa ilikuwa haijaandaliwa vizuri na kuahirisha kikao cha CC.

Sasa kikao cha Baraza la wazee kitaitwa katika siku chache zijazo ili kumlazimisha JK kuacha.

Hivi Unatambua Kwamba ni Kosa Chini ya Sheria ya Mtandao Kutoa Taarifa za Uongo Mtandaoni? You have been warned.
 
1.jpg


Hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mchakato unaoendelea wa kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli uenyekiti wa chama hicho, kukumbwa na sintofahamu.

Taarifa kutoka ndani kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC), kilichofanyika juzi Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, zimethibitisha kutokea mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho.

Hali hiyo imekuja baada ya kutokea kwa mvutano juu ya tarehe rasmi ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu uliopangwa Juni mwaka huu, ambao pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete atakabidhi kijiti kwa Rais Magufuli.
Chanzo cha kuaminika ndani ya kikao hicho kilidokeza kuwa, kabla kilifanyika kikao kidogo kilichokuwa na wajumbe wanne ambao pamoja na mambo mengine walijadili ajenda muhimu ikiwamo ya kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano huo.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikao hicho kidogo kilishirikisha viongozi wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Habari hizo zinaeleza kuwa, katika kikao hicho kidogo viongozi hao walikubaliana wakatangaze tarehe rasmi, na Rais Magufuli alikubali kukabidhiwa uenyekiti wa chama kama ulivyo utaratibu wa CCM lakini baada ya kikao cha Kamati Kuu kuanza, Kikwete alikataa kuruhusu hoja hiyo ijadiliwe, hatua iliyozua mfarakano.


“Baada ya kumalizika kwa kikao kile viongozi hao wanne waliingia ndani ya kikao cha CC ambacho kilikuwa na ajenda kadhaa ikiwemo ya mkutano mkuu maalumu ambapo mwenyekiti alirusha na kutaka hoja ya tarehe isijadiliwe,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ilipofika ajenda ya tatu ambayo iliwasilishwa na Katibu Mkuu, Kinana kuhusu kutangazwa kwa tarehe ya mkutano mkuu maalumu, Kikwete aligoma isijadiliwe na badala yake aliahirisha kikao na kutoka nje.


Chanzo hicho kilisema, uamuzi wa Mwenyekiti Kikwete wa kuahirisha kikao ulijikita katika suala la gharama za mkutano ambazo zinakadiriwa kuwa ni zaidi ya Sh bilioni mbili, hivyo aliwataka wajumbe waahirishe kikao ili kutoa fursa ya kutafuta fedha.

Taarifa hizo zilieleza kuwa, kutokana na hali hiyo yaliibuka makundi mawili, moja linalomuunga mkono Kikwete na jingine linalopingana na hoja hiyo, likidai kuwa fedha si tatizo kwa chama hicho kwa kwani kina miradi, ruzuku na marafiki wengi.

“Wanaompinga mwenyekiti walishangazwa na hoja hiyo wakisema kuwa, suala la fedha ni la watendaji wa chama na si la mwenyekiti, kitendo ambacho wamekitafsiri kwamba mwenyekiti hana dhamira ya dhati ya kukabidhi chama kwa sasa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kutoa taarifa kuwa, baada ya Kikwete kugoma kujadili tarehe alisimama mjumbe Jenista Mhagama, ambaye alipinga uamuzi huo, huku akisema suala hilo ni lazima lijadiliwe kwa kina na tarehe ya mkutano mkuu itangazwe.

“Kauli ya mwenyekiti inaonekana iliwaudhi baadhi ya wajumbe, lakini Jenista alizungumza vizuri sana na kumhoji mwenyekiti inakuaje hataki kusema lini utafanyika mkutano mkuu maalumu ili akabidhi chama.

