Mvutano waanza baina ya Uturuki na Russia kuhusu Syria

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Baada za kupamba moto mivutano baina ya Moscow na Ankara kuhusiana na hali inayotawala huko kaskazini mwa Syria, Rais wa Uturuki ametangaza kuwa, nchi yake haitambui rasmi suala la kuunganishwa Rasi ya Crimea na ardhi ya Russia.

Recep Tayyip Erdoğan aliyasema hayo jana mbele ya waandishi wa habari akiwa pamoja na mwenjeji wake wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, mjini Kiev.

Erdoğan alisema kuwa hali ya Idlib nchini Syria haiwezi kudhibitiwa na kudai kuwa, zaidi ya wakimbizi milioni moja wanaendelea kuelekea kwenye mpaka wa Uturuki na kwamba suala hilo limefumbiwa macho na Russia.

Bila ya kuashiria suala la wanajeshi wa Uturuki kuingia katika ardhi ya Syria kinyume cha sheria, Erdoğan amedai kuwa, mashambulizi yaliyofanywa Jumatatu illiyopita na jeshi la Syria huko Idlib yamesababisha vifo vya watu 8, watano miongoni mwao wakiwa wanajeshi na wengine raia wa kawaida.

Matamshi ya Recep Tayyip Erdoğan kuhusu suala la kutotambua rasmi kuunganishwa eneo la Crimea na ardhi ya Russia ni msimamo wa kisiasa ambao kivitendo, hauna taathira yoyote.

Kwa msimamo huo, Uturuki inafanya jitihada za kuitia wasiwasi Kremlin kuhusiana na mustakbali wa uhusiano wa nchi hizo mbili. Pamoja na hayo Russia inaelewa vyema kwamba, Uturuki haina mabavu na uwezo wa kujitenga na Moscow au kwa uchache kwenda kinyume na siasa za Russia.

Ni zaidi ya miaka miwili sasa ambapo uhusiano wa Uturuki na washirika wake wa magharibi umevurugika, kwa kadiri kwamba, Ankara imelazimika kujikurubisha zaidi kwa Russia kwa ajili ya kupata mahitaji yake ya kijeshi ikiwa ni pamoja na kununua mfumo wa kujikinga na makombora wa S-400.

Suala hili linaifanya Ankara iwe tegemezi zaidi kwa teklonojia ya silaha ya Russia.

Katika upande wa nishati na utalii pia, Russia ina uwezo mkubwa wa kuathiri uchumi wa Uturuki.

Kwa wastani tu, Uturuki hupokea watalii milioni tano kutoka Russia. Vilevile sehemu kubwa ya nishati inayotumiwa nchini Uturuki inanunuliwa kutoka Russia.

Kwa msingi huo inaonekana kuwa, Russia haitatetereshwa na msimamo wa sasa wa Uturuki kuhusuana na eneo la Crimea ambao zaidi ni radiamali ya Ankara kuhusiana na yanayojiri sasa huko Syria.

Vilevile inatupasa kusema kuwa, hatua ya Ankara ya kutotambua rasmi suala la kuungwanishwa Rasi ya Crimea na Russia halina taathira yoyote katika msimamo wa Moscow juu ya eneo hilo.

Ama kuhusiana na hali ya medani ya vita, hapana shaka kuwa maeneo ya Idlib na Halab (Aleppo) huko kaskazini mwa Syria ni sehemu ya ardhi ya nchi hiyo na yataendelea kuwa chini ya mamlaka ya serikali ya Damascus.

Hivyo basi, hatua yoyote ya Uturuki katika maeneo hayo bila ya ushirikiano na mwafaka wa serikali ya Syria ni ukiukaji wa mamlaka ya nchi hiyo.

Hivyo basi, hatua yoyote ya Uturuki katika maeneo hayo bila ya ushirikiano na mwafaka wa serikali ya Syria ni ukiukaji wa mamlaka ya nchi hiyo. Katika mazingira kama haya Uturuki haina khiari zaidi ya ama kuondoka huko kaskazini mwa Syria na kukabidhi maeneo inayokalia kwa mabavu kwa serikali ya Damascus au kuzidisha machafuko katika eneo na kanda hii.

