Mvua zinazoendelea Tanzania ni neema na ni funzo kwa wakandarasi feki na watawala wapenda 10%

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,434
2,000
Wana JF
Umuofia kwenyu,

Tanzania siku za nyuma ilikuwa na ukame wa kutisha, mifugo ilikufa sana hata wanyama wa porini nao walikufa. Tuliimizana sana kupanda miti kuondoa majangwa, watu waliitikia, sasa mvua inanyesha kila mkoa ni jambo la neema na kumshukru Mungu.

Nchi yetu imegubikwa na rushwa, hatuna wazalendo kabisaa, mvua zinazoendelea zinatuonyesha miundombinu mibovu ambayo wasimamizi wake aidha walichukua wakandarasi feki au rushwa ilitamalaki wakajenga vitu vinavyokinzana na uhalisia wa mazingira.

Kila siku tunashuhudia barabara zikibomoka. Wamejenga madaraja mabovu, barabara zimepunjwa vifusi zinaelea, mikondo ya maji inazidiwa hii yote ni kwa sababu ya 10% au ma-engineer feki.

Juzi tuliona Rais wetu akitaka kumtumua waziri, mwaka juzi tuliona Makonda akiwasimamisha makandarasi lakini baadae waliachiwa waendelee sijui naye alipata hiki kijiti au mule amekuta ni kampuni za wakubwa wake.

Sasa hivi barabara za mitaani zimefumuka vibaya lakini za Tanroad zina uhafadhali sijui TARURA ndio kuna mulungula zaidi mpaka wanapata kandarasi hovyo.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
9,281
2,000
Msala aliokutana nao Mfanya biashara Ramadhani Ntunzwe ni uthibitisho kuwa nchI hii Rushwa imeshamiri kiasi kikubwa kwa awamu hii ya tano.
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,434
2,000
Msala aliokutana nao Mfanya biashara Ramadhani Ntunzwe ni uthibitisho kuwa nchii Rushwa imeshamili kiasi kikubwa kwa awamu hii ya tano.
Makonda siku hizi anaishi kwa vijembe na kuomba kazi ya kuwafinyanga wapinzani badala ya kukagua kinachokwamisha maji kwenye mitaro.

Muda wa makandarasi kukabidhi barabara zilizokamilika.
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,277
2,000
Mliambiwa tangu mwanzo habari za mtu huyu mkageuka kuwa wapiga mapambio na kusifu hata akilala juu ya mawe! Mtu huyu alikuwa ndani ya biashara ya kandarasi kwa miaka 15+ na kapiga hiyo10% za kutosha na hata Sasa anapiga you bila kuangalia na hakina wa kumuuliza Wala kuhoji!

Waziri unafokewa hadharani na kuomba msamaha as if amekosea yeye ilihali ni rafiki wa mtu huyu ndiye mkosaji!
Na Mungu alivyo wa ajabu anayafunua .adhambi yake polepole ili kuwadhihirishia kuwa mtu huyu hakuwa na hajawahi kuwa msafi hata siku moja! La miundombinu ni moja, mengine yatafuatia tu!
 
duu hii ngumu kumeza
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom