Mvutano wa China na USA: Ni nini maoni yako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvutano wa China na USA: Ni nini maoni yako?

Discussion in 'International Forum' started by Zhule, Apr 18, 2010.

 1. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si mvutano unaoweza kuleta vita la asha. Ni mvutano wa kibiashara.Tukiacha mambo ya kuuzia Taiwan helkopta za kijeshi.

  USA wanatuhumu China kwamba wamepunguza thamani ya pesa yao. Kwa kufanya hivyo wana boost export na ku-create ajira kwao. Wanasema ubora wa bidhaa zinazozalishwa China na kusafrishwa ulaya na north America kwa sasa zinaubora sawa na bidhaa zinazozalishwa uko USA na ulaya lakini bei zake ziko chini. China wana sera za ku-subsidize bidhaa zote zinazokuwa exported abroad) (Ndo maana unaona wanataka viwanda hapa kwetu vimeshidwa competetion). Wamarekani wanasema serikali yao isipochukua hatua ajira kwao kurudi kama ilivyozamani ni ndoto. Wanasema serikali yao iliwawezesha nchi za Japan Korea kusini na sasa inafanya hivyo kwa China. Wanawauzia technology na hi-tech goods then wanaanza kujitengenezea wenyewe na kwa bei nafuu na kuuza Asia na Africa. China pia ina-enjoy tax exemption or little in north America na Ulaya kwa bidhaa zake nyingi tu zikichukuliwa ni kwa ajili ya wananchi maskini lakini kwa sasa hata middle class wanazitumia.

  Wamarekani wameanza kurespond. Moja ni kuanza kuweka masharti za ku-export high-technology kwenda China na kuweka tax kwa baadhi za bidhaa kama tyres. Obama pia ana-encourage watu wapunguze consumption za external goods na ku-increase kwa za ndani. Hizo sera za Obama Beijing hawaziafiki. Akijibu maswali kwa waandishi wa Habari kwenye press conference ya mwaka huu (inafanyika mara moja kwa mwaka) Waziri mkuu alisema uzoefu unaonyesha kwamba China na America wakiwa na mgongano nchi zote zina-loose wakiwa na mapatano nchi zote zina-gain. Anawaalika waandishi wa habari watembelee China interior wajionee wenyewe umaskini. Hapo ni katika kujibu swali la kwa nini hawako active kwenye migogoro yanayojiri duniani wakati ukiwa na nguvu majukumu nayo yanaongezeka.

  Waandishi wa habari pia waligusia ubaguzi wa viwanda vya wenyeji dhidi ya wageni vilivyopo China Wanasema hawapati viwanda vya ndani yaani za wenyeji wana-subsidized na serikali kwaiyo bidhaa zao ziko chini na wanauza sana. Vya kigeni hakuna subsidies pei ina kuwa Kwaiyo viwanda viko nchini lakini havifaidi wananchi wa wenye kipato cha chini na cha kati. Waziri mkuu anasema mwaka huu atatembelea viwanda vya wageni ili afahamu matatizo yao kwa undani.

  Anasema pesa yao itapanda kwa kadiri uchumi wao unavyokua na si kwa vigezo vya magharibi lakini ni kwa vigezo vya Beijing. Anasema 60% za bidhaa za China zinazokuwa exported zinazalishwa na viwanda vya wageni kwaiyo kuiwekea china vikwazo ni kuwawekea makampuni yao. China wanarespond pia kwa ku-encourage internal consumption kwa ku-subsidize bidhaa zinazouzwa vijijini ili watu wamudu na kupunguza uchumi kutegemea export. Karibuni wameanza kuonyesha ushirikiano kwa kushiriki mazungumzo ya kuwekea Iran vikwazo. Hii ni kuwatuliza ulaya na marekani maanake uchumi wake unategemea sana mabara hayo.

  Respond nyingine ni ku-expand export to Africa.

  Kuhusu hali ya hewa China, India na Brazil transition economies wanasema waliochafua hali ya hewa yaani nchi za viwanda wawe mstari wa mbele kupunguza CO2 emissions. Ulaya wanasema wasifanye makosa waliyoyafanya wao kuaribu zaidi bali watumie technology mbadala kwa sababu sasa hizi zipo. Wao wanasema technologia mbadala bado ni gali, chumi zao haziwezi kumudu. Wanasema wata-adopt taratibu na pia nchi za viwanda lazima zichangie gharama hizo.

  Ulaya pia kama unavyojua hivi karibuni wameanza mikakati ya kuwekeana mikataba ya kuuzia Africa kwa muda wa miaka ishirini na mitano. Hii yote ni watu kujihakikishia masoko. Kama ilivyokuwa kipindi cha ukoloni watu waligawana Africa kwa ajili ya mali ghali na masoko. Sasa ni kwa ajili ya masoko.

  Kwa maoni yenu wakuu je nani afanye nini ili ionekane ni win-win situation?

  La pili kipengele tena cha jinsi China inavyolinda viwanda vyake vya ndani imenivutia kidogo. Kwa hapa nyumbani ni sera zipi kwa mifano zinazopendelea viwanda vya ndani ili kulinda ajira?

  Nimeona karibuni kwamba cement from China, Pakistani na kwingineko pamoja na ku-incur transportation cost ni bei poa kuliko ya Tanzania sikuelewa.
   
Loading...