Mvurugano nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki: Je, Bahima Empire inafitinishwa?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
156,324
2,000
Miaka 5 ya awamu ya tano inafikia tamati na pigo toka kwa nchi mwanachama kuweka katazo la bidhaa za jirani na mwanajumuiya zisiingizwe nchini mwake...Rwanda imepiga marufuku bidhaa za Tanzania zisiingie tena nchini mwake na sasa anataka na kufunga mpaka wa Rusumo

Migongano ipo popote na hata kwenye jumuiya kubwa kama hii haiwezi kukosekana.. Migongano na migogoro ipo mahali popote hata ndani ya familia...tatizo sio migogoro...!!! Tatizo ni namna ya kutatua tatizo linapotokea ama kuviwahi viashiria vya tatizo kabla halijamea

Hapa tutoke kidogo nje ya mipaka yetu ..tujadili siasa za kikanda, mahusiano na majirani na ushirikiano ndani ya jumuiya kubwa ya Africa mashariki...kwa hii miaka mitano jumuiya imekumbwa na migongano ya hapa na pale

Uganda na Kenya kuhusiana na mradi mkubwa wa bomba la mafuta...Uganda waliwachomolea Kenya dakika za mwisho na kupewa Tanzania...hii ilimuuma sana Kenya ambaye naye sasa anamcheka Mganda baada ya mradi husika kufunikwa na sintofahamu kubwa...!!!
Uganda na Rwanda.... Ishu ya wakimbizi na kufadhili ama kuhifadhi vikundi vya wapiganaji wenye nia ya kupindua serikali za mataifa husika

Kenya na Tanzania kuanzia kuchomeana bidhaa hai, kutaifisha mifugo ama kupiga faini kubwa mpaka kufikia kuwekeana makatazo ya kibiashara kwenye usafiri wa anga kisingizio kikiwa covid-19

Burudi na Rwanda ishu ya makundi yanayopinga serikali zao..tuhuma za kuhifadhi na kufadhili makundi husika

Lililo jipya ni hili la Tanzania na Rwanda kuhusu bidhaa na inavyoelekea mambo yanakwenda kwa haraka mno....lakini ninini kimetokea kati ya haya mataifa mawili? Jirani halafu wanajumuiya moja?

Mwanzoni mwa awamu ya tano mahusiano yetu yalikuwa ni mazuri sana mpaka redio mbao zikawa zinasema yake

Ya kwamba
Ushauri wa kununua ndege tena kwa cash tuliupata Rwanda

Ya kwamba
Ukuta wa Mererani lilikuwa ni wazo la Rwanda na eneo lote likawa linalindwa na wanajeshi wa Rwanda

Ya kwamba
Rais alikuwa na ulinzi maalum toka Rwanda

Ya kwamba
ushawishi wa Rwanda na ukaribu wa viongozi wakuu ndio uliochochea reli kujengwa kwenda Rwanda nchi ya watu wasiozidi milion kumi na kuacha kuipeleka Kongo nchi yenye watu zaidi ya milion mia

Ya kwamba
Mradi wa ujenzi wa bandari kavu eneo la Ruvu mizani na miundo mbinu ya moja kwa moja mpaka airport na bandarini ni ushawishi wa Rwanda kwa ajili ya mizigo yake

Sasa kama yote haya ni kweli ....ninini kimetokea all of a sudden!? Kuna wambea wanasema chinichini ni uhuni aliofanya rais wa Rwanda kwenye madini...kwamba alipiga mzigo wa kutosha na kusepa nao kihuni....zile za kimjinimjini.

Pamoja na kwamba sababu kubwa ni covid-19 ...kwakuwa kama jumuiya hawakuwa na sauti moja kwenye kukabiliana na hilo gonjwa na kila mtu akatenda kivyake

Mwanzoni wananchi wa nchi jumuiya walitishwa kuwa viongozi wao wana andaa kitu kinachoitwa BAHIMA EMPIRE na wanahakikisha hiyo ndoto inafanikiwa..hicho ni kipindi ambacho viongozi walikuwa wanatembeleana na kufanya mijadala pamoja
Viongozi walikuwa wanaalikana kwenye matendo ya furaha na huzuni pia.

Kwasasaa jumuiya ni kama imekuwa mfu...likitokea jambo lenye manufaa hasa kiuchumi wanaanza choyo na ubinafsi na kufanyiana hila
Zikitokea changamoto za usalama na mambo ya kisiasa wanaaza kunyoosheana vidole na kutuhumiana wenyewe kwa wenyewe.

Kule kutembeleana na kupeana zawadi kumekoma...covid inaweza kuwa kisingizio lakini nyuma ya pazia kuna picha kubwa zaidi isiyotolewa hadharani na pengine hii ndio inayofitinisha ile ndoto kubwa na ya muda mrefu ya kuwa na BAHIMA EMPIRE.!!
Lakini katika wote hawa MFITINI mkubwa ni nani!? Muda utasema..!!
 

911sep11

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
2,363
2,000
Unajua bila picha hainogi
Museveni-and-kagame-visit.jpg
 

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,110
2,000
Nimetumia neno redio mbao kwakuwa haikuwahi kuthibitishwa popote
Binafsi Babu zangu wametokea Rwanda, na nimebahatika kufanya kazi Rwanda kule ziwa KIVU katika miradi wa kuzalisha umeme wa GESI ya METHANE nimefanya kazi kwa siku 87 hii jamii ya ipo Smart sana na ukweli nikuwa Rwanda imefanya wizi mkubwa wa madini kutoka Congo.

Bahati nzuri ni kuwa wao wanaiba wanafanya maendeleo makubwa kujenga nchi yao sisi tunachimba ya kwetu hatuna faida nayo wanabeba mabwenyenye na kugawana na mafisadi.

Tuna la kujifunza kutoka kwa bahma (Tutsi) maana bahma ndio imefanya ustaarabu wa East Afrika imeleta challenge katika Elimu ndio maana KAGERA ndio mlango wa ELIMU ya TANZANIA ukitaja ustaarabu wa Tanzania bila KAGERA bado haujakuwa sahihi hata HAYATI BABA WA TAIFA (MZANAKI) NI JAMII YA BAHMA

Hapa tunapata kuwa ustaarabu wa Afrika unatokana na Bahma maana BABA WA TAIFA (J.KAMBARAGE) amechangia pakubwa katika ustaarabu wa Afrika na ni damu ya Bahma.
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
12,029
2,000
Na we ni bahima..
Binafsi Babu zangu wametokea Rwanda, na nimebahatika kufanya kazi Rwanda kule ziwa KIVU katika miradi wa kuzalisha umeme wa GESI ya METHANE nimefanya kazi kwa siku 87 hii jamii ya ipo Smart sana na ukweli nikuwa Rwanda imefanya wizi mkubwa wa madini kutoka Congo.

Bahati nzuri ni kuwa wao wanaiba wanafanya maendeleo makubwa kujenga nchi yao sisi tunachimba ya kwetu hatuna faida nayo wanabeba mabwenyenye na kugawana na mafisadi.

Tuna la kujifunza kutoka kwa bahma (Tutsi) maana bahma ndio imefanya ustaarabu wa East Afrika imeleta challenge katika Elimu ndio maana KAGERA ndio mlango wa ELIMU ya TANZANIA ukitaja ustaarabu wa Tanzania bila KAGERA bado haujakuwa sahihi hata HAYATI BABA WA TAIFA (MZANAKI) NI JAMII YA BAHMA

Hapa tunapata kuwa ustaarabu wa Afrika unatokana na Bahma maana BABA WA TAIFA (J.KAMBARAGE) amechangia pakubwa katika ustaarabu wa Afrika na ni damu ya Bahma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom