Mvua zitaanza kunyesha Kuanzia tarehe 18 Mpaka 26 Mwezi huu ingawaje hazitakuwa nyingi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
MVUA ZITAANZA KUNYESHA KUANZIA TAREHE 18 MPAKA 26 MWEZI HUU INGAWAJE HAZITAKUWA NYINGI

Anaandika, Robert Heriel,
Mwanajiografia

Hali ni Tete Kwa sehemu ya nchi kuwa na uhaba wa mvua. Hii ni kusema kuna janga la ukame kinaendelea.
Kijiografia Mvua zilipaswa zianze mwezi mmoja baada ya jua kuingia Ikweta 21September hivyo ingepaswa mvua kuanza kunyesha tarehe 20/21 oktober kukaribisha mvua za vuli ambazo zingedumu Kwa siku 60, siku hizo zingetosha kuyaotesha baadhi ya mazao Kama mahindi, ambayo Kwa siku hizo 60 yatakuwa yamefikia ukuaji wa mpaka kuonyesha mbelewelu na kukomaza mahindi. Hii ni kutokana na sababu kuwa mazao mengi huchukua siku 60 - 90 kukomaza mazao/matunda yake.
Kjiografia siku hizo 60-90 ni msimu unaojiyosheleza kabisa.

Mvua kiasi ilitarajiwa kunyesha tarehe 01-08november sio ajabu muda huu Maeneo mengi yana-expirience joto jingi.

Wakati huu ndio msimu wa Ndege kuruka makundi makundi na wakati WA Ndege kuchagua makazi yao mapya ya kujenga viota vyao. Kwaajili ya kujiandaa na miezi ya January.
Hata hivyo hii haihusishi Ndege waliojenga viota vyao kwenye majumba ya watu ambao wao hutaga tofauti na Ndege wajengao viota kwenye miti.

Sasa mvua hazijanyesha Kwa Maeneo mengi ya nchi. Na zilizonyesha ni kidogo Sana.

Tuliosoma Jiografia na kuielewa tunaweza kuona kuwa mvua zilizobakia Kwa mwaka huu zinaratiba kama ifuatavyo;

i. 18 - 26 November
Wiki hiyo mvua zitanyesha Maeneo mengi ya nchi.
Sababu kuu za mvua kuonyesha wiki hiyo
a) Itakuwa ni katikati ya msimu wa mbili
b) itanyesha mvua ya kuivisha maembe na matunda yote ya msimu wa Vuli.
c) kutakuwa na mwandamo wa mwezi. Hivyo mvutano wa mwezi wa Dunia mara nyingi hupelekea Unyevuunyevu angani na kusababisha mawingu, ambayo Kwa misimu ya masika na vuli hupelekea mvua kubwa kunyesha.
Kwa misimu ya kiangazi na Baridi mvutano wa mwezi hupelekea manyunyu kiasi au mvua ambayo haijabalehe kunyesha.

ii. Tarehe 8-16December
Wiki hii mvua itanyesha ingawaje haitakuwa kubwa kama ya November 18-26.
Hii itakuwa ni Nusu ya mwezi wa mwisho wa msimu wa vuli.

iii. Tarehe 23 - 29 December
Mvua itanyesha kumaliza msimu wa vuli. Pia jua litakuwa limeshafika kizio cha kusini/Tropical ya Kaprikoni hivyo litakuwa linageuza Kurudi Ikweta.
Mvua itanyesha kukomaza mimea iliyooteshwa Mwanzoni mwa msimu WA vuli.
Kama ni Wakulima wale wakutegea mvua basi itawapasa wapanda mimea Yao kuanzia tarehe 14-18 November

iv. Tarehe 07-15 January 2023
Hii itakuwa mvua ya kuuaga msimu wa vuli . Jua litakuwa linasiku 15-20 tangu liache kizio cha Kusini.
Mvua ya hapa itakuta mimea mingi imechanua au itanyesha ili mimea hiyo ichanue itoe Maua Kwa ajili ya uchavushaji.
Mvua hizi hazitakuwa nyingi kwani nature itazifanya inyeshe kwa lengo la kutoa Maua.

Kisha jua la mwezi wa Kwanza litayasaidia Maua hayo pamoja na nyuki kufanya tendo la uchavushaji.
Jua litakuwa Kali hali na joto la usiku litaongezeka Hali itakayofanya Asubuhi mimea iwe na umande ili kuivisha na kukomaza mazao yaliyokuwa kwenye mimea ambayo yalipandwa Kwa wakati.
Wakati huo Ile mimea iliyochelewa kupandwa ikijikuta katika Hali ngumu ya ukosefu wa Maji. Hali itakayopelekea kukauka.

Hapo Msimu wa Vuli utakuwa umeisha, na Mavuno ya Vuli yatavunwa January 18 Mpaka February 10 kutegemea na Aina ya mazao ya mmea husika.

Mambo yanayotarajiwa ni haya;
i. utakuwa ni msimu wa Ndege kujenga viota vyao kujiandaa kutaga. Hivyo Ndege wengi mwezi January mwanzo watakuwa na mayai ili mpaka msimu wa mavuno mayai hayo yawe yameanguliwa. Hii itawasaidia Ndege kulisha makinda Yao Kwa urahisi. Hata hivyo ninaposema mazao ya mimea sio tuu mimea yakuliwa na binadamu Bali hata mimea ya kondeni inayoliwa na wadudu na Ndege.

2. Wadudu watambaao Kama jamii za sisimizi, chungu, siafu n.k wataongezeka maradufu mwezi January Kwa lengo la kujenga makazi Yao na kukusanya chakula cha akiba wakijiandaa na msimu wa masika ambapo mvua kubwa hunyesha hivyo hujificha katika majengo waliyoyajenga mwezi January na Kula chakula walichokikusanya mwezi January mwishoni.

3. Joto litaongezeka maradufu Kama miaka mingine ilivyo. Mwezi January mwishoni mpaka mwezi watatu kwani jua litakuwa linarejea Ikweta.
Hivyo kutakuwa na Jua kama unavyoliona jua la November oktober 22- November 15.
Kama jua na joto la muda huu.

Mambo ya kufanya ili kufanya nature ifanye kazi vizuri;
1. Serikali iandae mpango mkakati WA kupanda miti. Iweke Sera na sheria Kwa nchi nzima kuwa kila nyumba iwe na wastani wa miti miwili. Na kila mtu apande mti moja

2. Serikali iweke sheria Kali kuwa sio ruhusu Kwa mtu kukata mti wowote bila kupewa kibali maalumu.

3. Vyombo vya habari na watu mashuhuri wenye ushawishi wapewe agenda ya kupromoti utunzaji wa miti na mazingira.

4. Mitaala ya elimu iweke mada ya elimu ya utunzaji wa Mazingira kila Darasa mwanafunzi akiingia mpaka Chuo kikuu.

5. Serikali iweke sheria kuwa Maeneo ya kutotelea Huduma za umma yote bila kujali ni ya kiserikali au kibinafsi au mashirika yawe na idadi Fulani ya miti kadiri Wataalamu WA Mazingira watakavyoshauri.

6. Mamlaka za ujenzi wa makazi iweke sheria za mipangilio ya makazi ili kutoa nafasi Kati ya nyumba na nyumba na kuacha sehemu za wazi ili Kupunguza joto katika miji.

7. Utupaji wa taka usimamiwe kikamilifu na wapewe jukumu watu au makampuni yenye Elimu ya kutosha ya mazingira au waliosomea kozi zenye masuala ya environmental protection and conservation.

8. Viongozi wa dini wapewe jukumu la kuhamasisha watu wapende mazingira na Kupanda miti.

9. Serikali isisitize mpango wa kutumia nishati mbadala nje ya mkaa Kwa kutoa elimu na Kupunguza gharama za nishati hizo

Ni Yule Kuhani kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
ii. Tarehe 03-08 December
Wiki hii mvua itanyesha ingawaje haitakuwa kubwa kama ya November 18-26.
Hii itakuwa ni Nusu ya mwezi wa mwisho wa msimu wa vuli.

iii. Tarehe 20 - 27 December
Mvua itanyesha kumaliza msimu wa vuli. Pia jua litakuwa limeshafika kizio cha kusini/Tropical ya Kaprikoni hivyo litakuwa linageuza Kurudi Ikweta.
Mvua itanyesha kukomaza mimea iliyooteshwa Mwanzoni mwa msimu WA vuli.
Kama ni Wakulima wale wakutegea mvua basi itawapasa wapanda mimea Yao kuanzia tarehe 14-18 November

iv. Tarehe 01-05 January 2023
Hii itakuwa mvua ya kuuaga msimu wa vuli . Jua litakuwa linasiku 15 tangu liache kizio cha Kusini.
Mvua ya hapa itakuta mimea mingi imechanua au itanyesha ili mimea hiyo ichanue itoe Maua Kwa ajili ya uchavushaji.
Mvua hizi hazitakuwa nyingi kwani nature itazifanya inyeshe kwa lengo la kutoa Maua.

Kisha jua la mwezi wa Kwanza litayasaidia Maua hayo pamoja na nyuki kufanya tendo la uchavushaji.
Jua litakuwa Kali hali na joto la usiku litaongezeka Hali itakayofanya Asubuhi mimea iwe na umande ili kuivisha na kukomaza mazao yaliyokuwa kwenye mimea ambayo yalipandwa Kwa wakati.
Wakati huo Ile mimea iliyochelewa kupandwa ikijikuta katika Hali ngumu ya ukosefu wa Maji. Hali itakayopelekea kukauka.

Hapo Msimu wa Vuli utakuwa umeisha, na Mavuno ya Vuli yatavunwa January 18 Mpaka February 10 kutegemea na Aina ya mazao ya mmea husika.

Mambo yanayotarajiwa ni haya;
i. utakuwa ni msimu wa Ndege kujenga viota vyao kujiandaa kutaga. Hivyo Ndege wengi mwezi January mwanzo watakuwa na mayai ili mpaka msimu wa mavuno mayai hayo yawe yameanguliwa. Hii itawasaidia Ndege kulisha makinda Yao Kwa urahisi. Hata hivyo ninaposema mazao ya mimea sio tuu mimea yakuliwa na binadamu Bali hata mimea ya kondeni inayoliwa na wadudu na Ndege.

2. Wadudu watambaao Kama jamii za sisimizi, chungu, siafu n.k wataongezeka maradufu mwezi January Kwa lengo la kujenga makazi Yao na kukusanya chakula cha akiba wakijiandaa na msimu wa masika ambapo mvua kubwa hunyesha hivyo hujificha katika majengo waliyoyajenga mwezi January na Kula chakula walichokikusanya mwezi January mwishoni.

3. Joto litaongezeka maradufu Kama miaka mingine ilivyo. Mwezi January mwishoni mpaka mwezi watatu kwani jua litakuwa linarejea Ikweta.
Hivyo kutakuwa na Jua kama unavyoliona jua la November oktober 22- November 15.
Kama jua na joto la muda huu.

Mambo ya kufanya ili kufanya nature ifanye kazi vizuri;
1. Serikali iandae mpango mkakati WA kupanda miti. Iweke Sera na sheria Kwa nchi nzima kuwa kila nyumba iwe na wastani wa miti miwili. Na kila mtu apande mti moja

2. Serikali iweke sheria Kali kuwa sio ruhusu Kwa mtu kukata mti wowote bila kupewa kibali maalumu.

3. Vyombo vya habari na watu mashuhuri wenye ushawishi wapewe agenda ya kupromoti utunzaji wa miti na mazingira.

4. Mitaala ya elimu iweke mada ya elimu ya utunzaji wa Mazingira kila Darasa mwanafunzi akiingia mpaka Chuo kikuu.

5. Serikali iweke sheria kuwa Maeneo ya kutotelea Huduma za umma yote bila kujali ni ya kiserikali au kibinafsi au mashirika yawe na idadi Fulani ya miti kadiri Wataalamu WA Mazingira watakavyoshauri.

6. Mamlaka za ujenzi wa makazi iweke sheria za mipangilio ya makazi ili kutoa nafasi Kati ya nyumba na nyumba na kuacha sehemu za wazi ili Kupunguza joto katika miji.

7. Utupaji wa taka usimamiwe kikamilifu na wapewe jukumu watu au makampuni yenye Elimu ya kutosha ya mazingira au waliosomea kozi zenye masuala ya environmental protection and conservation.

8. Viongozi wa dini wapewe jukumu la kuhamasisha watu wapende mazingira na Kupanda miti.

9. Serikali isisitize mpango wa kutumia nishati mbadala nje ya mkaa Kwa kutoa elimu na Kupunguza gharama za nishati hizo

Ni Yule Kuhani kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mkuu habari njema hii kupitia dhana ya kisayansi na kijografia. Pia hata nabii/mtume Mwambosya naye katoa utabiri akiwa Tabora wa kulifungua anga la Tanzania ili mvua inyeshe.

Kwa hakika hizo ni habari njema sana masikioni mwa watu wote wenye mapenzi mema na Watanzania, hasa wakulima.
 
Mvua za mwaka huu zitasogea kidogo mpaka January kwenye Juma la Kwanza
 
Mvua zilivo chache inabidi mwaka huu nipande Bangi ili kukimbizana na msimu, serikali ishauri mazao yanayokomaa kwa muda mfupi yalimwe kwa wingi
 
Back
Top Bottom