Mvurugano wa mambo uliopo Tanzania ni matokeo ya kuyumba kwa CCM Kisera

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Kwani hasa CCM inasimamia misingi gani sasa huwezi kupata jibu la wazi.

Tuchukue walau huu muda wa miaka 20 iliyopita utaona ukweli wa mambo. Nakusudia kutoka mwaka 2000.

Kuanzia mivutano ya Kupata mgombea wa Urais wa JMT na kuvuana magamba na kuasisiwa mitandao kulikiacha chama peupe kabisa na kila upande kujivutia na kuweka watu wao. Visasi vilishamiri na ikawa sasa misingi ya CHAMA INATAFSIRIWA NA WALIOPO MADARAKANI kwa lengo la kuwadhibiti wengine.

Hata vyama vya Upinzani vilitengenezwa na siasa ya nchi ilifuata nani yupo madarakani pale kwenye CCM. Iliyumba CCM , Taifa limeyumbishwa hii ni kutokana na Historia ya Nchi yetu na urithi wa TANU na ASP.

Hebu fikiria mivutano ya wanamtandao na kashfa ya kujiuzulu akina Mzee Lowasa na tibwili la Uchaguzi wa 2010, Serikalini kulikuwa na mvurugano wa kambi na kudhoofishana kwa kupigania madaraka na wala si nchi au Taifa. Wapambe walikingia kifua kila kitu dhidi ya Mwenyekiti kwa Kisingizio cha AMIRI JESHI MKUU . Vyombo vyote vya Dola vilifuata Mwelekeo wa rais aliyekuepo wakati Huo.

Naam hadi uchaguzi wa 2015 na mivutano yao ikatuletea Aina ya rais ambaye leo kaiacha hio legacy iliyopo. Kuingia tu naye Mzee Magufuli akatandaza wa kwake kwenye Serikali na kutengeneza CCM yake . Bunge likahodhiiwa , Mahakama ikashikiliwa na Sheria nyingi kuvurugwa mbele ya wastaafu na viongozi wakongwe wa CCM. Utafikiri sio CCM ile ile. Na Hapa napo kisa AMIRI JESHI MKUU na vyombo vyote vya Dola vikafuata mwelekeo huo na wala si wa wananchi au umoja wa kitaifa wetu. Misamiati ya Uzalendo, Wasaliti, Mafisadi ikatamalaki kuhalalisha dhulma na uvunjaji wa Sheria. Si Mwana CCM yeyote alithubutu kuinua Mdomo utafikiri akili zilienda likizo. Mambo yakavurugika kuhusu Uendeshaji wetu wa Nchi na sasa ndio hio picha iliyopo.

Utashangaa nini leo Vyama vya Upinzani na Wapinzani kuteswa, watu kubambikiziwa kesi, Sheria kutofuatwa, Ubabe wa Viongozi, Vyombo vya Dola kukiuka misingi yake , mauaji , kutesana, n.k. Nani angehoji? Ina maana CCM haikuwa na Responsibility kwa Serikali yake hadi haya yakatokea? Jibu ni kuvurugikwa kwa CCM. Waliokuwepo madarakani kwenye CCM ndio hao wana mtandao au supporters wa Huyo Rais na Mwenyekiti. Wengine waliufyata na Kuogopa Rungu la Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa Chama. Wengine walisemea kwenye vibubu na huko huko walidukuliwa . Hii ni dhahiri kama Chama tawala, kama mtawala kuishiwa.

Mdogo Mdogo 2021 baada ya Kufariki Mzee , Leo Mama na Rais unamuona hivyo alivyo. Analazimika kuwepo katikati tu bila kutarajia. Anajua mabaya yote ya Uongozi wa awamu ya Tano na ana ramani yake lakini anashindwa kuwa Direct kutokana na mifumo kujawa na Supporters wa Kiongozi aliyepita. Wanajuana na kila mmoja ana hofu juu ya mwenzake. Hao wote ni CCM tunayoambiwa ni moja na yenye ITIKADI. Mivurugano yao na hofu zao zinayumbisha nchi yetu na hadi vyombo vya kutoa HAKi, Bunge na Vyombo vya Usalama.

Imefika wakati, CCM inasaidiwa kazi na Polisi ya kudhibiti Wapinzani badala ya jumuiya zake kukosa uwezo na uhalali wa kisiasa. Hakuna tena wajenga hoja na ushawishi wa kuvuta hisia za watanzania. Kuna CCM mpya iliyofuata kila Mwenyekiti alichotaka na kuacha misingi yetu. Mama wa Watu unamuona anaujua ukweli lakini analazimika kuufyata tu.

Kazi ya kulindana imekuwa ndio Desturi ya CCM kwa kila awamu baada ya awamu. Viongozi waliopo wanalazimika kula matapishi na kumeza maovu yote yaliyotengenezwa na waliopita. Ushawishi wa kuwaaaminisha watanzania umepotea sasa wanatangulizwa Polisi kupiga mikwala, Mahkama, Bunge la CCM na Vyombo vyengine vya Dola.

Diplomasia yetu inashindwa kuwa Direct, tunalazimika kuchanganya Unafiki ili maisha yaende. CCM inajifanya haioni haya na hakuna wa kukosoa.

Mambo ni mengi. Ufupi wa Maneno ni kwamba CCM ilishavurugika kitambo, Sasa Tanzania inapitia hii hali iliyopo kutokana na CCM.

Mfumo wetu wa Elimu, Mahkama, Uajiri, Bunge , Utendaji wa Vyombo vya Dola vimeathiriwa na UCCM na Makandokando yake ndio leo ukaona Hakuna Chombo kinamsimamia Mwenzake Kuinyoosha nchi na Mshikamano wetu wa kitaifa. Sana sana ni kukingiana kifua.

Katika Mazingira hayo ya Kudhoofika kwa CCM katika Udhibiti wa NChi kwa Maana pana ya Dhana ya Taifa kuendelea kijamii, kisiasa, na watu wake bila upendeleo , ndio leo ukaona kila kitu hakiendi. Ndani ya CCM kuna Tatizo la msingi la ATHARI ZA MAKUNDI. Huyu ndie Adui Mkubwa wa Tanzania. Mazingira hayo yanajenga Uadui wa KUDUMU NA HOFU ZA KUPIKUANA.

Ndio yanajenga hisia na maamuzi ya kupitisha sheria kandamizi na kutumia ubabe, kuvunja sheria n.k ili kudhibiti hali. Hatima yake ndio Tanzania nayo inavurugika kwa sababu ya kuvurugika kwa CCM.

Ili kuondokana na hilo na kungoa mizizi hii ya Uadui kwa wananchi na ndani ya CCm kwenyewe tunahitaji kuanza UPYA. Kuanza Upya kutapatikana kwa kuja KATIBA MPYA.

Kwa Mtazamo wangu Hili ni hitajio la wakati. Wakati unaonesha kuvurugika kwa CCM ambayo haiko tayari kuondoka Madarakani ilihali yenyewe imeshavurugika. Na kwa Asili na Historia Yake ilivyojichimbbia kwenye Dola visasi na kulipizana hakutoisha mpaka tutaka[poamua kusimika Upya mfumo wetu wa kujitawala.

Katiba Mpya ndio Tanzania mpya.


Kishada.
 
Katiba mpya haiepukiki maana wanasiasa wanaugusa mfumu wa kiuchumi wa taifa kwakutengeneza sera ambazo hazina tija na zinazo badirika barika. 'Ineffective policies, uncertainty policies' and herding behavior in decision making and economy
 
Back
Top Bottom