“Maana suala la makabidhiano ni la utamaduni wa ndani ya CCM, Jenista alisema aliyekaa muda mrefu alikuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pekee lakini na yeye alikabidhi kwa mzee Mwinyi (Ali Hassan) na pia ilipofika wakati kama huu mzee Mwinyi naye alikabidhi kwa mzee Mkapa.

“Si hilo tu hata mzee Mkapa naye alikabidhi chama kwake (Jakaya Kikwete), sasa inakuwaje yeye leo hataki kufuata utaratibu huo ambao ni wa kawaida ndani ya chama?,” kilihoji chanzo hicho.

Chanzo kingine cha habari kilisema kuwa baada ya mwenyekiti huyo wa CCM taifa kuahirisha kikao hicho juzi, aliondoka na kurejea jijini Dar es Salaam kwa gari tofauti na ratiba iliyokuwa imepangwa.


“Ratiba ya chama ilikuwa baada ya kikao cha jana (juzi) mwenyekiti angelala Dodoma na badala yake alipoahirisha kikao kwa utata alipanda kwenye gari na kuondoa hali ya kuwa alitakiwa kurejea Dar leo (jana).

“Baada ya kikao hicho alitoka mzee Kinana akiwa amekasirika sana, tena huku akiwa amekunja sura, unajua siku zote mzee Kinana anaamini kwamba kile kilichokuwa kinapiganiwa na chama hivi sasa ndicho kinachotekelezwa na Rais Magufuli tena kwa vitendo tofauti na huko nyuma,” kilisema chanzo chetu.

Baraza la Wazee kukutana.

Taarifa nyingine zinaarifu kwamba, kutokana na hali hiyo Baraza la Wazee la CCM linaloundwa na viongozi wastaafu, linatarajiwa kukutana kati ya leo na kesho kwa lengo la kujadili hali hiyo ili kuondoa mtanziko huo uliojitokeza.

“Ninachotaka kukuambia katika kipindi cha siku mbili baraza la ushauri la wazee litakutana na kujadili hali hii na baada ya hapo watakwenda kwa mwenyekiti kumshauri juu ya uamuzi wake na autafakari kwa kina.

“Tunajua tunakwenda vizuri katika hili na hakuna kitakachoharibika na wazee wetu watamshauri vema mwenyekiti ili kupata mwafaka wa kudumu na mkutano mkuu utafanyika mwezi uliopangwa,” chanzo hicho kilisema.

Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM, linaongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (Mwenyekiti), Pius Msekwa (Katibu) na wajumbe ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu (Bara), John Malecela.

Chanzo: Mpekuzi
 
Andishi lililojaa unafiki na majukungu. kwa mujibu wa katiba ya chama JK anatakiwa kukabidhi uenyekiti kwa JPM oktoba mwakani. Sasa hili ulilolileta mtoa bandiko kutoka huko mpekuzi huru, haliwezi kuwa bandiko sahihi. Kilichosababisha kuahirishwa kwa hoja hiyo kunatokana na theruthi tatu ya wajumbe kutaka JK aendelee mpaka oktoba mwakani huku wachache wakipinga hilo. Pia jingine lililoleta mgogoro na kusababisha kikao kuahirishwa ni kutokana na mheshimiwa Rais Kuwa mgeni katika masuala ya uongozi hasa wa kichama kwa kuwa chama kina mambo mengi ya kuwekwa vizuri na pia ni lazima wanachama wawe wanapelekwa kwa utaratibu na sio kama suala la kutumbua majipu
Wewe ndio umejaa unafiki na unaogopa Magufuli akikabidhiwa chama atakukamua usaha uliooza. Magazeti yote yameripoti sawa na mwanzisha thread na inaonyesha kabisa Kikwete na kundi la mafisadi waliopo CCM wanataka kuvuta muda ili wasitumbuliwe! Vyombo vya usalama inabidi viwe macho na hawa mafisadi wanaopinga Magufuli kuchukua uenyekiti kwani inaonekana wana ajenda isiyo nzuri!
 
Back
Top Bottom