Kwa kutilia maanani mafanikio ya jeshi la Syria na kuendelea kukomboa maeneo zaidi ya ardhi ya nchi hiyo, inaonekana kuwa, Uturuki itaendelea kubanwa na kulazimika kuchagua moja kati ya machaguo hayo mawili.

Mkwamo na hali hii ni matunda ya siasa zisizo sahihi za serikali ya Ankara na sera zake za kuzidisha machafuko na ukosefu wa usalama nchini Syriia.

4bv57661ae19271kx8k_800C450.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo maneno ya Edorgan ni kuwapumbaza tu Ukraine na kujaribu kutumia Crimea kufunika mambo yanayoendelea huko Idlib kwani anafahamu fika kuwa Crimea ilishatwaliwa (mpaka kura ya maoni ilihalalisha utawala wa Urusi) na hakuna chochote kinachoweza kubadili hilo.
 
Naona unazidi kuviona vioja na vichekesho vya Erdogan

Kama NATO Na Kujimwambafai Kwao Kote Wamechemka Kwa CRIMEA Huyu Mpuuzi Yeye Kama Nani Anajifanya Kuipiga Biti RUSSIA

Kuna Viongozi Wanachekesha Sana Asee Hawa Angalii Hata Namataifa Wanayoyapiga Biti Basi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Uturuki siyo nchi ya kuimock kama hivyo unavyonadi maana historia inajieleza yenyewe

Angalia historian yao au uchumi wao utagundua kuwa siyo mshirika ambae Russia anataka kumpoteza kwa muda huu kwa ajili ya warabu wa Syria

Kabla ya US na GB kuwa superpowers basis kulikuwa na Ottoman Empire kuanzia Europe ya sasa, Asia hadi Afrika kote ilitawala

Situation aliyokuwana Erdogan saivi ni kama ya Kikwete kipindi cha nyuma huko Rwanda ambapo Kagame hataki kuongea na waasi huku wakimbizi wanazidi miminika kwenda nchi jirani

Mkumbuke tu wale mnao waita waasi huko Syria ni raia halali wa nchi hiyo ila walikuwa na mitizamo tofauti na serikali

Swali lakujiuliza ni kwanini raia wa Syria bado wanakimbilia kwenye trapped Idlib na wasirudi miji mingine ya karibu kama Aleppo ambayo imeshakombolewa na serikal?

Sidhani kama unajua kwann Russia anampigania Assad kwa nguvu hivi

Kiufupi ni kuwa hapo Syria kuna bomba la gesi linatakiwa lipite from Qatar to Europe na kama hilo bomba likipita basi huo ndio utakuwa mwisho wa urusi kuuza gesi ulaya so Russia yupo hapo kudhibiti hicho kitu

👊👊👊! Safi mkuu kwa kuliona hili. Uturuki nchi muhimu sana katika eneo hilo hasa katika hali ya Sasa.
 
Sidhani kama unajua kwann Russia anampigania Assad kwa nguvu hivi

Kiufupi ni kuwa hapo Syria kuna bomba la gesi linatakiwa lipite from Qatar to Europe na kama hilo bomba likipita basi huo ndio utakuwa mwisho wa urusi kuuza gesi ulaya so Russia yupo hapo kudhibiti hicho kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu swali, Crimea inaihusu nini NATO?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanakimbia kimbia kujibu swali yako hapa

Ukraine sio member wa NATO na hajawahi kuomba hata hiyo membership hadi hapo Russian alivyochukua Crimea

Sasa ndio wanaona umuhimu wa hiyo NATO na kuifanya priority katika sera zao kimataifa, hapo wakulaumiwa ni hawa UN ambaye yeye ni member na siyo NATO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanakimbia kimbia kujibu swali yako hapa

Ukraine sio member wa NATO na hajawahi kuomba hata hiyo membership hadi hapo Russian alivyochukua Crimea

Sasa ndio wanaona umuhimu wa hiyo NATO na kuifanya priority katika sera zao kimataifa, hapo wakulaumiwa ni hawa UN na EU ambaye yeye ni member na siyo NATO

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa kama Ishu Sio Memba Wa NATO Imekaaje Kwa TURKEY Ambae ni NATO Memba Alipo nunua s300 kutoka RUSSIA

Haya Ikawaje Baada Ya UK Kudai Kwamba MOSCOW Ilitaka Kumuua Jasusi wao kwa kumpa sumu katika ardhi ya UK

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom