Mvunja nchi ni Mwanasiasa na Kiongozi wa Kidini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvunja nchi ni Mwanasiasa na Kiongozi wa Kidini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jun 6, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa na hata kiongozi wa kidini. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi binafsi na ya kundi dogo badala ya yale ya kitaifa.

  Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Hili ni jambo la hatari sana.

  Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao. Kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.

  Wahenga walisema ”kamba hukatikia pabovu”. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa.


  Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania.
  Mungu Ibariki Tanzania.


  Maggid Mjengwa,
  Iringa.
   
 2. mgashi

  mgashi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 304
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Na kwanini iwe kwa maslahi ya kundi fulani na isiwe kwa ajili ya kupigania kwa ajili ya watanzania wote? wahusika acheni kupalilia mbegu mbaya ya udini mnako tupeleka ni mungu tu ndo anaejuwa.
   
 3. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hakuna vita mbaya kama ile ya dini, huwa haishi kizazi na kizazi, tusiruhusi dini iwe chinjio ya damu zetu , tupinge mapema kabla mambo hayajawa mabaya sana.
   
 4. A

  Albimany JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Usisahau na taifa moja kujifanya kubwa mbele ya mwenzake. Ni hatari mbeleyetu.
   
Loading...